Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Ndege ya kwanza ya Riyadh Air aina ya Boeing 787-9 #Dreamliner imepakwa rangi. Shirika hilo linamilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF), Riyadh Air itanunua Boeing 787-9 Dreamliner 39 ikiwa na chaguo kwa ndege 33 za ziada.

Taarifa ya:
@aeronews
Video: Bei Facebook anmelden
FB_IMG_1685898528320.jpg
FB_IMG_1685898533906.jpg
FB_IMG_1685898537010.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
AirLander 10, awali ilijulikana kama Hybrid Air Vehicle (HAV 304) iliundwa kwa ajili ya mpango wa Jeshi la Marekani la Long Endurance Multi-intelligence Vehicle (LEMV).
Safari yake ya kwanza ilifanyika mwaka 2012 huko Lakehurst, New Jersey, Marekani.

Mnamo 2013, mradi wa LEMV ulifutwa na Jeshi la Marekani na ilipata tena kurejeshwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Cardington nchini Uingereza, na kurekebishwa kwa matumizi ya kiraia, na katika hali hiyo ilipewa jina upya la Airlander 10.

Airlander 10 ilirekebishwa na kuidhinishwa majaribio ya usanifu kabla ya kusimamishwa mradi baada ya ajali ya upepo mkali ulisababisha hitilafu upande wa mbele tarehe 18 Novemba 2017 huko Cardington.

Airlander 10 inapaa kwa kutumia lifti ya 'aerostatic' na 'aerodynamic' na inaendeshwa na propela nne zinazoendeshwa na injini ya dizeli.

Airlander 10 inaweza kubeba hadi abiria 90, kubeba vifaa vya mawasiliano na uchunguzi na wafanyakazi kwenye misheni ya ulinzi na usalama na ubebaji mizigo hadi tani 10.

Airlander 10 imeratibiwa kukamilisha uidhinishaji mwishoni mwa 2024 na kuingia katika huduma ya kibiashara mnamo 2026.

Chanzo:
Wikipedia
FB_IMG_1685899544228.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
In 1990, the windshield of British Airways Flight 5390 came off at an altitude of 17,000 feet. This triggered a sudden decompression in the cockpit, resulting in the captain being partially ejected out of the aircraft.

As luck would have it, Nigel Ogden, a flight attendant, was… twitter.com/i/web/status/1…
20230607_070204.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
In 1990, the windshield of British Airways Flight 5390 came off at an altitude of 17,000 feet. This triggered a sudden decompression in the cockpit, resulting in the captain being partially ejected out of the aircraft. As luck would have it, Nigel Ogden, a flight attendant, was on his way into the cockpit at that moment. He managed to grab hold of the captain and maintain his grip for over 20 minutes while the copilot attempted an urgent landing. Although the majority of the crew presumed that the pilot had already lost his life, Ogden did not let go. There was a prevailing fear that if Ogden did release his hold, the pilot's body might strike the plane's engine, wing, or stabilizer, causing even more chaos. All Ogden knew was that the pilot was gradually slipping more and more out of the window and his head was continuously being battered against the airplane's body. Finally, after a distressing 20-minute flight with a gaping window, the aircraft was safely brought down at Southampton Airport. In the course of events, Ogden suffered from frostbite on his face, damage to one of his eyes, and a dislocated shoulder. In a miraculous turn of events, the pilot survived the ordeal, although he had frostbite and multiple fractures on his arms and hands. The image is a recreation from the television series "Mayday!"

FxfB0M7aIAETUB-.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NDEGE ZISIZO NA INJINI (Glider)

Glider ni aina maalum ya ndege ambayo haina injini.
Kuna aina nyingi za glider, hata ndege tunazounda kwa karatasi na kurusha ni mfano mzuri.
Pia ndege nyingi zenye injini uundwa kwa asili ya kuelea angani (Gliding) hata pasipo msukumo wa injini.

Mfano, Space Shuttle ilikuwa inarudi duniani kama glider (pasipo kutumia injini) kwa kuwa injini za roketi hutumiwa tu wakati wa kuinuliwa kutoka ardhini na matumizi mengine nje ya dunia (space).

Hata Ndugu wawili #WrightBrothers walipata uzoefu wa kuunda ndege ya kwanza kutumia injini kwa kupitia majaribio kadhaa kutengeneza mifano ya glider kuelea mnamo 1900 hadi 1903.

Katika upaaji 'Glider' ina kani 03 ikilinganishwa na kani 04 katika ndege zenye Injini.

Aina zote mbili za ndege,(Glider na zenye injini) zinakabiliwa na nguvu za kuinua (lift), kuburuta(Drag), na uzito(weight/Gravity) isipokuwa ndege inayoendeshwa na injini inazidi kani moja ya msukumo wa injini (Thrust).

Ili Glider ipae lazima ipate kianzio cha nguvu kukabiliana na uzito wake, hivyo basi 'Glider' nyingi huvutwa kwa kamba na ndege yenye injini hadi angani na baada ya kupata nguvu fulani inayohitajika, kamba hukatwa, hapo glider kuendelea kuelea nyenyewe

Kumbuka lakini Glider haina injini ya kuipa msukumo kwenda mbele ili mbawa zizalishe lift hivyo nguvu ya kuanzia inahitajika.

Mfano, kwa glider zetu za karatasi hupata nguvu ya kwenda mbele kwa kuirusha.
Glider nyengine marubani huanza kwa kuruka kutoka upande wa kilima au mwinuko mkubwa.

Je! Glider inawezaje kuelea angani kwa masaa pasipo kushuka chini?

Jibu ni kwamba, ndege hizo zimeundwa kuwa na ufanisi mzuri wa kuelea (gliding) na kushuka polepole sana kwakuwa mlinganyo tofauti kati ya mbawa na kitovu cha mvuto au 'Center of Gravity' hivyo angani hufanya tabia ndogo ya kuinama upande wa mbele ambayo huipa mwendo mdogo huku mbawa zake ndefu isivyo kawaida kuendelea kuzalisha lift.
Lakini hivyo haitoshelezi kukaa angani kwa hadi saa tatu au zaidi.

Ikiwa angani, Rubani hutafuta vifuko vya hewa 'air pockets' inayopanda juu ambavyo huitwa #updraft.

Vifuko hivyo hupatikana wakati upepo unaovuma kwenye mlima/vilima kupanda juu, ambapo rubani hutumia faida hiyo kunyanyuliwa juu zaidi.

Pia rubani hupaa maeneo yenye ardhi yenye asili ya weusi ambayo inanyonya joto kali kutoka kwenye jua.
Hewa au vifuko vya hewa katika maeneo hayo hupata joto kirahisi hivyo hutanuka, kuwa nyepesi na kupanda juu.
Hewa hiyo huitwa #Thermals.

Matumizi ya hewa hizo ni darasa la asili tunalosoma kutoka katika viumbe hai.
Ndege wengi wakubwa kama Tumbusi na mwewe mara nyingi huonekana wakizunguka maeneo hayo ili kupata kuelea kirahisi bila kuchapa mbawa zao.
Glider hufanya pia.

Glider inaweza kupakia mtu mmoja au wawili kulingana na ukubwa na ni ndege maalumu kwaajili ya starehe na burudani ya kujivinjari angani.

Kumbuka pia, pamoja na kukosa injini, ndege hii ina 'control' zote muhimu (vielekezi) kama ilivyo ndege ya kawaida

#Admin
 

Attachments

  • FB_IMG_1686186121341.jpg
    FB_IMG_1686186121341.jpg
    17.2 KB · Views: 6
Ilyushin II-96 ni ndege ya kwanza umbo pana ya iliyoundwa kipindi cha Umoja wa Kisovieti, kutokea Ilyushin II-86.
Tofauti na mtangulizi wake, II-96 ina uwezo wa kwenda masafa marefu na ina vifaa vya teknolojia ya kisasa. Imewekwa vijimbawa (Winglets) pamoja na cockpit ya vioo vya elektroniki na teknolojia ya udhibiti wa ngamizi (Flybywire).

Mnamo 1988, ndege hiyo ilifanya safari yake ya kwanza.
Mnamo 1992, Il-96 ilipewa cheti cha toleo lake.
Ndege hiyo ina matoleo makuu matatu ambayo ni Il-96-300, Il-96M/T, na Il-96-400.

Il-96-400 ni sawa na Il-96M lakini, tofauti Il-96M ina injini za Pratt na Whitney wakati Il-96-400 imewekwa na injini na mifumo ya avionics kutoka Urusi.

Ndege hiyo ni quadjet- inaendeshwa na injini nne za #Aviadvigatel PS-90A1 "twin-spool high-bypass turbofan".
Ndege hiyo inaweza kubeba abiria 436 kwa mpangilio wa kawaida na abiria 386 kwa daraja mbili.
Inaweza kwenda masafa ya maili 5,400 huku ikibeba abiria 315 katika mpangilio wa madaraja matatu.

Il-96 inapaa usawa wa futi 43000 kutoka ardhini na kasi ya 459 hadi 469 knots, uzito wa juu wa kuruka kilo 265,000, mzigo wa juu wa tani 58, uwezo wa tank ya mafuta ya galoni 40,322.
Mnamo Februari 2013, Shirika la Anga la Cuba lilisaini mkataba na Ilyushin kuagiza ndege tatu aina ya Il-96-400.

Chanzo:
[emoji991]
Wikipedia
FB_IMG_1686226270756.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE, NDEGE INARUDI NYUMA?

Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).

Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.

Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.

Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.

Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo

1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust

2>'Brake' za matairi na

3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.

Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.

Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.

Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.

Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug

1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'

2>Kuepuka ulaji mafuta

3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.

4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.

5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.

#Admin
Credit
#boldmethodView attachment 2620053
Well said..ndege kurudi kinyume nyume possible theoretically but in really world kuna ugumu wake.
 
Ameandika Mhandisi Matengenezo ya Ndege ..
Habari wakereketwa wa tasnia ya Usafiri wa anga. Tunachokiona hapo ni pua ya ndege/ sehemu ya mbele kabisa ya ndege ikiwa imefunguliwa.
Hapo ndani tunaona kifaa kiitwacho " weather radar" - kazi yake ni kutuma na kupokea signal (EM waves) kujua kama mbele ya ndege kuna mawingu yenye mvua na kuonyesha katika kifaa husika ndani ya chumba cha rubani.
Rubani atatoa maamuzi baada ya kuona picha ya mawingu hayo, kama ayakwepe ama anaweza kuyaingia na kusepa bila ya shida.

Maridadi Farid
FB_IMG_1686279683676.jpg
FB_IMG_1686279687440.jpg
FB_IMG_1686279691141.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Water Salute" ni nini?

Kwenye usafiri wa anga, 'Water salute' au salamu ya maji ni tukio linalofanyika kama sherehe kuashiria heshima au shukrani.

Saluti/salamu ya maji inaweza kutumika kwenye kumuaga Rubani wa muda mrefu katika kustaafu, kuwasili kwa ndege mpya, kuaga watumishi wakubwa katika usafiri wa anga, kukaribisha safari ya kwanza au kuaga safari ya mwisho ya shirika la ndege, kuaga/kukaribisha safari ya kwanza au ya mwisho ya ndege yenyewe.
Katika upande wa jeshi 'water salute 'hutumika pia kupokea au kuaga askari waliopoteza maisha katika kitendo cha kizalendo au matukio mengine muhimu.

Soma zaidi:
Tovuti za Mtandaoni
FB_IMG_1686280062522.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
SWALI,
KWANINI WANAANGA ZA MBALI HUSHINDWA KUTEMBEA WANAPORUDI DUNIANI?

Kukosekana kwa mvutano wa ardhi (Gravity) nje ya dunia kunamaanisha mwili unapoteza nishati ya kujenga misuli inayohitajika kubeba uzito wa mtu pia ubongo na masikio hupoteza balansi ya kumuweka sawa.
Nje ya dunia hakuna kuhisi uzito, juu wala chini.
Mikao yote mwili unahisi sawa hata kulala mithili ya popo kwenye chombo.

Safari ya wiki moja au mbili nje ya dunia inatosha kukusahulisha kumbukumbu ya mfumo wa balansi chini juu, juu chini na kuhisi kizunguzungu kila ukijaribu kusimama unaporudi duniani.

Hii ndiyo sababu wanaanga wakirudi duniani wanakuwa hawawezi kutembea husaidiwa kubebwa kufikishwa kwenye hema za matibabu.
Hii inakuwa kama mlevi aliyekunywa kupindukia na kushindwa kutembea, isipokuwa kwa mwanaanga anabaki na akili timamu.

Anapojaribu kusimama anahisi kama kitu kizito kinamkandamiza kurudi chini kwa nguvu au kumbebesha nusu tani ya mizigo.
Kwahiyo usistaajabu mwanaanga kutambaa kama nyoka ingawa huwezi kuwaona sana katika hali hii.

Mwanaanga mmoja alisema baada ya kutua duniani,
"Unaposimama kwa mara ya kwanza, unahisi mzito mara tano kuliko unavyotarajia si ajabu kuhisi kichefuchefu, tena kama umekaa anga hizo miezi sita au zaidi, dalili ni kali zaidi"

Hivyo hutumia muda kadhaa kulala ili mwili kurudisha hali ya mazoea ya dunia kisha kulazimisha kutembea kama mtoto anayejifunza kutembea.

Aidha kuna mambo mengi ya kufurahisha pale mwanaanga anaporudi kutoka kwenye anga za mbali.
Kwasababu ya mvutano dhaifu nje ya dunia, unapoacha hewani huwa kinaelea, basi warudipo duniani, kuvunja vikombe, simu, laptop huwa ni kawaida kwa wiki za mwanzo.

Wengi hujisahau na kuachia vikombe vya udongo au simu hewani na kusituka ikipiga chini.
Au kujiachia kukaa kwenye kiti akijua ataenda 'slow motion' kisha kujikuta anapigiza makalio chini kwa nguvu.

Hali hii hudumu kwa siku /wiki kadhaa kisha kurudi kawaida.

#Admin wetu

Chanzo:
#NASA/Astronauts tales
FB_IMG_1686281411743.jpg
FB_IMG_1686281415111.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
SABABU YA DIRISHA ZA NDEGE KUWA NA UMBO LA DUARA

{Tafsiri nyepesi}

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa sekta ya usafiri wa anga ulimwenguni, utakumbuka ajali tatu mfululizo zilizotokea ndani ya miezi 12 zilizohusisha ndege za #Uingereza aina ya #De_Havilland #Comet #DH106 na kugharimu maisha ya watu kadhaa karibu miaka sabini iliyopita.

Hizi zilikuwa miongoni mwa ndege za kwanza za abiria zenye kutumia injini za #jet, kipupwe {a/c}, sambamba na hewa yenye mkandamizo ndani (#Cabin_pressurization).

Moja ya sababu za kupata ajali mfululizo ikiwa angani ni kuibuka kwa nyufa katika kona za madirisha yake ambayo yalikuwa na pembe nne.

Ndege nyingi zenye kipupwe {#air_conditioning} zinapokuwa angani ndani hutengeneza mkandamizo wa hewa (#cabin_pressure) ili kufanya abiria ahisi kama amezungukwa na mazingira ya mkandamizo wa hewa ya asili iliyozoeleka ardhini kwakuwa kadri unavyoenda kimo cha juu mkandanizo wa hewa (#pressure) na hewa ya oksijeni vinapungua.

Mkandamizo wa hewa ndani ya ndege ndiyo sababu inayofanya muda mwingine hewa kutoka nje kwa kishindo mfano wa mlipuko endapo litatokea tundu ndege ikiwa angani na kama usukaji wa malighafi zinazounda ndege ni dhaifu basi ndege huweza kukatika kabisa na kusababisha ajali.

Hivyo basi mkandamizo wa hewa au 'pressure' inayozalishwa ndani ya kiwiliwili cha ndege husababisha misukosuko {#stress} au nyufa katika baadhi ya maungio ya ndege ikiwemo dirisha zenye umbo lenye kona kona.

Tabia ya umbo la mviringo husambaza nguvu sawa kuzunguka umbile lake, ila tabia ya umbo lenye kona {#square} nguvu hukimbilia kwenye pembe au maungio hivyo kuleta udhaifu.

Ajali ya ndege za "Comet" kukatika angani ziliathiriwa na nyufa kwenye kona za dirisha zake ukijumuisha na usukaji dhaifu wa malighafi iliyounda ndege hizo.
Ndiyo maana kwa sasa ni ngumu kukuta dirisha za pembe nne kwenye kiwiliwili cha ndege {#fuselage} zenye mkandamizo wa hewa.
Tangu hapo waundaji wa ndege walipata somo na kuanza kuunda dirisha zenye umbile la duara.

Upande wa mbele, ndege nyingi utakuta dirisha za pembe nne lakini si hatarishi kwasababu ya mfumo madhubuti unaotumika kuunda kuzunguka dirisha hizo.
Mfumo huo una uzito kiasi hivyo hauwezi kutumika kwenye dirisha zote

Admin.

#AviationForum/KLMsyllabus
FB_IMG_1686297312822.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameandika Mhandisi Matengenezo ya Ndege ..
Habari wakereketwa wa tasnia ya Usafiri wa anga. Tunachokiona hapo ni pua ya ndege/ sehemu ya mbele kabisa ya ndege ikiwa imefunguliwa.
Hapo ndani tunaona kifaa kiitwacho " weather radar" - kazi yake ni kutuma na kupokea signal (EM waves) kujua kama mbele ya ndege kuna mawingu yenye mvua na kuonyesha katika kifaa husika ndani ya chumba cha rubani.
Rubani atatoa maamuzi baada ya kuona picha ya mawingu hayo, kama ayakwepe ama anaweza kuyaingia na kusepa bila ya shida.

Maridadi FaridView attachment 2650608View attachment 2650609View attachment 2650610

Sent using Jamii Forums mobile app
Marekebisho kidogo. Hiyo ni weather radar antenna. Weather redar ni system ambayo unahusisha Antenna na transceicer. Hapo kwenye pua ya ndege ni Antenna.
 
Back
Top Bottom