KAKA KUONA BINGWA WA NGUVU ZA KIUME
Ni jina maarufu la mnyama ambaye kwa kimombo anajulikana kama (pangolin )au (scaly anteater).
Jina kaka kuona linatokana na uhadimu wake wa kutokuonekana kwa imani huchukuliwa kwamba kuonekana kwake ni bahati kwa namna moja au nyingine .
Kaka kuona huonekana kwa adimu hii ni kutokana na maumbile yake ambayo hufanana na sehemu ambazo hupenda kuishi.kwa mfano hupenda kukaa kwenye miti yenye magome yenye kufanana na magamba yake hiyo humfanya kutamblika kwake kuwa kwa adimu kumtambua.
Kaka kuona amekuwa mnyama maarufu sana katika nchi za Asia ambapo hutumiwa kama kitoweo, dawa,urembo,ambapo dawa maarufu ambayo hutoka kwake ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume(manspower)
#mambo_usiyo_yafahamu_kuhusu_kakakuona
1_Ulimi mrefu, akiurefusha kwa
kuutoa nje ya kinywa unafikia urefu
wa sentimita 40.
2)Ulimi huo ambao pia unanata,
huutumia kwa ajili ya kukusanya
wadudu ambao ndiyo mlo wake wa
pekee, hana mwingine zaidi ya huo
kutokana na kukosa meno.
3_Asilimia 20 ya uzito wa mwili wa
mnyama huyo unatokana na magamba.
Kakakuona hutumia magamba hayo
kama silaha ya kujilinda dhidi ya
maadui.
4_Licha ya kuwa hutumia mbinu hiyo
kujilinda, lakini anapojikunja ndiyo
inakuwa rahisi kwa watu kumkamata
na kumbeba.
5_kakakuona huishi miaka 20
JE WAJUA? Kakakuona ndie mnyama anayewindwa kwa biashara haramu kuliko wote duniani.
# SABABU 20% mwili wa kakakuona umezungukwa na magamba "scales" ambayo yana protini aina ya "keratin" aina ambayo pia iko kwenye nywele na kucha za binadamu na pembe za faru.