Madaktari 100+ wapata kazi nje ya nchi

Madaktari 100+ wapata kazi nje ya nchi

Sasa wanangoja nini? mbona wengi sana tu wako huko toka zamani? waende tu. Kwani wanaikomoa Serikali? Unanchekesha!

Wasisahau kuwatumia shangazi zao dola za matumizi.
 
Hii serikali itatumaliza wananchi wa hali ya chini tunaotegemea kutibiwa kwenye hospitali za serikali. Haiwekani kiongozi wa nchi ufanye maamuzi kisiasa eti madaktari msiporudi kazini mtakuwa mmejifukuzisha kazi!! Kwanza serikali ilitakiwa iwabembeleze madaktari kutokana na mishahara kiduchu inayowapa kwa kazi ngumu na hatarishi bila vifaa vya kisasa. Madaktari wetu pamoja na utalaamu wao hawana thamani katika nchi yao wenyewe badala yake wanathaminiwa nje ya nchi wakienda kufanya kazi. Wanasiasa wengi huwa hawana nia nzuri kwa watu wao ni waauji.
 
Kuna nchi nyingine wanawathamini sana Wataalamu wa nyanja mbali mbali toka Tanzania na siyo kudharauliwa kama wanavyofanyiwa nyumbani. Halafu Serikali itaanza kulalama tuna upungufu mkubwa wa madaktari nchini!!! Hongera zenu.
 
Sasa wanangoja nini? mbona wengi sana tu wako huko toka zamani? waende tu. Kwani wanaikomoa Serikali? Unanchekesha!

Wasisahau kuwatumia shangazi zao dola za matumizi.

Tatizo ni kuwa wamesomeshwa kwa gharama ya serikali na serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwalea wanaenda kuwapa faida mataifa mengine.
 
Tatizo ni kuwa wamesomeshwa kwa gharama ya serikali na serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwalea wanaenda kuwapa faida mataifa mengine.

...Siyo kosa lao Mkuu na wala wao si wa kulaumiwa, kama Serikali iliyowasomesha haiwathamini basi ni lazima watafute sehemu ambapo utaalamu wao utathaminiwa na wao kulipwa ujira ambao utakidhi gharama za maisha.
 
Back
Top Bottom