1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Tatozo la Waafrika ni Elimu zetu za Kikoloni.
Elimu inayowafanya wasomi kujiona ni wazungu kwa sababu ya kahitaji ya kizungu.
Uafrika wetu tumeuondoa na kukimbia uzungu kwa nguvu zote.Wakati wazungu wakitendeana utu mkubwa sana wao kwa wao.
Kila msomi wa Kiafrika anaamini na kuwaza kuwa ipo siku ataingia kwenye nafasi ya ulaji tuu, na sio kutumikia wananchi na kutumia elimu yake kuwasaidia wengine.
Ndani ya mwaka mmoja Bilionea Mzee Ruksa amekabidhiwa mali za mabiloni kwa kodi za watu maskini sana.
Kikwete yeye aliamini kuwa maisha bora yanamfaa kila mtu awe nayo . Akasema maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana.
Mama ameanza kumgawia Bilionea Gari la mamilioni.
Bila shaka maskini wanasubiri mgao wao kutokana na Rasilimali walizopewa wote na Mungu.
Mungu ana Hekima kubwa sana.
Ingekua Hewa ya Oxygen inagawanywa na watawala leo hii mgawanyo ungekuwa kwa Upendeleo na kujuana na sio kwa haki .
Ingekua kifo kingepangiwa Ratiba na watawala wetu wa kiafrika na dunia basi ratiba ya kifo isingeonekana kutemblea maeneo ya wakubwa wala magonjwa.
Kuua Demokrasia ilikua ni jambo baya sana katika nchi hii.
Waoua demokrasia wamepoteza utu na uwajibikaji wa viongozi wetu kwa karne ijayo.
Walaaniwe wakurugenzi na wote walioshiriki kuua Demokrasia katika nchi hii.
Nchi yenye Demokrasia wapiga kura wanaheshimiwa kwa kupewa keki ya taifa mana wanahoji na wanawakataa viongozi wanaotumia vibaya rasilimali za umma kwa manufaa yao.
Nchi siyo na Demokrasia Wapiga kura hawana thamani mana hawawezi kubadili utawala na uongozi.
Tanzania tulipotezwa sana kwa kupumbazwa na watu wa chache kwa manufaa yao huku Demokrasia ikiuawa sasa matokeo yake ni haya.
Watumishi wanaolipwa mshahara laki nne kwa mwezi huku wakiwa wanajitafutia wenyewe mahitaji yao yote mpaka nauli za kufika ofisini na nyumba ya kuishi na chakula wanaambiwa mishahara yao inatosha na serikali haitaongeza mishahara mana sio kipao mbele chake.
Huku watawala wakiwa wanajipa kila kitu kwa kodi za wananchi. Wafanyakazi hawana tena thamani mana waliambiwa kura zao hazifiki hata laki 5 hivyo hazina maana. Na atakayethubutu kumpigia kura mpinzani atakiona cha mtema kuni.
Kazi inaendelea.