John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Sakata la maji ya Mto Mara kubadilika rangi huku Samaki wakifa ikielezwa kuwa kuna kemikali za sumu limechukua sura mpya baada ya malaka husika kutoa kuhusu kinachoendelea.
Maji hayo yamebadilika rangi na kuwa meusi huku wakazi wanaoishi katika vijiji vilivyopo kandokando ya Mto Mara wakiwa hawatumii maji hayo tena kwa matumizi ya nyumbani.
Serikali Mkoani Mara imezuia matumizi ya maji hayo kwa wananchi wake kutokana na maji hayo kupoteza sifa ya kuwa maji safi na salama.
Pia Serikali imezuia shughuli za uvuvi zinazofanyika katika mto huo pamoja na ulaji wa samaki zinazotoka ndani ya mto huo.
Awali, kabla ya taarifa hiyo kutolewa kulikuwa na madai ya chinichini kuwa sumu hiyo ya kwenye maji imetokana na matumivi ya kemikali kutoka kwenye midogo iliyopo maeneo husika japo hakuna uthibitisho rasmi juu ya hilo.
SABABU MAJI YA MTO MARA KUWA MEUSI
Baada ya sintofahamu hiyo ya maji ya mto Mara katika eneo la Kirumi, Bodi ya Maji bonde la Ziwa Victoria imekuja na taarifa za uchunguzi wa awali baada ya kuchukua sampuli ya maji ya mto huo.
Mkurugenzi wa bodi hiyo, Renatus Shinhu amesema katika maji hayo wamebaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta pamoja na kukosekana kwa gesi ya Oksijeni kwenye maji hayo.
“Baada ya bodi kuchukua sample yam aji ya maeneo hayo tumegundua kuwa kuna kiwango kikubwa cha mafuta oil na grease kuliko kiwango kinachokubalika, kitu cha pili ni kukosekana kwa hewa ya oxygen kwenye maji.
“Hivyo kukosekana kwa oxygen kwenye maji kumetokana na kiwango kikubwa cha mafuta, kuhusu rangi ya maji kuwa meusi uchunguzi bado unaendelea,” - Renatus Shinhu.
Source: Clouds TV
Pia soma > Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu Mto Mara