𝗞𝗪𝗔𝗡𝗜𝗡𝗜 𝗛𝗘𝗟𝗜𝗞𝗢𝗣𝗧𝗔 𝗛𝗔𝗭𝗜𝗣𝗔𝗜 𝗝𝗨𝗨 𝗦𝗔𝗡𝗔?
Helikopta hupaa kwa kuzungusha panga zake (Rotors) ambapo husukuma hewa kwenda chini, na kuruhusu Chopa kwenda juu.
Neno 'Chopa' linatokana na sauti ya 'chop chop' pale panga zinapokata upepo.
Lifti inayozalishwa na panga huathiriwa kadri Helikopta inapopanda juu kwani hewa inakuwa nyembamba kadri unavyokwenda angani, hivyo Helikopta huhitaji panga kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kuendelea kuzalisha lifti.
Kwa wastani, helikopta inaweza kuruka futi 10,000 hadi15,000 juu ya usawa wa bahari.
Hata hivyo, urefu huu unaweza kutofautiana kulingana na aina ya helikopta.
Kwa mfano, baadhi ya helikopta za kijeshi zimeundwa kuruka urefu wa juu zaidi.
Urefu wa juu ambao helikopta inaweza kufikia huathiriwa na joto na msongamano wa hewa (Air density & Temperature)
Kuendelea kuruka juu nje ya uwezo wa Helikopta ilivyoundwa (performance envelope), Helikopta itaanza kukosa lifti, kutetemeka, kukosa udhibiti na hata kuanguka.
Ndiyo maana, si ajabu sana kuona baadhi ya Helikopta zikiwa zimegalala juu ya milima mirefu ya barafu kwenye kujaribu kufanya kazi za uokoaji (rescue missions) Panga hushindwa kuendelea kuzalisha lifti au kuganda angani (hovering) hivyo Helikopta kukosa 'balance' na kuanguka.
Marubani wengi wa helikopta huzingatia futi 10,000 kama kikomo cha juu cha urefu bora wa kuruka kwa helikopta za kawaida.
Admin:
Tafsiri ya:
Helicopter forums & Magazine