Madai ya Wafanyabiashara wa Kariakoo dhidi Ya Wachina ni ya kweli ?

Wafanyabiashara wetu sio waaminifu katika suala la bei na kuagiza bidhaa kupitia online market,wengi bei zao ni ghali na huwapelekea Wateja bidhaa sio huko mikoani.
 
Si mlikua mnawasema wasouth kuwa wanawafukuza wageni kwa sababu wanachukua ajira zao na nyie mbona mnawaonea wivu wachina mmezoa kupandisha vitu bei
Sijawaone wivu Wachina,bali nimeuliza madai ya wafanyabiashara wetu pale k-koo yana ukweli ?
 
Nakubali Wachina, wapelekeeni moto hadi waombe po. Haiwekani TV ya 350,000 uniuzie 600,000.

Kariakoo bila Uwinga Uchwara inawezekana.
Alafu tunaona ndo ujanja kesho na kesho kutwa biashara ikiwa ngumu unaanza kulalamika kumbe ni sababu ya ujinga wako kuuza bidhaa bei isito halali
 
Watanzania wanalalamika kupewa elimu ya jinsi ya kufanya biashara na Wachina! Inashangaza sana​
Yeah. WaTz wanapewa Tuition ya jinsi ya kufanya biashara bila ada au kutoa mchango wa Ushiriki (bure) halafu tena wanalalamika badala ya kushukuru.
Ni kweli Inashangaza sana.
 
Yeah. WaTz wanapewa Tuition ya jinsi ya kufanya biashara bila ada au kutoa mchango wa Ushiriki (bure) halafu tena wanalalamika badala ya kushukuru.
Ni kweli Inashangaza sana.
Elimu ya bure inakataliwa, wapewe nini Watanzania?​
 
Vitu vingine vipo exaggerated vingine ni kweli.

Ila vingi ulivyosema ni kweli ila sio kwa 100%.

Wapo wachina wenye mitaji mikubwa na wenye uwezo wa ku supply kariakoo bila uhaba, na wapo wachina Mawinga na wao wananunua na kuuza.

Issue ya Risiti sisi pia tuna matatizo, mtu akitajiwa bei anasema sitaki risiti nipunguzie, ila hata kama wasipotoa risiti still kodi anayokwepa ni ndogo sababu ameshapitia bandari, Wakwepaji wakubwa wa kodi ni wafanyabiashara wa kati na wadogo.

Vibali vya kufanya kazi maybe, ila sidhani kama ni issue sana kwao, Vibali sio gharama nchi hii na sidhani kama wanashindwa kulipa.
 
Kuna kazi waruhisiwe wageni wawekezaji lakini sio kazi ya rejareja ya kushindana na mtanzania mitaani au sokoni.
 
Ikumbukwe, kwa Tabia; waTz wanaUnafiki wa kificho. e.g. hao wafanya biashara hawasemi au hawataji kero yao wazi-wazi bali Wanawalalamikia Mchina lakini mbona hata kabla ya ujio wa mchina waliwahi kuwalalamikia Machinga?
Hoja hapo ni kwamba UKWELI wanataka wawe hapo sokoni WAO WENYEWE hawauwezi ushindani wa kibiashara-Hawamudu kukuru-kakara za soko huria. Na wakiweza kuwatoa wachina hapo kwa mizengwe au kwa namna yoyote ile wanarudi kwenye ule mtindo wa kufanya biashara kwa mazoea(Business as usual)
 
Aliyewaruhusu kuingia nchini na kufanya hizo kazi walikubalianaje nao?
 
Hii nchi inatatizo kubwa sana la ajira, kuna vijana wengi sana hawajaajiriwa almost miaka 10 tangu wamalize vyuo.
Ukiangalia comments za watu wengi hapa utaona kabisa hawajali, au hawaelewi wanazungumza nini!huwezi toka hapa Tz hata kama una mtaji ukapenya kwenye masokoya hapa hapa Africa achana na China ambapo ni pagumu sana kwa forigner kufanya wanachokifanya hawa machinga wa kichina.

Matatizo haya haya ndio yalileta Xenophobia SA, ni lazma hawa watu wafanye walichosema wamekuja kufanya,(Uwekezaji) sio uchuuzi,wachuuzi ndio watanzania wanafanya na kupata walau chochote kitu kuendesha maisha.

Kwa hali inavyoenda ni lazma serikali ichukue hatua kali sana na madhubuti,otherwise hili bomu litakuja kuwalipukia,uwezo wa serikali kuajiri watu wake ni mdogo sana,tumeona issue ya waalimu na TRA majuzi hapa,lazma tulinde hichi kidogo Kkoo na Tz kwa ujumla kwa kuangalia tunadeal vp na hawa wachuuzi wa kichina,tukicheka naye kkoo yote itakuwa yao!..
Sisi tutakuwa soko lao na hatutaweza kukompete!

God bless Tz!
 
Wachina wameporomosha bei ya bidhaa mara tatu hadi saba. Kitu ambacho mfanyabiashara wa Tanzania alikuwa akiuza kwa cha laki na nusu mchina anauza elfu hamsini.




Je watanzania wenzetu walikuwa wanatupiga pesa ndefu? Je walikuwa wanapata faida mara 3 hadi mara kumi?


Mwenye maelezo kamili angeelezea
 
Nimejiuliza wachina wanafanyaje kuuzia wanachi LUKU kwa bei rahisi? Kuna mmoja amesema ukitoa elfu 25 unapewa Unit 100 yaani Bei Kitonga nusu nzima.
 
Yes hiyo nzuri, pesa za safari za china na Accomodations unaongezea stock
Wachina wengine wanauza bidhaa mpaka vijijini hadi kwenye minada na magulio ya vijiji vya ndanindani. Wachina wengine wanauza bidhaa hadi kwenye mitumbwi visiwani ndani ndani. Nguo ya 20000 kwa mtanzania mchina anauza elfu saba
 
Tatizo watanzania tumezidi udalali ukienda Kaliakoo ukitaka jins ya 19 utauziwa 23 udalali umezidi bora wachina bei zao zimenyoka 💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…