MADA YA WEEKEND: Wazee wa Dar na Benz la Mwinyi

MADA YA WEEKEND: Wazee wa Dar na Benz la Mwinyi

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Wakati wa uzinduzi wa kitabu cha maisha ya mstaafu mzee Ally Hassan Mwinyi mambo mengi yamesemwa na hata baadaye kuonekana issue hii kuibukia kwa Simba na Yanga.

Twende kwenye hoja.
Wazee wa Dar waliofika kumsikiliza mama kama walikuwa 1000 basi kwa bei ya gari linalotakiwa anunuliwe mstaafu Rais Mwinyi kila mzee angeweza kurudi na tshs 250,000 nyumbani lakini akasema hana hata elfu 30!.

Mfano angalia prices ya hii benz,
IMG_20210509_080128.jpg
 
Tofauti ni moja wale ni wananchi wa kawaida walioenda kumsikiliza rais... Na yule ni rais mstaafu mwenye mtoto rais, aliyeenda kuzindua kitabu cha maisha yake
Kila mmoja hapo anakula kwa urefu wa kamba yake..
 
Wakati wa uzinduzi wa kitabu cha maisha ya mstaafu mzee Ally Hassan Mwinyi mambo mengi yamesemwa na hata baadaye kuonekana issue hii kuibukia kwa Simba na Yanga.

Twende kwenye hoja.
Wazee wa Dar waliofika kumsikiliza mama kama walikuwa 1000 basi kwa bei ya gari linalotakiwa anunuliwe mstaafu Rais Mwinyi kila mzee angeweza kurudi na tshs 250,000 nyumbani lakini akasema hana hata elfu 30!.

Mfano angalia prices ya hii benz

Twende na hesabu : Tshs 450,000,000/= zingetosha kuwalipa wazee 1000 pensheni ya Tshs 30,000/ = kwa miezi 15 tu.
 
Ili mwenye nacho azidi kuwa nacho hufanyika hivyo kwa gharama za walalahoi na watu fukara. Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe bali wa tajiri mali zake.
 
Kwani pale alifika kwa kutambaa. Benz atalitumia kwa safari kama ile ambayo alikuwa anatumia gari za juu zinazomchisha kwa umri wake. Mbona Magufuli alimpa nyumba mpya, kwani hakuwa na nyumba.

Eeh.. kumbe alishapewa na nyumba tena..? 🙄
 
Back
Top Bottom