[emoji840]️Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu..
[emoji840]️Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake magumu na makali yanakosa uwezo wa kunyakua chakula..
[emoji840]️Mdomo wake uliochongoka unapinda, mabawa yake yanakuwa mazito na kunata kwenye kifua chake hivyo kumfanya kuwa mzito kuruka na kuwa mwenye kasi ndogo..
Katika hali hiyo ndege huyo hubakiwa na maamuzi mawili;
[emoji841]️Aidha akubali kufa au afanye mabadiliko katika mwili wake ili aendelee kuishi miaka 30 iliyobakia..
[emoji841]️Akichagua kufanya mabadiliko kwenye mwili wake humchukua siku 150 sawa na miezi 5, hivyo huenda katika kilele cha mlima mrefu na kujificha katika pango ambapo watu na wanyama wengine wanaoweza kumzuru hawafiki..
[emoji841]️Ndipo huanza kujivua kucha, midomo na mbawa zake zilizozeeka huku akisikilizia maumivu makali, baada ya mabadiliko hayo hurudi katika hali yake ya mwanzo ya kuweza kuruka kwa kasi na kupata chakula chake kizuri (fresh meat)..
View attachment 2060092