Madai ya Wanafunzi kusomea chini ya mti Shule ya Msingi Kwembe (Dar), Serikali yasema walikuwa katika programu maalumu

Madai ya Wanafunzi kusomea chini ya mti Shule ya Msingi Kwembe (Dar), Serikali yasema walikuwa katika programu maalumu

Idadi ya waliofanya mtihani ni ileile idadi ya wanaofanya masahihisho, kwa nn wasifanyie kwenye darasa walilofanyia mtihani?
Mazuzu mpo wengi humu jf siku hizi
Yaani unahoji mbinu za fundishaji wa mwalimu? Inawezekana aliwatenga vipanga wasiohitaji sana usimamizi wakae darasani waendelee kufanya maswali
Halafu masanga upepo kama wewe wanahitaji kusimamiwa tit fo tati huku wakipunga upepo nje
 
KUKANUSHA TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MWANDISHI DICKSON NG'HILY NA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO

Kumekuwa na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kumkamata mwandishi wa habari ambaye pia ni Mhariri wa biashara na Mkuu wa Kitengo cha Mtandaoni (digital) Ndugu Dickson Ng'hily kutoka Gazeti la The Guardian.

Taarifa hiyo imeeleza pia mwandishi huyo alipigwa sana na kuumizwa kwenye mkono na simu yake kuvunjiwa kioo huku sababu ikielezwa kuwa ni kupiga picha wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe waliokuwa wanasoma chini ya mti. Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa mwandishi huyo alipelekwa ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye kushikiliwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kukanusha taarifa hiyo iliyoleta tahahuruki kwa wananchi na waandishi wa habari. Ukweli ni kwamba mwandishi huyo hakupigwa na mtu yeyote isipokuwa aliulizwa na Mwalimu Mkuu kwa nini anapiga picha bila ridhaa yao wala kujitambulisha.

Baada ya mwandishi huyo kukataa kutoa ushirikiano alipelekwa Ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye akapelekwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujiridhisha kama kweli ni mwandishi na ana kibali cha kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo leo Julai 10, 2024, Mhe. Mkuu wa Wilaya alikuwa kwenye ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mburahati na hivyo hakuhusika wala kutoa amri yoyote kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo.

Aidha, ni kweli kuwa wanafunzi walikuwa nje ya madarasa yao kwa ajili ya programu maalumu ya kufanya masahihisho ya mtihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inathamini na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kufanikisha kazi yao muhimu ya kuhabarisha Umma juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo, ni muhimu Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo katika kutimiza haki yao ya kutafuta, kuchakata na kusambaza habari.

Joina Nzali
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Taarifa za nyuma kuhusu tukio hili soma bofya hapa:
~ THRDC yakemea Mwandishi wa Habari kukamatwa kwa kupiga picha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe wakisoma chini ya mti

~ Mwandishi wa Habari wa The Guardian anadai amepigwa na Walimu baada ya kupiga picha Wanafunzi wakisoma chini ya miti
Hapa imekaa sawa sio wananchi wanakaa serikali haijibu kitu wala hailezi utafikiri serikali ni gogo kumbe ni watu!
 
Una akili kidogo sana ,madarasa A,B,C,D wakae chumba kimoja

USSR
Mwenye Akili nyingi umeng'amua kuwa madarasa A,B,C,D sasa hv yame condense au yamebomoka hvyo hawawezi fanyia masahihisho sio? Shule haina Bwalo la hata kuhifadhi wanafunzi mikondo minne? Less than wanafunzi 180?

Hivi guts za kutetea huu uhuni unazitoa wapi we popoma?

Wasomee madarasa A,B,C na D, mitihani wafanyie humo, masahihisho tu ndo wafanyie kwenye mchanga, hata kama unajiita mwenye akili basi hizo akili ni kama za ndugu zako kina Msukuma na Lusinde!
 
Wewe utakuwa punguani kabisa.

Ufahamu kuwa, hata leo hii ukianzisha shule, kigezo kimojawapo muhimu ili upate kibali, pamoja na kuwa na madarasa, ni lazima shule iwe na ukumbi. Lengo mojawapo la ukumbi ni kutumika kwenye matukio yanayohusisha wanafunzi wengi. Yaani ukumbi unaweza kuwahifadhi hata wanafunzi wote kwa mara moja.

Hiyo shule inayoshindwa kuwa chumba hata cha kuwahifadhi japo wanafunzi wa darasa moja tu, itakuwa ni shule zile duni kabisa.

Tunafanya matumizi ya hovyo ya kutapanya pesa za nchi kama kuzurula nje na wasanii, kunua magoli, misafara mirefu ya watawala, wakati hata vitu basic kabisa, hatuna!!
Popoma USSR .....
 
Mazuzu mpo wengi humu jf siku hizi
Yaani unahoji mbinu za fundishaji wa mwalimu? Inawezekana aliwatenga vipanga wasiohitaji sana usimamizi wakae darasani waendelee kufanya maswali
Halafu masanga upepo kama wewe wanahitaji kusimamiwa tit fo tati huku wakipunga upepo nje
Hawana bwalo la kuhifadhi wanafunzi 180 as moja kigezo cha kuanzishwa shule?....Nawe unajiita Genius?
 
Mimi niko bado na mwandishi, kasema amekuwa akipita kila mara anawaona nje. Ndiyo akaamua awapige picha kwa matumizi ya baadaye.

Pamoja na hii barua kukanusha, sasa ndiyo mtashangaa madarasa mapya yanajengwa, baada ya kuumbuliwa. Tumeshaona video nyingi, watoto wanasomea nje au darasa mbavu za mbwa. Jengeni madarasa acheni kununua magari ya gharama.
 
Safi sana, makanjanja wa habari wengi, mitandao imejaa habari za uongo.
Ni ngumu sana kwa nchi kama Tz kuendelea ikiwa na waislam.. wao hakuna wanachojua zaidi ya kuridhika na mtawala akiwa dini yao. Mengine yote hawayaoni. Huu upuuzi huwez kuona kwa wakristo, hili limedhihirila kipindi cha magufuli.. aliluwa akipogwaa spana hata na kanisa lake. Ni masikitiko makubwa kuwa kwenye jamii iliyojaa wapuuzi kama hawa. Wako waislam wachache sana wanaojitambua haswa wanaotoka bara ila pwani yote ni masifuri kichwani. Wanachojali wao ni vigodoro na ndoa saba...shwain kabisa
 
Idadi ya waliofanya mtihani ni ileile idadi ya wanaofanya masahihisho, kwa nn wasifanyie kwenye darasa walilofanyia mtihani?
Wakati wa mitihani huwa wanatumia madarasa ya shule nzima ikibidi kwa vile mkondo mmoja wa darasa la mtihani ni wanafunzi 25 sasa wakiwa watahiniwa 200 ina maana ni mikondo 8,ndio maana siku za mitihani ya mock na ile ya taifa wanafunzi wengine hawaendi shuleni.
 
Mimi niko bado na mwandishi, kasema amekuwa akipita kila mara anawaona nje. Ndiyo akaamua awapige picha kwa matumizi ya baadaye.

Pamoja na hii barua kukanusha, sasa ndiyo mtashangaa madarasa mapya yanajengwa, baada ya kuumbuliwa. Tumeshaona video nyingi, watoto wanasomea nje au darasa mbavu za mbwa. Jengeni madarasa acheni kununua magari ya gharama.
Mwandishi angekuwa makini angepata picha Bora kabisa kuzidi hizo alizopiga.Amefanya serikali ijibu kirahisi tu hoja yake.Laiti kama angefanya timing nzuri angepata picha ambazo Ingekuwa ngumu Kwa serikali kujibu.Ukiona Kuna jambo limetokea ujue Kuna mambo mengi Sana yaliyojificha.
 
Ni ngumu sana kwa nchi kama Tz kuendelea ikiwa na waislam.. wao hakuna wanachojua zaidi ya kuridhika na mtawala akiwa dini yao. Mengine yote hawayaoni. Huu upuuzi huwez kuona kwa wakristo, hili limedhihirila kipindi cha magufuli.. aliluwa akipogwaa spana hata na kanisa lake. Ni masikitiko makubwa kuwa kwenye jamii iliyojaa wapuuzi kama hawa. Wako waislam wachache sana wanaojitambua haswa wanaotoka bara ila pwani yote ni masifuri kichwani. Wanachojali wao ni vigodoro na ndoa saba...shwain kabisa
Huko unafika mbali, Uislam unaharibiwa jina na poyoyo kama huyo lakini Uislam na Waislam ni wema sana.

Kwenye msafara wa mamba, kenge hawakosekani. Lakini usitake kuwaponda Waislam wte kwa kosa la mmoja au wawili.

Huyo kafanya makosa kafahamishwa na kakiri kweli kafanya makosa. Ajenge sasa mabweni afate sheria zote ndiyo achukuwe wanafunzi.
 
Hawana bwalo la kuhifadhi wanafunzi 180 as moja kigezo cha kuanzishwa shule?....Nawe unajiita Genius?
Kwanza sijasema mimi ni genius ila nakumbuka mwalimu wetu wa mathe alikuwa anatumwaga nje tunafanya hesabu huku tumekaa chin ya miti tukipata kipupwe safi siyo kwamba madarasa hayakuwepo ila ilikuwa mbinu yake ili tusiigiliziane oya nilijikuta napenda hesabu na nikapata A
 
Mazuzu mpo wengi humu jf siku hizi
Yaani unahoji mbinu za fundishaji wa mwalimu? Inawezekana aliwatenga vipanga wasiohitaji sana usimamizi wakae darasani waendelee kufanya maswali
Halafu masanga upepo kama wewe wanahitaji kusimamiwa tit fo tati huku wakipunga upepo nje
Kama wewe ulivyo zuzu!
 
Back
Top Bottom