Athari za muda mrefu za pombe hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za kiafya kwa watumiaji wa
viwango vya chini vya pombe hadi madhara
makubwa katika hali ya matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu.
Viwango vya juu vya matumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo, kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa kongosho , ugonjwa wa ini kutokana na pombe, na kansa. Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe.
Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.
Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.
Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida
zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo
wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa
moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo
inayotokana na kutumia kinywaji 1- 2 kwa siku, hata
hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swala lenye utata. Shauku
zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta ya
dawa, wadau wa sekta ya pombe piawamehusika
katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe.
Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na hipependekezwi kwa-ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizo thibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba za dawa.
Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za
matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na
ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha,
vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho na presha.
Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo, wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwatahadhari kwa sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza
matumizi wastani ya pombe kunaweza kusababisha ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana.
Manufaa haya ya matumizi wastani ya pombe yanapitwa na hatari za matumizi ya pombe wastani.