"..𝗕𝗼𝗲𝗶𝗻𝗴 𝗶𝗹𝗶𝘆𝗼𝗽𝗮𝗶𝘀𝗵𝘄𝗮 𝗺𝗶𝗴𝘂𝘂 𝗷𝘂𝘂 𝗸𝗶𝗰𝗵𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗶𝗻𝗶"
Mnamo Agosti 6, 1955 rubani wa majaribio wa Boeing Alvin "Tex" Johnston alizungusha upande nyuzi 360° (Barrel Roll) kuonyesha uwezo wa Boeing 707.
Ikiwa sehemu ya mpango wa maonyesho, wakati huo rais wa Boeing Bill Allen aliwaalika wawakilishi wa Chama cha Viwanda vya Ndege na Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga kwenye mbio za Seattle za 1955 Seafair and Gold Cup Hydroplane zilizofanyika Ziwa Washington mnamo Agosti 6, 1955.
Boeing 707 (iliyojulikana kama 367-80, iliyopewa jina la utani "Dash 80") iliratibiwa kufanya safari rahisi ya kuruka chini chini kwenye maonesho, lakini Tex Johnston badala yake alitumbuiza kwa mtindo wa "barnstormer barrel roll" kitu ambacho huwa kinafanyika kwenye ndegevita (Fighter Jet) ila si kwa ndege ya biashara ya abiria ya kupakia 140-189.
Siku iliyofuata, Rais wa Boeing, Allen alimwita Johnston ofisini kwake na kumwambia asifanye ujanja huo tena, Johnston akamjibu kuwa kufanya hivyo ni salama kabisa.
Allen akamuuliza: “Ulikuwa unafanya nini?” Johnston alijibu "Nilikuwa nauza ndege."
Tex aliendelea kushika nafasi yake kama rubani wa majaribio na hakupata matatizo yoyote ya kisheria kwa matendo yake.
Mtindo wake wa kuruka na mavazi ya aina ya cowboy (Johnston alipata jina lake la utani, "Tex" kwa sababu kila mara alikuwa akivaa kofia yake ya ng'ombe ya Stetson na buti za cowboy alipokuwa kwenye mstari wa ndege)
Unaweza kutazama video husika kwa kubofya link ifuatayo;
View: https://youtu.be/f28cITAXtww?si=C4E18RB0_DGuQO4S
Soga za kweli za Admin
Aviation Media Tanzania