MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Mtoto wangu yeye ana miezi 17,akitAKa kitu anakushika mkono anakuvuta mpaka kilipo kitu anachokihitAji kama anataka maji atakupelekA kwenye ndoo yA maji, na akitaka kunyonya anakuvutA mpaka kwenye kiti ili ukae anyonye .

Mpeleke kwenye hospital yoyote yenye audiologist mzuri amkague kwanza. Majibu atakayokupa unaweza kushare na mimi kupitia 0765886191. Lakini pia, unaweza kunitumia video clip ambayo mtoto anaongea, anaongeleshwa na kuagizwa kitu au kupewa maelekezo fulani. Ni ngumu kwa mimi kukwambia chochote bila kulijua tatizo la mtoto wako.
 
Tatizo la watoto kuchelewa kuongea ni la miaka mingi sana lakini miaka ya hivi karibuni limeonekana kuongezeka kwa kasi sana siku hadi siku.

Kuchelewa kuongea ni moja kati ya matatizo ya mawasiliano ambayo huwakuta watoto: tatizo hili hujitokeza pale ambapo watoto hushindwa kuongea kuendana na hatua ya ukuaji walioifikia. Mtoto hushindwa kuongea au kuwaelewa watu wengine wakiongea. Aidha maendeleo ya lugha kwa mtoto husimama au huenda taratibu sana.

AINA ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Zipo aina tatu za tatizo la kuchelewa kuongea kwa watoto. Aina ya kwanza ni ile ambayo mtoto hushindwa kusikiliza nini anaambiwa. Aina ya pili ni ile ambayo mtoto hushindwa kujieleza juu ya ni nini anataka. Aina ya tatu ni ile ambayo mtoto hushindwa kufanya vyote: yaani hushindwa kujielezea na kusikiliza wengine.

Kutokana na uzoefu wangu, aina ya tatu hujitokeza kwa watoto wengi zaidi, watoto wanaoshindwa kujieleza kwa kuongea pia hushindwa kujua nini wanaambiwa na watu wengine.

DALILI ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Mtoto ambaye ana tatizo hili la kuchelewa kuongea mara zote huwa nyuma ya hatua zake za maendeleo na ukuaji. Ili mzazi/mlezi aweze kujua kama mtoto wake ana tatizo hili anaweza kuangalia kama mtoto wake ana dalili zifuatazo:-

Moja, Mtoto kushindwa kupiga kelele zisizo na mpangilio mpaka kufikia miezi 15. Kelele kama “Yaaa Yaaa”, “Daaa Daaa” au “Bluuuuu Bluuuu”

Mbili, Mtoto kushindwa kuongea mpaka kufikia miaka miwili. Kuongea neno moja moja au mawili ambayo yanaweza kumpa mzazi muelekeo juu ya nini mtoto anataka kusema. Kama vile “Mama tamu” “Mama acha” au “Baba Pira”

Tatu, Mtoto kutoweza kuzungumza sentensi fupi mpaka kufikia miaka mitatu. Sentensi kama vile “Naomba maji”, “Nataka kojoa”, “Naomba maziwa”, “Nataka mpira” au “Shikamoo Baba!”

Nne, Mtoto kuwa mzito kufuata maelekezo mpaka kufikia miaka mitatu. Mtoto kutoelewa nini anaambiwa na wenginine. Kwa mfano anaambiwa: “kaa chini” na anashindwa kujua nini anatakiwa kufanya na hata akifanya mara nyingi hufanya kinyume.

Tano, Matamshi ya maneno kuwa mabaya mpaka kufikia miaka mitatu. Kwa mfano, mpaka kufikia miaka mitatu mtoto anatamka neno, Shika-chika, Sasa – chacha au Mkate – Nkate.

Sita, mtoto kushindwa kuweka maneno katika sentensi mpaka kufikia miaka mitatu. Mtoto anaweza akawa anayajua maneno mengi lakini akawa anashindwa kuyaweka maneno katika sentensi moja akielezea kile anachokitaka hivyo huishia kulisema neno moja moja tu. Kwa mfano mtoto huishia kusema: “kula” akimaanisha anataka chakula, au “piga yule” akitaka kusema yule kampiga.


SABABU ZA TATIZO LA KUCHELEWA KUONGEA KWA WATOTO

Kutokana na uzoefu na tafiti zangu binafsi nimebaina ya kuwa zipo sababu nyingi za watoto kuwa na tatizo la kushindwa kuongea kwa wakati, kuendana na hatua na maendeleo ya ukuaji wao. Zifuatazo ni baadhi ya sababu:-

Moja, matatizo ya kusikia kwa watoto. Mtoto mwenye matatizo ya kusikia vizuri ni ngumu sana kuweza kuzungumza kwa wakati kama watoto wengine. Ni muhimu mzazi akiona mtoto wake anashindwa kufuata maelekezo na kuitumia lugha vizuri kuendana na umri wake afuatilie kama anaweza kuwa na tatizo lolote la kusikia ili aweze kupata msaada unaotakiwa mapema.

Mbili, Usonjii (Autism). Japo kuwa kuna baadhi ya watoto hawaathiriwi na autism katika maendeleo yao ya lugha lakini, kwa watoto wengi hupelekea kuchelewa kuongea. Angalau 70% ya watoto wenye Usonji huchelewa sana kuongea. Watoto wenye usonji huongea baada ya wataalamu kuwasaidia kujifunza na kutumia lugha kuendana na mahitaji yao. Ni ngumu kwa wao kuweza kujifunza kutumia lugha bila jitihada za wataalamu.

Tatu, mtoto kukosa watu wanaozungumza mara kwa mara karibu yake. Watoto huchukua lugha moja kwa moja kutoka kwa wazungumzaji wengine na ndiyo maana mtoto akiwekwa kwa watu wanaotumia lugha ya kiingereza atazungumza kiingereza, akiwekwa na wazungumzaji wa kiswahili atazungumza kiswahili n.k hivyo kwa mtoto kukosa watu karibu yake ambao huzungumza mara kwa mara humfanya ashindwe kuchukua lugha hali inayoweza kupelekea mtoto kuchelewa kuzungumza.

Nne, Wazazi kutokuwa na maarifa na hatua na maendeleo ya ukuaji wa mtoto. Sababu hii imekuwa ikipuuzwa sana na wataalamu kila wanapoelezea tatizo hili lakini binafsi nafikiri ni moja kati ya sababu kubwa kabisa. Wazazi wengi hawajui nini wafanye ili kuwapitisha watoto wao katika hatua mbalimbali za ukuaji pindi waoneshapo changamoto hali inayoweza kupelekea watoto kukwama katika matatizo bila usaidizi. Watoto wengi hushindwa kuongea mapema kwasababu wazazi wao hawana ufahamu na jinsi lugha kwa mtoto inavyojengeka na nini wafanye endapo kukitokea changamoto.

Tano, Mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake (Njiti). Mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake huweza kuleta matatizo mbalimbali likiwemo na hili la kushindwa kuongea mapema kwa mtoto. Kwani kuna baadhi ya viungo muhimu vya mwili wake vinakuwa havikumalizika kujiunda hivyo huendelea kujiunda taratibu mara baada ya kuzaliwa kwake.

Sita, Kumwacha mtoto atumie vifaa vya kielekroniki kama vile TV na simu kwa muda mrefu. Sababu hii pia haisemwi na wataalamu wengi, lakini nimeona ni moja kati ya sababu kubwa. Mtoto wa kuanzia miezi mpaka miaka mnne endapo ataachwa kwenye TV kwa muda mrefu yaana kwa zaidi ya saa moja kwa siku ni lazima itaingilia maendeleo ya ubongo. Ubongo ndiyo unafanya na kuratibu kila kitu kinachohusiana na maendeleo ya lugha kwa mtoto hivyo kwa maendeleo ya ubongo kuvamiwa na vifaa hivi vya kieletroniki vitu vingi vinavyotegemea maendeleo ya ubongo kuendelea pia husimama. Tutaliongelea hili kwa kina wakati mwingine kwani ni pana sana.

Saba, Mahusiano mabaya kati ya mtoto na mzazi/mlezi. Mtoto kuwa na mahusiano mabaya na mzazi/mlezi wake ni sababu nyingine ya mtoto kuchelewa kuongea. Mzazi/mlezi ambaye haoneshe mapenzi na ukaribu na mtoto wake au ambaye ni mkali kupitiliza kwa mtoto akiwa bado mdogo kabisa anaweza kupelekea mtoto kutotaka kuelezea hisia au mahitaji yake mapema hali inayoweza kupelekea mtoto akachelewa kuongea.

Nane, Familia kutumia lugha zaidi ya moja. Watoto wengi wanaokuwa katika familia inayotumia lugha zaidi ya moja huwa na tatizo la kuchelewa kuongea kwani watoto hulazimika kutumia nguvu ya ziada kutoa tafsiri ya baadhi ya maneno na kufananisha katika lugha zote mbili jambo ambalo huweza kuwachukua muda ukilinganisha na yule anayekua kwenye familia inayotumia lugha moja.

Tisa, Matatizo ya mdomo kama vile uzito wa ulimi. Mtoto mwenye ulimi mzito asipopewa tiba mapema tatizo hili ni lazima litamkuta kwani ulimi ni moja kati ya viungo muhimu sana kwenye uzungumzaji wa mtoto. Yapo mazoezi na jinsi ya kufanya ili mzazi aweze kulimaliza tatizo hili. Nitaligusia siku nyingine nikiwa naelezea juu ya jinsi ya kufanya ili kumaliza tatizo hili kwa watoto.

Kumi, Matatizo ya ubongo. Baadhi ya matatizo ya ubongo kama vile Majeraha kwenye ubongo yanaweza kuathiri misuli ambayo ni muhimu katika maendeleo ya lugha kwa watoto.

Hitimisho, Matatizo mengi ya maendeleo ya lugha na kuzungumza kwa watoto yanatibika kirahisi sana kama mzazi/mlezi atatafuta tiba mapema kabla ya mtoto kufikisha miaka mitano hivyo ni muhimu wazazi/walezi wakatambua mapema kuwa watoto wao wana tatizo hili na kutafuta tiba kutoka kwa wataalamu mapema.

Tuendelee kuwa pamoja nitaandika juu ya jinsi ya kupambana na tatizo hili wakati ujao. Ni rahisi tu, endapo mzazi/mlezi ukijitoa kwa moyo na kushirikiana na wataalamu.
Kwangu Mimi hi ni mada ya maana kuliko zile zilizozoeleka humu ....
 
Umeisoma makala yote? Mtoto anayechelewa kuongea huwa katika hatari ya kuwa nyuma katika kila kitu. Nimesaidia watoto wa namna hiyo, kama haujawahi kusaidia wala kuwa na mtoto wa namna hiyo unaweza usione uzito wa tatizo. Usipende kurukia hitimisho rahisi kwenye matatizo sensitive kama haya kwani kuna wazazi hawalali kisa matatizo kama haya.
Unaanzaje kupata usingizi mzuri au kufanya kazi vizuri endapo ukaona damu yako ina shida?

Unaweza ukawa na furaha ila kuna muda ukikaa unaona kuna uchungu unaingia ndani kuhusu mtoto.

Hongera kwa bandiko lenye elimu pana, huyo jamaa mpuuzie tu na kisha umsamehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TV inarudisha sana maendeleo ya ukuaji wa ubongo wa watoto. Nimefanya diagnosis kwa watoto wengi wenye tatizo hili, chanzo kwa wengi nimebaini ni TV. Nitaandika makala juu ya hili nikipata wasaa.
Inaweza ikawa ni kweli, pamoja na kuwapa simu watoto kutazama makatuni kwa muda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za Kazi.

Naombeni msaada wa ushauri hapa. Nina mwanangu ana miaka mitatu na miezi sita na mwaka huu nimemuanzisha shule. Tatizo lake ni kwenye kuwasiliana imekuwa changamoto sana. Anaweza kuimba nyimbo za shule toka asubuhi hadi jioni, anaweza kuhesabu, kuandika na kusoma 1-20, Anaweza kusoma herufi zote A-Z.

Randomly kuna maneno mengi anatamka shida ni kwamba hawezi kujibu chochote utakachomuuliza labda ukimuambia afanye kitu flani ndo anaweza. Ila ukimwambia aseme neno flani au kitu flani anakuangalia tu. Hapa shida inaweza kuwa nini na suluhisho lake ni nini? Kama kuna mtu ana namba ya mtaalamu naomba anisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Mwanangu Wa Kiume , Ana Umri Wa miaka miwili na Miezi Miwili, lakini Ajabu Hadi Sasa hajui kutamka Mama Wala baba Yeye Akishamka Ni kuguna Tu Na Kuimba hadi Siku Inaisha Ni Mhhh..... Aahhhh
.... Eeeeh.......!!!

Majirani Wanamsema Vibaya Kuwa Mtoto Mkubwa lakini Anazidiwa Hata Na Wadogo wenzie yaani Hajui kuongea chochote, hii Inanipa Stress Mimi Kama Mzazi Najisikia Vibaya Sana Na Sijui Nifanyeje Ili Mwanangu Aongee

Naombeni Mnisaidie Jinsi gani Nitamfanya mwanangu Ajue Kutamka Maneno kama baba n.k
 
Habari wakuu..

Mtoto wangu ana miaka minne na miezi miwili hajajua kuongea vizur..wala hawez kuunganisha maneno vizuri yaeleweke..ushauri nifanyeje wakuu.

Mtoto ni wa kike
 
Mwanangu wa sita kuzaliwa alikua anasubiri nikirejea anaanza kutoa mashtaka...
Aaa baba.....
Kisha naitika, then anasema
Aaa mama akuma chini...🤣🤣
Kisha namuuliza, ikawaje
Then anajibu, akuma aaamimi achafuka sana....😂😂
Then baada ya hapo, namuuliza tena unasemaje??😆😆
Wakati huo alikua anaumri wa mwaka mbili na nusu....😅😅
 
Mzee stress kisa majirani wamesema?

Unataka tukuambie uende kwa mganga?

Kama ana afya, uzito unaohitajika, anatembea kwa umri wake mi sioni shida.
 
Usisikilize maneno ya hovyo na kukatisha tamaa ya majirani. Huyo mtoto bado mdogo kwa umri huo kumhukumu. Hata hivyo watoto hawafanani katika hatua za makuzi. Wengine wanawahi kuongea wengine wanachelewa. Sasa majirani wanataka mtoto wa miaka 2 awe anaongea kama chiriku!!!
 
Ni Kati ya sababu ya kum bembenda mtoto waulize watu maana ya kubemenda mtoto halafu ndio utajuwa kama ulifanya kosa
Hiizi ni fikra za hovyo sana mkuu, bila shaka wewe ni msikiliza maneno ya majirani na kitaa sana
 
Sina uzoefu sana na hili ila jaribu kumpeleka shule za vidudu akachanganyike na wenzie, wataalam wanadai inasaidia
Siungi mkono huu ushauri aiseeee....
Mtoto wa kiTanganyika inapendeza akianza shule akiwa na umri wa walau miezi 30
 
Back
Top Bottom