Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Tuhuma za Lissu kuhusu Abdul kuhonga watu zinaacha maswali mengi na tata sana,
1. Kwa nini Abdul ndiye anahonga watu na sio watu wa CCM au serikali?
Kwa nini hawakutumika watu magwiji wa hiyo michezo ambao wasingeacha alama au ushahidi ikiwa wangeweza au hata wangeshindwa kumuhonga Lissu?
2.Wanawahonga CHADEMA ili iweje?
Kwani mtu si anaweza kuchukua pesa na akiendelea kuinyuka CCM na serikali tu, kauli mbiu mojawapo ya Lema akiwa anagombea Arusha alikuwa anasema kula "CCM kulala CHADEMA", alikuwa anawaambia wapiga kura wachukue hongo/takrima ya CCM lakini waipigie kura CHADEMA. Haiwezekani viongozi wa CHADEMA wanaodaiwa kuhongwa wameamua kutembea na msemo wa Lema?!
3.Pesa zinazohongwa zinatoka katika mfuko gani wa serikali ambao haujazua maswali mpaka sasa?
4.Kama kusingekuwa na hiyo hongo nini kingekuwa cha tofauti CHADEMA kwa sasa?
5.Kwa nini haya madai mpaka sasa yanahusisha Wenje na Lissu tu? Kwa nini Lissu hataji watu wengine alioambiwa wamehongwa?
6.Haiwezekani hao anaoambiwa wamehongwa hawajahongwa bali ni mchezo wa kisiasa tu? Ana ushahidi gani zaidi wa maneno ya kuambiwa kwamba kuna wengine wengi wamehongwa?
7.Lissu alikuwa anataka kuhongwa shillingi ngapi na Abdul?