MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Poleni sana, hakikisheni anakuwa muda mrefu na watoto wenzie na hata kama mnaweza kuwaomba hao watoto muda mwingi wajaribu kumuongelesha labda inaweza kusaidia naye akaanza kuongea. Hakikisheni pia hana matatizo ya ukiziwi. Kila la heri.
Ni vema wakajaribu kumuweka karibu na watoto wenzake lkn anaweza bado akajitenga hata ukifanya hivi. Pia ajitahidi kumuandikisha kwenye klabu mbali mbali zinazokutanisha watoto wa umri wake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu fidelis zul zorander

Mtoto wangu alikaza shingo vizuri akiwa na miezi 2, aliweza kukaa vizuri akiwa na miezi 3, kutambaa alianza akiwa na miezi 6, kutembea alianza akiwa na mwaka mmoja na miezi 4.
 
Last edited by a moderator:
Je hapo unapoishi kuna watoto wengine? ikiwa hakuna watoto wengine waweza kuwa sababu .....
Kabanga,nashukuru kwa ushauri wako,Watoto wa umri wake wapo,ila tatizo ni kwamba mara nyingi hapendi kujichanganya na wenzake,hata tukimlazimisha kucheza na wenzake bado atatafuta namna ya kuwa pekee.
 
Ablessed nashukuru kwa ushauri mkuu, Kuhusu Tongue tie, tulishampeka kwa Daktari wa watoto Muhimbili na pia CCBRT. Kote wakamcheki ulimi na kusema hana tatizo lolote kwenye ulimi.
 
Nawashukuru sana ndugu zangu wote mliotoa Maoni na Ushauri mbalimbali,Ntafanyia kazi mawazo na ushauri wenu,naamini kupitia Mawazo yenu Mungu atatenda jambo na mtoto wangu ataanza kuongea vzr.
 
mzee wa busara zingatia maelezo ya Honey Faith, ulichosema na alichosema Honey Faith hutokea sana ktk jamii, bint yangu alichelewa kuongea, wakati huo tupo kota mkoani kikazi, tumerudi dsm, mtaani kwetu kakutana na lundo la watoto wenzie, ndani ya wiki 1 tu, ni anaongea kupitiliza, amekuwa muongeaji mzuri sana, yaani amekuwa na uwezo mkubwa sana wa kujieleza!

Nawahauri kama watu wa aafya wamethibitisha hana tatizo lolote, kuweni na amani, wakati wake ukifika ataongea tu!
 
Samahani, lakini hizo ni sign za ugonjwa unaitwa Autism. Ni social interaction and communities difficulties, jitahidi kumchanganya sanaa na watoto wenzake, hata improve lakini mpeleke hospital kama ami au tumaini watakuwa na idea bongo hawana.
 
Kabanga,nashukuru kwa ushauri wako,Watoto wa umri wake wapo,ila tatizo ni kwamba mara nyingi hapendi kujichanganya na wenzake,hata tukimlazimisha kucheza na wenzake bado atatafuta namna ya kuwa pekee.

Ni PM mkuu kama bado ilo tatizo analo
 
Bado anaenda miaka 4 sasa ikifika sept

Ameanza kucheza na wenzake au bado anajitenga, akicheza na vitu uwa anavipanga foleni kama magari anayapanga kwa mstari, anaweza kukaa chini kwa dakika zaidi ya 5, au anakuwa anahangaika na kurukaruka saa zote yaani hyperactive au mtundu aliyepitiliza, je Usiku analala vizuri na kula uwa anakula au anachagua sana aina ya vyakula?
 
Hapana bado Anajitenga kulala sio mbaya mwanzo alikuwa anasumbua sana usiku kucha kuhusu kula anachagua sana mboga bila nazi hali tena anapenda wali mbaya zaidi hatafuni anameza tu.ni mtundu pia anapenda kushika vitu mkononi na kuchezea vitabu
 
Pole Sana Dada! Huenda Akawa Hana Tatizo La Kiafya Kabisa...Tatizo Linaweza Kuwa Mazngira Aliyokuliwa Na Yanayomzunguka! Jaribu Kubadili Mazingira.
 
Back
Top Bottom