Madai ya Wafanyabiashara wa Kariakoo dhidi Ya Wachina ni ya kweli ?

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,616
Reaction score
14,106
Muda huu nasikia kipindi cha Good Morning,kinacho rushwa na WSF na Kuna shutuma zinatolewa kwa Wachina kwamba wamekuwa chanzo Cha matatizo kadhaa hapa nchini.

Wachina wanashutumiwa kusababisha uhaba wa dola,hawatoi risiti,hawana vibali vya Kazi,wanafanyakazi za wazawa nk

Binafsi naomba kuuliza humu kwa GT ,kwamba hizi shutuma dhidi ya Wachina niza kweli zote au zingine zimetiwa chumvi na wafanyabiashara baada ya kukutana na changamoto mpya za kibiashara toka kwa wageni ?

Na,pia mamlaka zetu hazioni jambo hili ?ambalo mwananchi analiona na kulalamika ila mamlaka ziko kimya tu,bila kuchukua hatua stahiki ?
 
Ni chuki za mtu mweusi pale anapohisi fursa zake za kiuchumi ziko hatarini. Wachina wanauza bidhaa kwa bei ya chini mno hivyo wateja wengi hukimbilia kwao na hilo limekuwa pigo wa "wazawa" waliozoea kujipatia faida mara tatu au nne ya mtaji wao!
Solution ni wakubali kushusha bei ya bidhaa waende sawa na wachina au watafute biashara nyingine maana hili ni soko huria.
Wachina wana maduka, wanalipa kodi na wamesajili biashara zao aidha kwa majina yao au majina ya wake zao (ambao ni watanzania)
Kama tulivyoruhusu Wahindi, Waarabu na Wasomali kulitawala soko basi tuwaache Wachina pia wafanye yao.
 
Mamlaka zetu haziaminiki kabisa, watendaji wake ni waroho sana na Hawana nguvu za kuishinda dhambi ya kula rushwa
Ushawahi nunua chochote kwa mchina maisha yako yote. Chochote kwa mchina yoyote, popote pale duniani?
Na kama ndio ulinunua akiwa wapi?
 
Muda huu nasikia kipindi cha Good Morning,kinacho rushwa na WSF na Kuna shutuma zinatolewa kwa Wachina kwamba wamekuwa chanzo Cha matatizo kadhaa hapa nchini.

Wachina wanashutumiwa kusababisha uhaba wa dola,hawatoi risiti,hawana vibali vya Kazi,wanafanyakazi za wazawa nk

Binafsi naomba kuuliza humu kwa GT ,kwamba hizi shutuma dhidi ya Wachina niza kweli zote au zingine zimetiwa chumvi na wafanyabiashara baada ya kukutana na changamoto mpya za kibiashara toka kwa wageni ?

Na,pia mamlaka zetu hazioni jambo hili ?ambalo mwananchi analiona na kulalamika ila mamlaka ziko kimya tu,bila kuchukua hatua stahiki ?
Si mlikua mnawasema wasouth kuwa wanawafukuza wageni kwa sababu wanachukua ajira zao na nyie mbona mnawaonea wivu wachina mmezoa kupandisha vitu bei
 
Wameshazoea faida mara 3+ washenzi hao.
Uwe na akiba ya maneno

Screenshot_20250318-090012.jpg
 
Kwa hiyo siku hizi hakuna haja ya kwenda China kufata mzigo, wachina wanaleta wenyewe hadi kariakoo?
Yes hiyo nzuri, pesa za safari za china na Accomodations unaongezea stock
 
Muda huu nasikia kipindi cha Good Morning,kinacho rushwa na WSF na Kuna shutuma zinatolewa kwa Wachina kwamba wamekuwa chanzo Cha matatizo kadhaa hapa nchini.

Wachina wanashutumiwa kusababisha uhaba wa dola,hawatoi risiti,hawana vibali vya Kazi,wanafanyakazi za wazawa nk

Binafsi naomba kuuliza humu kwa GT ,kwamba hizi shutuma dhidi ya Wachina niza kweli zote au zingine zimetiwa chumvi na wafanyabiashara baada ya kukutana na changamoto mpya za kibiashara toka kwa wageni ?

Na,pia mamlaka zetu hazioni jambo hili ?ambalo mwananchi analiona na kulalamika ila mamlaka ziko kimya tu,bila kuchukua hatua stahiki ?
kwani hao wabongo wenyewe wanatoa risiti, kariakoo ukiomba risiti wanakuona kama mchawi, mtu unaomba risiti anakutolea jicho hilo kama umemkosea
 
Kama bidhaa zote tunanunua China basi bora waje watuuzie huku huku ili kuepusha hao mawinga wanaojiita wafanyabiashara wa Kariakoo. Hao "mawinga" wanaolalamika dola wakafanye shughuli za kuleta dola kama kuzalisha viwandani, kuchimba, kulima parachichi kisha waexport.
 
Back
Top Bottom