Muda huu nasikia kipindi cha Good Morning,kinacho rushwa na WSF na Kuna shutuma zinatolewa kwa Wachina kwamba wamekuwa chanzo Cha matatizo kadhaa hapa nchini.
Wachina wanashutumiwa kusababisha uhaba wa dola,hawatoi risiti,hawana vibali vya Kazi,wanafanyakazi za wazawa nk
Binafsi naomba kuuliza humu kwa GT ,kwamba hizi shutuma dhidi ya Wachina niza kweli zote au zingine zimetiwa chumvi na wafanyabiashara baada ya kukutana na changamoto mpya za kibiashara toka kwa wageni ?
Na,pia mamlaka zetu hazioni jambo hili ?ambalo mwananchi analiona na kulalamika ila mamlaka ziko kimya tu,bila kuchukua hatua stahiki ?