Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #21
Unasema hivyo kwa kuwa hayajakukuta .lakini siku yakikukuta utajutia maneno yako haya yaliyokosa utu ,huruma ,upendo kwa wenzetu na ubinadamu.Upuuzi mtupu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unasema hivyo kwa kuwa hayajakukuta .lakini siku yakikukuta utajutia maneno yako haya yaliyokosa utu ,huruma ,upendo kwa wenzetu na ubinadamu.Upuuzi mtupu.
Wewe wasema hivyo kwa kuwa hayajakufika .lakini siku maradhi yakikufika utalaani sana siku ulipoyatoa maneno haya. Utaomba huruma ya Mungu wakati wote ili ufikiwe na mkono wake kupitia madaktari bingwa. Utajikuta moyo wako sasa unaanza kuwa na huruma na kuwaonea huruma wapitiapo katika hali za magonjwa.Upuz mtupu
Ova
Uwe na heshima mdogo wangu.CCM nyie ni wajinga sn
We endelea kusifia wewe ndiyo hayajakukutaWewe wasema hivyo kwa kuwa hayajakufika .lakini siku maradhi yakikufika utalaani sana siku ulipoyatoa maneno haya. Utaomba huruma ya Mungu wakati wote ili ufikiwe na mkono wake kupitia madaktari bingwa. Utajikuta moyo wako sasa unaanza kuwa na huruma na kuwaonea huruma wapitiapo katika hali za magonjwa.
Vipi mmeshatoka kwenye semina?Uwe na heshima mdogo wangu.
Sasa Kama yamekukuta kwanini uwe na roho mbaya kiasi hicho na kukosa huruma kwa watu?We endelea kusifia wewe ndiyo hayajakukuta
Ova
Si nilikwambia upunguze moshi kichwani mwako dogo langu..Vipi mmeshatoka kwenye semina?
Poa semina njema mkuuSi nilikwambia upunguze moshi kichwani mwako dogo langu..
Ukikua na kukomaa akili utaacha kuandika utoto wako hapa jukwaani.Poa semina njema mkuu
ephenNani kama Lucass
Daah !Luca ass
Kwani ephen anasemaje😅😅😊😊Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan alikuja na mpango kabambe na uliokonga na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania wa kuwapatia tabasamu, furaha, kicheko na matumaini wagonjwa mbalimbali walioko mikoani .kwa kuwasogezea huduma ya Madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali karibu yao kabisa au karibu na majumbani kwao.
Hii maana yake nini? Maana yake ni kuwa mgonjwa aliyetakiwa kuuza kuku, ng'ombe, mbuzi, uwanja, mahindi ya chakula, nguruwe ili apate pesa ya nauli na matibabu kwenda Dar es salaam kuonana na madaktari bingwa sasa aliweza kusogezewa huduma ya kuonana na madaktari bingwa Kilometa chache tu kutoka nyumbani kwake pasipo gharama kubwa ya usafiri na matibabu.
Kuna wagonjwa walikuwa wamejikatia tamaa na kujilalia majumbani mwao na kusubiri tu huruma ya Mungu baada ya kuwa hawana uwezo wa kusafiri hadi muhimbili kupata huduma za kibingwa, lakini sasa chini ya mpango huu wa Dkt Samia wa kupeleka madaktari Bingwa mikoani wanakoweka kambi ya siku kadhaa kwa ajili ya kuonana na kutibu wagonjwa.umeweza kuponya wengi,kuwapa tabasamu na matumaini ya maisha watu wengi sana.
Kuna watu nimeshuhudia wakibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kufanyiwa upasuaji wa Uvimbe ndani ya miili yao walioteseka nao kwa maumivu na uchungu mkubwa sana kwa muda mrefu, kutokana na umaskini wa kushindwa kusafiri hadi muhimbili kupata matibabu. Lakini leo kwa upendo wa mama, huruma za mama yetu kipenzi Mheshimiwa Mama Samia wameweza kufikiwa huko huko waliko na kupewa matibabu mazuri na kupona matatizo yao.
Madaktari Bingwa hawa wa mama wamesaidia kuokoa maisha ya watu,kuondoa maumivu na machungu ya watu,kuokoa mali za watu ambazo zingeuzwa kwa hasara kwa ajili ya kugharamia matibabu, pamoja na wakati mwingine kupoteza kabisa maisha kwa kukosa tiba sahihi kutokana na wengine kuamua kuanza kutumia mitishamba kwa wingi huku ugonjwa ukiendelea kukua na kukomaa na kuwa mkubwa na sugu.
Kwa huruma na upendo wa Rais Samia kwa watanzania wanyonge ameweza kufikisha mkono wake wa upendo kwa wagonjwa waliopo majumbani na kuwafuta machozi ya maumivu na kuwapatia tabasamu na matumaini ya kuendelea na maisha mapya yenye afya njema na nzuri kwa ajili ya ujenzi wa Taifa letu.
Nani kama Mama? Nani kama Rais Samia?
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
No!Jitahidi kuvumilia katika kutofautiana mitizamo. Utaishi kwa raha.Inaweza ikawa siyo sana,ila ni raha muheshimiwa.Kuna mijitu inakera hadi unatamani kama unafuga jibwa kali jitu hilo lipite karibu na nyumbani kwako ulisukumizie huko mbwa walifanye kitoweo,eti madaktari wa mama!
Umeambiwa huyo mama yako kawatoa nyumbani kwake!