Madagascar waongeza lockdown baada ya kirusi kuzingua balaa, hivi hawa si ndio Wabongo walifuata dawa yao kwa ndege

Madagascar waongeza lockdown baada ya kirusi kuzingua balaa, hivi hawa si ndio Wabongo walifuata dawa yao kwa ndege

"Serikali haijachukua dawa ya kutibu virusi vya Corona kutoka nchini Madagascar kwa lengo la kugawa kwa wananchi bali ni kwa ajili ya utafiti na uchambuzi"

Endelea kupotosha maana nyuzi zako bila kupotosha huwa unaona hujaandika chochote yaani,

Serikali Kuifanyia Uchunguzi Dawa ya Virusi vya Corona Kutoka Madagascar
Sometimes tuachane na ushabiki wa Tz vs Ke na tuwe wakweli. Utafiti wa aina gani wakati walishaanza kuinywa hukohuko Madagascar kabla hata haijatua nchini? Na nasikia ilipotua hapa wakagawana! 🤔 🤔 isitoshe utafiti unachukua miezi mingapi maana hadi leo hawajatueleza walichogundua.
 
Sometimes tuachane na ushabiki wa Tz vs Ke na tuwe wakweli. Utafiti wa gani wakati walishaanza kuinywa hukohuko Madagascar kabla hata haijatua nchini? Na nasikia ilipotua hapa wakagawana! 🤔 🤔 isitoshe utafiti unachukua miezi mingapi maana hadi leo hawajatueleza walichogundua...
Hawakuwa wagonjwa waliionja tu,

Utafiti uliofanyika huenda iligundulika kuwa dawa haiko vizuri ndio maana serikali ipo kimya na hawajaagiza tena na ukumbuke ile haikununuiwi walipewa tu kwa ajili ya tafiti kwanza,

Halafu umeandika ilipotua hapa wakagawana ukiwa na maana kuwa huna uhakika na ulichosikia yaani ni story tu za vijiweni,

Serikali iliongeza nguvu kwenye dawa zake NIMRCAF na COVIDOL na hizi ndio dawa zinazotumika kutibu hapa Tanzania.
 
Kama suala ni vifo mbona hata malaria yanaua (tena kwa kiwango kikubwa)! Ukimwi unaua, TB inaua, hepatitis inaua, saratani inaua n.k...
Hayo magonjwa uliyoyataja hayaambukizi kama hiki kitu, na hayajasababisha dunia iingie kwenye lockdown, hayajasababisha tubadilishe desturi zetu za kusalimiana kwa mikono na kuziba nyuso kwa mabarakoa mpaka tunafanana mazombi.
Kwa kifupi, hiki kitu hakitaondoka kwa kuficha vichwa ardhini au kujichokea, lazima mapambano ya kisayansi yaendelee.
 
Hawakuwa wagonjwa waliionja tu,
Hiki ni kichekesho cha mwaka. Unaonjaje dawa ambayo hujaifanyia utafiti kuwa kama ina madhara au lah.

Utafiti uliofanyika huenda iligundulika kuwa dawa haiko vizuri ndio maana serikali ipo kimya na hawajaagiza tena na ukumbuke ile haikununuiwi walipewa tu kwa ajili ya tafiti kwanza,
Suala la kukaa kimya eti kwa sababu waligundua kuwa haiko vizuri ni uongo mtupu. Kwa kuwa walitutangazia wenyewe kuwa wanaifanyia utafiti hivyo walipaswa kurudi kutueleza walichogundua badala ya kukaa kimya.

Halafu umeandika ilipotua hapa wakagawana ukiwa na maana kuwa huna uhakika na ulichosikia yaani ni story tu za vijiweni,
Naona wewe ndiyo unaongea speculation (stori za vijiweni). Kwa kifupi hujui chochote kuhusiana na dawa ya Madagascar.

Serikali iliongeza nguvu kwenye dawa zake NIMRCAF na COVIDOL na hizi ndio dawa zinazotumika kutibu hapa Tanzania.
Hapa pia unaongea speculation au unahisi. Dawa za NIMRCAF na COVIDOL zilishatengenezwa baada ya kufanyiwa utafiti hata kabla Prof. Kabudi hajaenda Madagascar...
 
Hayo magonjwa uliyoyataja hayaambukizi kama hiki kitu, na hayajasababisha dunia iingie kwenye lockdown, hayajasababisha tubadilishe desturi zetu za kusalimiana kwa mikono na kuziba nyuso kwa mabarakoa mpaka tunafanana mazombi.
Kwa kifupi, hiki kitu hakitaondoka kwa kuficha vichwa ardhini au kujichokea, lazima mapambano ya kisayansi yaendelee.
Naomba fanya utafiti, japo kidogo tu, kuhusu magonjwa yanayosababishwa na virusi (virus diseases), utanielewa...
 
Unachokifanya hapa ni ubishi wa kijinga na kupotezeana muda,

Uambiwe walichogundua ili uweje...ili uagize?

Dawa lishe zilizotengenezwa hapa Tanzania zimesaidia kupambana na corona kama hutaki endelea kuamini unachokiamini cha muhimu ni kwamba inasaidia wagonjwa wa corona.

Unachokifanya hapa ni ubishi wa kijinga na kupotezeana muda,
Uambiwe walichogundua ili uweje...ili uagize?
Wewe ndiye unayeleta ubishi wa kijinga. Walitutangazia wenyewe kuwa wanakwenda kufanya utafiti, walipaswa kurudisha mrejesho.

Dawa lishe zilizotengenezwa hapa Tanzania zimesaidia kupambana na corona kama hutaki endelea kuamini unachokiamini cha muhimu ni kwamba inasaidia wagonjwa wa corona.
Hoja hapa siyo dawa lishe zilizotengenezwa nchini (kwa taarifa yako nazifahamu vizuri sana) bali suala ni dawa ya Madagascar. Kwa kifupi hujui chochote kuhusu suala hilo, nilichogundua toka kwako ni stamina ya ubishi tu...
 
Wewe ndiye unayeleta ubishi wa kijinga. Walitutangazia wenyewe kuwa wanakwenda kufanya utafiti, walipaswa kurudisha mrejesho.

Hoja hapa siyo dawa lishe zilizotengenezwa nchini (kwa taarifa yako nazifahamu vizuri sana) bali suala ni dawa ya Madagascar. Kwa kifupi hujui chochote kuhusu suala hilo, nilichogundua toka kwako ni stamina ya ubishi tu...
Wewe unayejua ungeandika tuone na sio kutaka kulazimisha ujinga unaouandika ndio ionekane eti ni hoja ya ukweli.
 
Wewe unayejua ungeandika tuone na sio kutaka kulazimisha ujinga unaouandika ndio ionekane eti ni hoja ya ukweli.
Nani aliyekualazimisha, naona unaleta ubishi wenu wa kijinga wa Tz vs Ke hata kwenye mambo yasiyohitaji ujinga (naona huu ndiyo msamiati wako mpya). Kwa kifupi nimeshakudharau...
 
Nani aliyekualazimisha, naona unaleta ubishi wenu wa kijinga wa Tz vs Ke hata kwenye mambo yasiyohitaji ujinga (naona huu ndiyo msamiati wako mpya). Kwa kifupi nimeshakudharau...
Aliyeanza kumquote mwingine ni nani?

Aliyeanza shobo ni wewe maana umekuja na bla bla eti mara umesikia dawa ilipotua tu wakagawana wenyewe!

Kungekuwa na sababu ya kuwatangazia mngetangiziwa ila ukiona kimya ujue hakuna umuhimu.
 
Crap!...
 
Naomba fanya utafiti, japo kidogo tu, kuhusu magonjwa yanayosababishwa na virusi (virus diseases), utanielewa...

Tangu hiki kitu kianze kuyumbisha dunia, nimetafiti hadi basi, nimekua nasoma kukihusu kila siku, na pia kukilinganisha na magonjwa mengine yakiwemo yanayosababishwa na virusi. Kwa kifupi dunia iko sahihi kwa kuchukua tahadhari hadi pale dawa ya uhakika itapatikana, na yenye bei nafuu......
 
Kumbe bado korona inawatesa? ,Tanzania korona imeshaisha maisha yamerudi kama kawaida.shule zimeshafunguliwa
Tanzania ugonjwa haujaisha, ila umepungua sana, ndio sababu serikali inasema tuchukue tahadhari
 
Tatizo vifo vinaendelea kushuhudiwa, hivyo ni vigumu kujichokea.....
Mwambie Uhuru aongeze makali ya lockdown, yani iwe marufuku mtu kutoka nje mpaka siku wagongwa wa corona wakifika negative 0 ndio mnatoka ndani!
 
Tangu hiki kitu kianze kuyumbisha dunia, nimetafiti hadi basi, nimekua nasoma kukihusu kila siku, na pia kukilinganisha na magonjwa mengine yakiwemo yanayosababishwa na virusi. Kwa kifupi dunia iko sahihi kwa kuchukua tahadhari hadi pale dawa ya uhakika itapatikana, na yenye bei nafuu......
Nakubaliana na wewe kwenye suala la kuchukua tahadhari lakini nikueleze tu kuwa magonjwa yote yanayosababishwa na virusi hayana dawa bali wanahangaika na dalili tu (symptomatically). Treatments can only help with symptoms while you wait for your immune system to fight off the virus. Antibiotics do not work for viral infections...

Imekuwa hivyo kwa magonjwa yote yakiwemo HIV/Aids, surua (smallpox), mafua (common cold/ flu), mumps, rubella, tetekuwanga (chicken pox), shingles, homa ya ini (hepatitis), mkanda wa jeshi (herpes and cold sores), homa ya kichaa cha mbwa (rabies), ebola and hanta fever, etc...
 
Kenya na covid.jpg
 
Bado tuko kwenye stage za mwisho kuanza kuigawa kwa watanzania.. 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 😉 😉 😉
 
Hayo magonjwa uliyoyataja hayaambukizi kama hiki kitu, na hayajasababisha dunia iingie kwenye lockdown, hayajasababisha tubadilishe desturi zetu za kusalimiana kwa mikono na kuziba nyuso kwa mabarakoa mpaka tunafanana mazombi.
Kwa kifupi, hiki kitu hakitaondoka kwa kuficha vichwa ardhini au kujichokea, lazima mapambano ya kisayansi yaendelee.
Huyo dogo anapenda neno la kujichokea...utadhani ni mtoto anayeanza kujifunza a e i o u....kujichokea ni nini ndugiu..kama huna msemo mingine tuambie tukupe unatuchosha sasa. Afu tu nikujibu kistaarabu ukitaka kujua mambo ya tz wala huna sababu ya kuharisha kqa usiyojua huku. Unajionesha ulivyo na hasira na roho mbaya. Tafuta wakenya ambao wamejazana huku waulize. Kama huna watafute wale wanaofahamika huku wapo wakenya kwenye timu zetu kibao wanafurahia maisha. Hicho kitu unachojifariji nachonhatuwezi fanana. Hutaki au unataka tatizo la corona limebaki historia huku. Hakuna anayekufa na kils wiki tunafunga vituo tulivyokuwa tumevitenga. Hakuna aliyejichokea huku maana hatujafungia. Tunapiga kazi kaziaana hapa ni kazi tu. Kama unaendelea kubabanywa ili tujue unajua kuchonga endelea ila siku mojs utakosa chs kubwabwanya huku. Mi nifanya kazi hospitalini tena za serekali hakuna wagonjwa wa corona. Mitaani the same. Ninyi wakenya mlikosea sana pale mlipomdharau Mungu mkajifanya wana sayasi wakati hata sayansinyenyewe inakataa lockdown zenu. Na sasa hivi mnachokipata ni fundisho kwamba Mungu hadhihakiwi. Sisi tulijua hatuwezi tukaamua kumtegemea aliyejuu ya wanasayansi wote na tumeshavuka huko hata kama ukisikia hivyo inakuuma lakin huo ndio ukweli. Unaweza tengeneza story ndefuuu but ukweli unaujua na ukweli haujifichi. Huwezi kuficha vifo wala ugonjwa. Ila kws vile unatafuta tufanane wewe endelea kuropoka tu huku sisi tunadunda. Poleni
 
Back
Top Bottom