Mada ya wanyama

Mada ya wanyama

Rattlesnakes na nyoka wengine wanaokaa mashimoni hutumia macho yao kuona wakati wa mchana, kama wanyama wengine wengi wenye uti wa mgongo, lakini wakati wa usiku, wanyama hawa wanaotambaa hutumia mfumo wao wa infrared kugundua na kuwinda mawindo ya wanyama wenye damu-joto ambao wasingeweza kuonekana kabisa katika anga za nyoka hao.

Kidubwasha chenye mfumo wa infrared kina umbo kama kikombe ambacho husaidia kutoa mionzi ya infrared na kuruhusu retina ya jicho la nyoka kupiga picha eneo la windo (prey) lenye joto na hatimaye kukamata windo.


Baadhi ya wanyama, ikiwa ni pamoja na tai, hedgehogs, na kamba, wanaweza pia kuona chini ya ultraviolet spectrum.
Binadamu hawawezi kuona mwanga wa infrared au
ultraviolet kwa jicho lake pekee.
 
Nimemkumbuka na Antlion( Chungu simba). Larva wa huyu bosi huwa anachimba kashimo ardhini na yeye anajifukia pale katikati ya shimo. Kuta za shimo zinakuwa ziko kwenye angle fulani. Kwenye zile kuta anajaza mchanga. Sasa sisimizi au siafu ikijichanganya na kudumbukia mpe inashindwa kutoka. Ule mchanga kwenye ukuta unakuwa unaporomoka kila akijaribu kutoka. Basi hapo jamaa anatoka na kumtafuna kisha anarudishia mchanga na kusubiri tena windo.
View attachment 1713108View attachment 1713107
Nimekumbuka mbali sana.
 
Hivi mshana umeacha kazi ranger safari sijakuona siku nyingi
WAJUE WANYAMA KWA SIFA ZAO ZA KIPEKEE.

1. Nyangumi.
Huyu ndio mnyama mkubwa kuliko wanyama wote, ukimuweka katika kiwanja cha mpira wa miguu, hubakiza mita chache ili kufikia nusu ya kiwanja hicho, mbali na ukubwa huo lakini ni mnyama mwenye macho madogo sana, ila sehemu za siri noma sana dume huwa na uume wenye futi 12.

2. Twiga.
Huyu ndiye mnyama mrefu kwenda juu kuliko wanyama wote unaowafahamu, anapenda amani, ni mpole lakini hapendi mizaha, miguu yake ndio silaha pindi anapovamiwa na hilo teke usiombe.

3. Kozi
Huyu ndiye kiumbe mwenye uwezo wa kukimbia kuliko mnyama yoyote, ni ndege mwenye ufanano sana na tai, ukimshitua akakimbia kama upo Dar es salaam usiendelee kumtafuta dar, wapigie ndugu zako moro kuuliza kama ametua huko au lah.

4. Nyegere.
Ndio anavunja rekodi kwa wivu alishawashangaza watalii hapo Serengeti baada ya jike wake kujikwaa, alichimba shimo refu kidogo kuhakiki kama ile ilikuwa ni ajali kweli, au kuna faulo alitaka kuchezewa kwa bae wake.

5. Kobe
Ndiye mnyama anayeishi miaka mingi duniani, pengine kuliko wanyama wengine wote hufikia miaka hadi 350, kwa Tanzania tunao wenye miaka 200+, kama nakuona raha za dunia zinavyokufanya utamani kuwa Kobe.

6. Kicheche.
Ndiye mnyama anayependa ngono kuliko kiumbe yoyote, wanapokutana jinsia tofauti kabla ya salamu huanza kusasambua kwanza, yaani hawa katika jamii zao hata msibani hukutana kwa mapenzi pia, inakadiriwa kwa siku ili walale usingizini mwororo auheni wapitiane mara 60 na zaidi ! Na ndio sababu hata mtu akiwa kiwembe huitwa kicheche.

7. Konokono.
Ndio kiumbe anayesafiri taratibu sana na hii ni kwa sababu hujitengenezea njia ya kupita kwanza ndipo apite.

8. Tai
Ndio kiumbe mkorofi kupita kiasi ni kawaida kunyang'anya watalii chakula, ni kawaida kusumbua ndege wenzie wanapoatamia, kupigana nk ili mradi fujo.

9. Nyati
Mnyama mwenye hasira na kisasi kuliko wanyama wengine wote, simba wanamwelewa vyema sana huyu kiumbe, wakithubutu kuua mtoto wake na wao huenda kukanyaga watoto wake vile vile au vipi bwana jicho kwa jicho, jino kwa jino tuone sasa.

10. Kipepeo.
Ndiye kiumbe mpenda amani pasina mfano, ukipita msituni umenuna usitegemee watakusogelea, ila mkipita na mwenza wako, mnacheka mna furaha, ahaa utashangaa wanawapamba !

11. Simba.
Pengine sababu ya kuitwa Mfalme ni ubabe, Dume la simba ndio mnyama pekee anayejijua kwamba anaogopwa na hata majike wake wanapopata dhahama, akipata taarifa hujitokeza mara moja na ukiona madume yameongozana mawili basi jua huo mziki mwamuzi ni Mungu.

12. Mbu
Ndio kiumbe aliyeweza kuua binadamu wengi sana kuliko mnyama yoyote yule unayemfahamu wewe, utapokaona tafadhari Katie kitasa.

13. Komba
Ndiye mnyama mlevi kuliko wanyama wote na akilewa hulia pasina sababu ya msingi, hata ukibahatika kumuona sura yake imekaa kilevi levi, hupendelea pombe za kienyeji kuliko bia, we watege kwa mnazi au ulanzi sio misosi hapo utawapata.

14. Popo
Pamoja kwamba mchoro wake hupendeza sana katika michoro, ila ni miongoni mwa viumbe wenye sura mbaya sana kuliko wengine wote.

15. Tembo
Ndiye mnyama mwenye uwezo wa kuhifadhi sana kumbukumbu katika kichwa chake, kama ulipojenga walihawi kupita tegemea kuna siku watakuwa wageni wako, wakati tunakazana kusema tembo wamevamia sehemu fulani tukae tukijua maeneo hayo wana historia nayo, sasa siku mpige jiwe mkutane baada ya miaka kumi ndio utajua ule mkonga ni bakora au pua.

16. Pomboo
Ndiye mnyama mwenye huruma sana kiasi kwamba akikuona una tatizo, huacha mambo yake na kutaka kukusaidia
Itaendelea...
 
Kalaaniwa kwani pig alifanya nini?
Kushindwa kuangalia angani siyo issue kubwa ni suala la anatomy ya misuli ya shingo yake kutoweza kuruhusu kuangalia angani like-wise hata wewe kushindwa kuangalia kisogo chako hakuharalishi kuwa wewe umelaaniwa. Ni suala la uamuzi wa manufacturer mwenyewe.
Mkuu una ushemeji na nguruwe,maana sio kwa kulalama huko
 
Kanyongwa? Au kajinyonga?
JamiiForums1153808109.jpg
 
Daaaaah! itakuwa wamepata pengo kubwa mzee wa lugha ngumu wakija wageni hata ungekuwa icu watachomoa oxygen ukafanye kazi.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kuna kazi hata ukistaafu unaongezewa mkataba
 
Kwa
Huyu ndo mnyama anaesadikiwa kuwa mvivu kuliko wote duniani.Mnyama huyu hulala kwa muda wa masaa 18 kwa siku kwa kuning’inia kwenye matawi ya miti na akiwa anatembea ardhini anatumia muda wa dakika 1 kutembea umbali wa kati ya Sentimeta 15-30 ambao ni sawa na urefu wa rula moja.kitaalamu anaitwa lazy sloth.View attachment 1710371
Imani inasema ni wavivu kwasababu imezoeleka all cold blooded mammals wanaspeed wanapomove, hawa wanatembea taratibu kwasababu yakusave energy miilini mwao. Kwa upole upole wao wanaliwa sana na duma weusi na wakijivu huko Costa Rica. Hata wakimuona adui wanashindwa kuongeza speed what a sad creature on Earth!
 
Back
Top Bottom