Mada ya wanyama

Nimepenpda huu msemo "kacute kumbe ka killer" umenitia hofup sn huu msemo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni mmoja ya wanyama wenye akili sana duniani. Kwenye top four kuna sokwe mtu, mbwa, pomboo(dolphin) na huyu jamaa. Pia ni bosi mmoja msafi sana. Kama umewahi mfuga utakuta anajisaidia mbali na anapokula.
Wakati ni haram kumla
 
Pen tailed tree shrew, kipanya kidogo , nadhani ni jamii ya komba, kinachopiga gambe siku nzima.



Kanaishi kwenye minazi na kakinywa nectar iliyooza (ferment) ya maua ya miti hiyo (bertam palm). Hiyo nectar inaweza fikia alcohol content ya ya 3-4%,

. Nilisikia kuwa komba (bushbaby) nao ni wapenzi wa pombe, kama kuna komba anaishi kwenye mti karibu na nyumba yako, ukiacha glass ya bia nje usiku, asubuhi utakuta komba alishajisevia.
 
Huyu ni noma. Niliona video kuna cayman (aina ya mamba wa south america) alijaribu kumfanya mmoja lunch akapigwa shoti hadi kufa.
Nimekuja kujua pia electric eel siyo true eel, bali ni aina ya knifefish ambaye yuko karibu zaidi kijamii na kambale kuliko eel wenyewe.

 
Bowerbird, huyu ndege vijana wa JF wanaweza kumuita baharia wa ndege. Wa kiume wanajenga viota na kuvipamba vizuuri ili kuvutia mpenzi. Wa kike wanakagua na kuchagua kiota kipi kimependeza ndo anaingia/kubali kuwa na huyo dume. Wako vizuri sana katika kupangilia rangi na wanatumia kila aina ya vitu kupamba kiota kama vile mawe, maua, vitu vya kibinadam kama vifuniko vya chupa, vipande vya glass...

Kibongobongo huyu ndege ni baharia mwenye ghetto lenye carpet la manyoya na bonge la sofa, huenda na subwoofer pia

 
Nimetokea kukaogopa sn haka ka ndege, kumbe ni kacute lkn ni kakiller.View attachment 2030830

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee ni warefu.

Anaweza fika 6 feet.

Now cassowary wanakula matunda. Na anajua mti wenye matunda ni huu, yeye akishahitimisha ni huu basi ndiyo ushakua wake sasa ajitokeze mtu au mnyama akapita karibu na huo mti.

Moto utakaowaka hapo si mchezo.
 
Kuna samaki wa ziwa Tanganyika naye ana hii tabia. Anakusanya makombe ya konokono na kuyapanga. Jike anaangali mzigo upi ni mwingi. Viumbe vyote wanawake wanamkubali mwenye uwezo.
 
Kuna samaki wa ziwa Tanganyika naye ana hii tabia. Anakusanya makombe ya konokono na kuyapanga. Jike anaangali mzigo upi ni mwingi. Viumbe vyote wanawake wanamkubali mwenye uwezo.
Noma sana. Surely wale samaki wengine wasio na mawe na walikosa majike kwa kuwa na collection ndogo watakuwa wanaishia kulalamika eti 'mademu wanathamini utajiri kuliko utu (usamaki?)
 
Noma sana. Surely wale samaki wengine wasio na mawe na walikosa majike kwa kuwa na collection ndogo watakuwa wanaishia kulalamika eti 'mademu wanathamini utajiri kuliko utu (usamaki?)
Hahaaaaaa
 
Orca (killer whale) naweza kusema ni kama genge la wahuni wa baharini. Pamoja na kuitwa killer whale, wao ni ana ya dolphin, ndiyo dolphin mkubwa katika jamii ya dolphins. Wanasayansi wanaamini hawa majamaa wana akili sana. Wanawinda kwa makundi na pia wanajua kutumia miili yao na movement ya kutengeneza mawimbi yanayoweza kumtungua seal aliye juu ya barafu majini. Pia wanaweza kujisogeza hadi ufukweni kiasi fulani kuwinda seal.

Kuhusu kushambulia shark, inasemekana na wao wamegundua kuwa shark anapata temporary paralysis akiwa upside down hivyo huwavizia kwa chini na kuwabinua ili wawe juu chini. Pia wanasayansi wameona mara nyingi sharks wanaopigwa na orca wanakuwa wametolewa ini, yaani orca anang'ata eneo ambalo huwa ini na organs zingine zipo na kunyofoa ini. Wanahisi ni kwa sababu ni source bora ya protein. Kwa hiyo pamoja na kufanya mauaji kwa sababu zao za kibabe na kihuni tu baharini, wanafanya hivyo kwa chakula pia.



orca aka killer whale aka panya road wa baharini.
 
Hawa wanaogopwa na kuheshimiwa kama watawala wa nyika.



Ila kama wewe ni mnyama wa kuwindwa (mf. punda milia), ukiwaona hawa wazee wanakufuatilia, we pambana na kimbia maana unaweza ukapona maana inasemekana simba wanashindwa kukamata mnyama mara nyingi zaidi kuliko kupata (success rate 25%).

Ila ukiona unawindwa na kundi la hawa jamaa wengine, mbwa mwitu, get your affairs in order na sali toba na sala zako za mwisho maana unaweza kuwa na uhakika wa kifo. Hawa jamaa ndo vinara wa successful hunt nyikani (85%). Wakikuamulia hawa jamaa jua umekwisha.

 
Napenda sana wanyama, tabia zao zinaweza kukutafakarisha yana jinsi mungu alivyo mkuu.
 
hivi tagi la mbwa mwitu linawz kuua binadamu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…