Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akijibu swali kuhusu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kutoa tuhuma za uwepo wa mazingira ya Rushwa na kukosekana kwa Uadilifu, amesema:
“Kuhusu tuhuma ambazo Makamu (Lissu) amezitoa kuhusu uadilifu, nisisitize kwa nafasi yangu ya utendaji mkuu wa Chama ikiwa kuna Kiongozi au Mtu yoyote wa CHADEMA ana tuhuma dhidi ya yoyote aziwasilishe ili zishughulikiwe kwa mujibu wa Katiba, Itifaki na maadili ya Chama na sio kutoa tuhuma za jumlajumla bila kusema hapa kuna huyu anatuhumiwa na huyu na hili na hili.”
“Tukipata tuhuma zenye ushahidi zitapelekwa kwenye Kamati Kuu ya Chama ambayo itaamua kushughulika nayo au kupeleka Kamati ya Maadili, kama kuna jambo liletwe.”