Madai ya Trump kuwa "Venezuela Ilituibia Mafuta" Yana Mashiko?

Madai ya Trump kuwa "Venezuela Ilituibia Mafuta" Yana Mashiko?

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351

Watu wengi mtakuwa mmeiona hii video ya Donald Trump akisema "we want our oil back" Tafsiri ya karibu ni "tunataka turudishiwe mafuta yetu". Trump anaonekana akidai hadharani kuwa mafuta ya Venezuela ni haki halali ya Marekani kiasi kwamba watu wanajiuliza kuwa "Hii video ni AI?" au "Trump ameanza kuchanganyikiwa?" Hakuna AI ila inawezekana Trump ameanza kuchanganyikiwa. Yale yalikuwa maneno yake halisi. Alisema hivyo jana, Desemba 18, 2025, akiwa katika kambi ya jeshi ya Joint Base Andrews (JBA), Wakati akijibu maswali ya waandishi kutetea msimamo wake wa vikwazo na blockade dhidi ya Venezuela.

Video hii imeibua mjadala na kufanya iswe tena dhana bali ni suala la wazi kuwa lengo la kusumbuana na Utawala wa Maduro sio madai ya Madawa ya kulevya wala kukosekana kwa Demokrasia nchini Venezuela ila ni hila za kutaka kunufaika na mafuta ya nchi hiyo.

Swali hapa haya madai ya Marekani kuwa Mafuta ya Venezuela ni ya kwao yanaanzia wapi?

Anachokizungumzia Trump ni tukio la kihistoria la miaka ya 1970.
Mnamo 1976, serikali ya Venezuela chini ya Rais Carlos Andrés Pérez ilitaifisha sekta yote ya mafuta na kuunda kampuni ya taifa PDVSA (Petróleos de Venezuela Sociedad Anónima). Kabla ya hapo, kampuni za kigeni, hasa za Kimarekani zilikuwa zikidhibiti karibu uzalishaji wote wa mafuta nchini humo:
Makampuni ya Kimarekani yaliyokuwa yamewekaza nchin Venezuela ni pamoja na;
  • Standard Oil of New Jersey (sasa ExxonMobil)
  • Creole Petroleum
  • Gulf Oil
  • Mobil
na zinginezo.

Marekani ilikuwa imewekeza mabilioni ya dola katika miundombinu, uchimbaji na usafirishaji. Utaifishaji ulifanyika kisheria chini ya sheria za Venezuela na kampuni zililipwa fidia (ingawa wengine wanasema fidia haikuwa ya haki kabisa).

Trump sasa anafufua hii "zombie case" ya miaka 50 iliyopita ili kuhalalisha sera yake ya blockade na maximum pressure dhidi ya serikali ya Maduro. Anadai kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwamba mafuta ya Venezuela "ni yetu" na yalichukuliwa kinyang'anyi. Jambo ambalo ni exaggeration kubwa ya kihistoria.

Kwa wazi, anachanganya utaifishaji wa 1976 (ulio na fidia) na matukio ya baadaye chini ya Hugo Chávez (2007) ambapo kampuni kama ExxonMobil na ConocoPhillips zilinyang'anywa hisa zao katika eneo la Orinoco Belt bila fidia ya kuridhisha, na zilishinda kesi katika mahakama za kimataifa iliyoitaka Venezuela kuzilipa mabilioni kampuni hizo.

Kwa nini Trump anaiibua ajenda hii sasa? Dhana kubwa ni juu ya mgogoro unaoendelea wa Essequibo na Guyana, ambapo ExxonMobil inachimba mafuta katika eneo la bahari linalodaiwa kuwa sehemu ya Venezuela, na Trump anaona nafasi ya kujimwambafai dhidi ya Caracas.

Ukweli ni kwamba Venezuela ilifanya utaifishaji wake kama haki yake ya kitaifa, kama zilivyofanya nchi nyingi za OPEC kipindi hiko. Trump anatumia historia hii kwa narrative ya kisiasa ili ku-justify vikwazo.

Baada ya Tamko hili tayali nchi tofauti ikiwemo China imeonesha msimamo wake wa kuiunga mkono Venezuela kitu wachambuzi wa siasa za kimataifa wanadhani, inaweza kuleta mvutano zaidi kati ya Marekani na China kuelekea 2026.
Ikumbukwe China ndiyo mnunuzi mkuu wa mafuta ghafi kutoka Venezuela, ambayo yanachangia takriban 4% ya bidhaa zake zinazoagizwa kutoka nje, huku kwa mwezi Desemba ikitarajiwa tu ikarajiwa kuagiza wastani wa zaidi ya mapipa 600,000 kwa siku.

China imeweka wazi kuwa inapinga aina zote za "unyanyasaji unaosikiliza upande mmoja (unilateral bullying)" na inaunga mkono nchi zote katika kulinda uhuru wao na hadhi ya kitaifa, Maneno haya yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi wakati akizungumza na mwenzake wa Venezuela Yvan Gil kupitia simu.
Hata hivyo alipoulizwa kama "uchokozi" wa Marekani dhidi ya Venezuela unaweza kuziweka China na Marekani katika mgogoro wa moja kwa moja kwenye eneo hilo, msemaji serikali ya Venezuela alirudia tu maneno ya Wang Yi na hakuongezea chochote.
 
(ingawa wengine wanasema fidia haikuwa ya haki kabisa).
Uzi ungeishia hapa tu!!
Anyway kama kampuni za USA zilionewa basi zingefungua kesi za madai au mashauri kwa arbitration ambazo nchi zote mbili zitaridhia ila hii solution ya kivita sidhani kama ina tija yoyote zaidi ya kuleta mgogoro kama wa Syria ambapo mataifa makubwa yakitoshana nguvu, vita haitoisha
 
When the subject is drug cartel,why target oil tanker?

Hii ilijulikana toka mwanzo kua issue ni oil na sio drugs,
Kama ni drugs,nchi nyingi tu zinazalisha na kusafirisha US hasa nchi za South America.
 
Pamoja na yote na hujuma ila najua hawezi vamia directly pale Venezuela china na Russia wanaweza kuwepo hapo hilo nalo ni tatizo jipya kwa america
Mcha mbuzi habari...humu jukwaani munadanganyana mno je wako wapi Russia na China?
 
Kumtegemea urusi na china ni sawa na kumtegemea mchepuko ukusaidie ukikosana na mama yako
 
Pamoja na yote na hujuma ila najua hawezi vamia directly pale Venezuela china na Russia wanaweza kuwepo hapo hilo nalo ni tatizo jipya kwa america
Russia amechoka., anapambana na hali yake sasa kwa miaka 4 hajui itsishaje 😅😅😅
 
Back
Top Bottom