Shaka Kasenzangakona, Shaka Zulu, chifu wa wazulu aliyetawala eneo lubwa la Afrika ya Kusini ya leo. Shaka alikuwa mtoto haramu kati ya mfalme ya wazulu, Kasenzangakona na binti mfalme wa Elangeni, Nandi.
Uharamu wa Shaka ulipelekea kukataliwa na baba yake hivyo yeye na mama yake waliishi maisha ya kutangatanga hadi pale walipopewa hifadhi na mfalme Dingiswayo kutokana na uwezo wake mkubwa kijeshi.
Baada ya Dingiswayo kufa askari wa jeshi, chini ya Ngomane walimchagua shaka awe mfalme wao mpya, mda mchache baadaye Kasenzangakona naye alikufa hivyo shaka akarudi Uzulu kwenda kuchukua Ufalme wa wazulu kwani amini kuwa ni haki yake kama mtoto wa kwanza wa Kasenzangakona.
Hapo ndipo safari ya Shaka kuzipiga falme nyingine na kuishia kutawala eneo kubwa la kusini mwa afrika. Shaka zulu alikufa mwaka 1828 baada ya kuuawa na kaka zake Mhlanga na Dingane kwa kile walichodai kuwa ni katika kuchukua hatua dhidi ya kuzidi kwa ukatili wa Shaka ulisababishwa na kifo cha mama yake Nandi.
Shaka anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wenye uwezo mkubwa kijeshi kama ilivyo kwa Julius Caesar na Napoleon Bonaparte.
Ukitaka kuamini kuwa Shaka alikuwa hatari, Sikia, baada ya shaka kukuza vuguvugu la mfekane huko afrika kusini, baadhi ya wangoni walishindwa kuvumilia hivyo wakakimbia vita na kuja maeneo ya afrika mashariki. Walipofika afrika mashariki, wangoni waliokimbia vita waligeuka kuwa mwiba mchungu kwa watemi wababe wa maeneo ya Afrika mashariki kama mtemi Mirambo.
Ufalme wa shaka katika kilele chake