KERO Madai ya malimbikizo ya madeni ya watumishi ni mchezo wa paka na panya

KERO Madai ya malimbikizo ya madeni ya watumishi ni mchezo wa paka na panya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa umma tumekua tukiomba nyaraka za madai ya madeni yetu mara kwa mara ila hayafanyiwi kazi.
Watumishi wengi wa umma wanaidai serikali malimbikizo ya madai mbalimbali ikiwemo kupanda daraja,likizo ,uhamisho nk lakini mchakato wa kulipwa imekua danganya toto.

Serikali kuu imekua na majibu tofauti na majibu yanayotolewa na halmshauri hasa kwa watumishi walio chini ya wizara ya TAMISEMI.Akijibu maswali wakati wa bunge la bajeti Naibu waziri wa Ofisi ya rais,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora mh.Riziwani Kikwete alidai kwamba waajiri ambao ni halmashauri haipeleki majina wa watumishi wanaoidai serikali malimbikizo hvo akatoa wito kwa wabunge kufatilia majina ya watumishi wanaodai.

Kinachofanyika uku halmashauri ni kwamba kila siku watumishi wanaombwa wapeleke nyaraka za kuonesha madai yao ya malimbikizo.

Ndani ya mwaka mmoja mtumishi anaweza kuombwa nyaraka hzo zaidi ya mara 7 na bado mwaka unaofata akaombwa tena ila halipwi wala nini,swali la kujiuliza je halmashauri hazina utaratibu wa kutunza nyaraka za watumishi wake? Kama jibu ni hapana basi inakuaje mtumishi anaombwa kuwasilisha nyaraka zile zile zaidi ya mara tano kwa mwaka? Hii hali inaleta dhana kwamba nyaraka hizi zinakusanywa na kutelekezwa bila kufanyiwa kazi ndio maana kila linapokuja tamko la kisiasa kuhusu madeni ya watumishi basi wanaomba nyaraka ili kutuliza upepo.

Ombi langu kwa Serikali na hasa halmashauri zinatakiwa kutoa orodha ya majina ya watumishi wote waliowasilisha nyaraka za madeni na kuthibitishwa kwamba madai yao ni halali, hii itasaidia watumishi kujua hali (status) ya madeni yao na kujijua kama humo ndani ya orodha ya wadai na kama haumo basi ufanye ufatiliaji ikiwemo kuwasilisha nyaraka za madai.Tofauti na sasa unakua kila muda unaambiwa peleka nyaraka.

Pili kwa wale ambao madeni yao yamethibitishwa ni halali basi madeni hayo yaingizwe kwenye mfumo wa ESS ili mtumishi aweze kuona deni analoidai serikali kama vile ambavyo mtumishi kwa sasa anavoona deni analodaiwa na bank,bodi ya mkopo au taasisi nyingine za kifedha.

Tatu halnashauri ziwe na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za watumishi wake.Nyaraka zinazodai haki za mtumishi mara nyingi uwa hazitunzwi kama nyaraka za kumchukulia hatua za nidhamu mtumishi.ukiwa na kosa la kinidhamu nyaraka zote wanazo hata za mwaka 1960 ila ukidai haki zako wanaanza janja janja hasa maafisa utumishi na watu wa kutunza kumbukumbu.
 
Mwisho wa mwaka wa serikali watalipa yote hold on tarehe si ndo hizi hizi?
 
Kuna Mzee wangu hapa Job kabakiza miaka 3 kustaafu,,, but anadai arrears zake za tokea 2012 alivyopanda daraja.
Nahisi watamuunganishia pamoja na Kiinua Mgongo chake😁
 
Back
Top Bottom