Madai ya Refund ya Wanafunzi Chuo cha DUCE, Uongozi wasema umeshalipa waliosalia ni Wanafunzi 11

Madai ya Refund ya Wanafunzi Chuo cha DUCE, Uongozi wasema umeshalipa waliosalia ni Wanafunzi 11

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna Wanafunzi wa Chuo cha DUCE (Dar es Salaam University College of Education) wamekuwa wakizungushwa kupata malipo yao ya “refund”, kwa kile alichoeleza kuwa Idara ya Fedha ya DUCE inawasumbua, ufafanuzi umetolewa na Chuo husika.

Mwanachama huyo alieleza kuwa Refund hiyo ni pesa ambazo Wanafunzi wanapaswa kurudishiwa baada ya wao kulipa ada ya masomo kwa makubaliano kuwa Serikali ikiingiza fedha zao za mkopo watrejeshewa.

Kusoma kile kilichoandikwa na Memba bonyeza hapa ~ Pesa za refund chuo cha DUCE ni kizungumkuti

UFAFANUZI WA CHUO
JamiiForums imewasiliana na Afisa Uhusiano wa DUCE, akasema anawasilisha hoja hiyo kwa uongozi na baada ya muda majibu kutoka Idara ya From Deputy Principal - Planning, Finance and Administration (Naibu Mkuu - Mipango, Fedha na Utawala) yakarejeshwa yakiwa na ufafanuzi huu:

“DUCE tumekamilisha malipo ya refund kwa Wanafunzi wote ambapo kiasi cha Shilingi 90,143,050 kimelipwa kwa Wanafunzi 186.

“Kesi inayozungumzwa ni ya Wanafunzi 11 ambao cheque yao ilikuwa deposited benki lakini ikabounce kutokana na majina ya akaunti kutofautiana.

“Hivyo, ililazimu kuwatafuta Mwanafunzi mmojammoja ili kupata majina na akaunti sahihi. Suala hilo lilikamilika na malipo ya Wanafunzi hao kupelekwa benki ambapo leo Jumatano tarehe 3 Julai 2024 ilitarajiwa wawe wamewekewa kwenye akaunti zao.

“Hivyo, kwa ujumla kesi inayozungumzwa ni ya Wanafunzi 11 wa mwisho kati ya 186, ambapo wengine 10 walieleweshwa na kuelewa.”
 
Back
Top Bottom