Madaktari baadhi yenu shida ni nini mtu anapotaka kufanya maamuzi yake?

Madaktari baadhi yenu shida ni nini mtu anapotaka kufanya maamuzi yake?

Kila mwezi nina siku zangu tatu za kuumwa tumbo na kichwa kwa sababu ni kitu ambacho siwezi kukwepa. Sasa safari hii hali ilikuwa tofauti hata nilipomeza dawa za maumivu hazikunisaidia kutuliza chochote japo kwa saa moja. Hivyo ilibidi niende tu hospital nikawaeleza nikachomwa sindano ya maumivu wakasema nyingine ni baada ya saa8, kilichofuata ni kama nilienda kujiongezea tatizo la kichefuchefu, mwili kuwasha na kuvimba hata sikurudi kwa ajili ya sindano ya pili.

Nilijikaza nikalala na matumaini labda dawa inafanya kazi asubuhi nitaamka na nafuu lakini ndio kwanza mwili umezidi kuwasha na kuvimba. Imebidi nirudi hospital kuwaambia, kwa mara ya kwanza wakasema ni allergy imesababishwa na dawa na sijawahi kuwa na hilo tatizo katika kumbukumbu zangu.

Yote haya ni kwa sababu ya kuumwa tumbo, lakini sasa nilishachoka na madaktari kila nikiwaambia tuchukue maamuzi magumu ya kunisaidia ili niondokane na hii shida mazima hawajawahi kukubaliana na mimi, majibu yao ni haya;

-Wewe huna mtoto huwezi toa kizazi sasa
-Haya maamuzi yanasababishwa na maumivu ya muda uliyo nayo yakitulia utajutia
-Kwa sasa ni mapema sana subiri umri uende
-Usichukue maamuzi ambayo utakuja kuyajutia badae
-Wewe hujawahi shuhudia vile watu wanaumwa tatizo lako ni dogo

Lakini madaktari kwani ni nani alisema lazima kila mtu awe na watoto? na mbona kiungo ni changu, maumivu napata mimi, shida napata mimi mwenyewe, kero naiona mimi mwenyewe lakini wanakuwa wagumu kufanya nachotaka. Kuna muda nakereka mpaka nahisi kama nachazika
Any doctor guesses the condition of his her patient

So ndo maana anauliza
 
Fanya uzae.kweli ukizaa shida hyo inaisha
Kabla sijazaa nilikuwa napata maumivu ya ovyo Sana side zote nikawa nawaza hata naumwa figo
Toka nilivobeba mimba hadi Leo yaani sijawai tena
Najua unasema hutaki mtoto
Ila nakuambia mtoto ni mtamu kuliko kitu chochote huwezi amini
Yes ni gharama Sana kulea ila ni baraka mno
Pls pls
 
Fanya uzae.kweli ukizaa shida hyo inaisha
Kabla sijazaa nilikuwa napata maumivu ya ovyo Sana side zote nikawa nawaza hata naumwa figo
Toka nilivobeba mimba hadi Leo yaani sijawai tena
Najua unasema hutaki mtoto
Ila nakuambia mtoto ni mtamu kuliko kitu chochote huwezi amini
Yes ni gharama Sana kulea ila ni baraka mno
Pls pls
Inaeza isha halafu nije nijipate nikilia kumliko huyo mtoto, yoo
 
Pole Sana

Inaonekana unatamani kupata mimba Ila umekosa na sasa upo depressed .

Kwahiyo unaona bora njia ya pili ndo itakufaa .

Ebu nenda hosptali kubwa uonane na wataalamu wa AFYA kwanza.
 
Mitishamba walisema nisijaribu nitaua figo
Katika vitu ambavyo modern medicine/ Big Pharma inajitahidi sana na kutumia billions of money ni kutuaminisha kuwa dawa zao za viwandani ndio bora kuliko. Do your research utakuja kukubaliana nami kuwa nature heals. The body knows how to heal itself ila hatuupi muda wa kufanya hivyo. Na sisemi usitumie dawa za hospital na nini, ila fahamu tu kuwa ipo mitishamba tena hapa hapa Tanzania inayoweza kukusaidia pakubwa. All the best OP, nakuombea upate suluhu muafaka kwa hali yako 🙏
 
Back
Top Bottom