Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #41
Anaendelea kuchagua mishono ya nguo mbalimbali kuvaa tunapokwenda ikulu naye😃😃Kwani ephen anasemaje😅😅😊😊
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaendelea kuchagua mishono ya nguo mbalimbali kuvaa tunapokwenda ikulu naye😃😃Kwani ephen anasemaje😅😅😊😊
Amani ya Bwana iwe pamoja nawe.Kuna mijitu inakera hadi unatamani kama unafuga jibwa kali jitu hilo lipite karibu na nyumbani kwako ulisukumizie huko mbwa walifanye kitoweo,eti madaktari wa mama!
Umeambiwa huyo mama yako kawatoa nyumbani kwake!
Mimi nimeshuhudia laivu watu wakibubujikwa na machozi ya furaha hadharani, baada ya kupata matibabu kutokana na magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua kwa muda mrefu.Hivi,wewe Luca,huwa unaona kububujikwa na machozi ni rahisi kiviiiileee?You've got big problems wewe mjamaa.
Sina swali muheshimiwa.😂😂😂Mimi nimeshuhudia laivu watu wakibubujikwa na machozi ya furaha hadharani, baada ya kupata matibabu kutokana na magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua kwa muda mrefu.
Safi sanaaaAnaendelea kuchagua mishono ya nguo mbalimbali kuvaa tunapokwenda ikulu naye😃😃
Unafahamu gharama za kumuandaa mtu mpaka anakuwa daktari bingwa?Yaan ni kama kulikua na Rais mwingine na wa Chama kingine aliongoza kwa miaka 60 akawafukuza madaktari wote bingwa mikoani kawaleta muhimbili sasa kama Mama Samia.
Ndendendeee Mwamba huyo…
Kawabeba madaktari wote kawapeleka mikoani wakakae na wagonjwa.
Hapo Hujui kama unakitukana Chama kijana.
Wengine ni wakuwasamehe bure tu maana unakuta mtu anaingia humu jukwaani akiwa amejaa msongo wa mawazo. Kwa hiyo anakuwa anatafuta pa kutolea mahasira yake. Uzuri wangu ni kuwa watu wa hivyo hawanipi shida zaidi ya kuwaambia tu kuwa "Amani ya Bwana iwe pamoja Nao."No!Jitahidi kuvumilia katika kutofautiana mitizamo. Utaishi kwa raha.Inaweza ikawa siyo sana,ila ni raha muheshimiwa.
Mwehu wewe chawa.😂😂😂Wengine ni wakuwasamehe bure tu maana unakuta mtu anaingia humu jukwaani akiwa amejaa msongo wa mawazo. Kwa hiyo anakuwa anatafuta pa kutolea mahasira yake. Uzuri wangu ni kuwa watu wa hivyo hawanipi shida zaidi ya kuwaambia tu kuwa "Amani ya Bwana iwe pamoja Nao."
Amani ya Bwana iwe pamoja nawe.Mwehu wewe chawa.😂😂😂
Nani asome gazeti Lalo sasaNdugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan alikuja na mpango kabambe na uliokonga na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania wa kuwapatia tabasamu, furaha, kicheko na matumaini wagonjwa mbalimbali walioko mikoani .kwa kuwasogezea huduma ya Madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali karibu yao kabisa au karibu na majumbani kwao.
Hii maana yake nini? Maana yake ni kuwa mgonjwa aliyetakiwa kuuza kuku, ng'ombe, mbuzi, uwanja, mahindi ya chakula, nguruwe ili apate pesa ya nauli na matibabu kwenda Dar es salaam kuonana na madaktari bingwa sasa aliweza kusogezewa huduma ya kuonana na madaktari bingwa Kilometa chache tu kutoka nyumbani kwake pasipo gharama kubwa ya usafiri na matibabu.
Kuna wagonjwa walikuwa wamejikatia tamaa na kujilalia majumbani mwao na kusubiri tu huruma ya Mungu baada ya kuwa hawana uwezo wa kusafiri hadi muhimbili kupata huduma za kibingwa, lakini sasa chini ya mpango huu wa Dkt Samia wa kupeleka madaktari Bingwa mikoani wanakoweka kambi ya siku kadhaa kwa ajili ya kuonana na kutibu wagonjwa.umeweza kuponya wengi,kuwapa tabasamu na matumaini ya maisha watu wengi sana.
Kuna watu nimeshuhudia wakibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kufanyiwa upasuaji wa Uvimbe ndani ya miili yao walioteseka nao kwa maumivu na uchungu mkubwa sana kwa muda mrefu, kutokana na umaskini wa kushindwa kusafiri hadi muhimbili kupata matibabu. Lakini leo kwa upendo wa mama, huruma za mama yetu kipenzi Mheshimiwa Mama Samia wameweza kufikiwa huko huko waliko na kupewa matibabu mazuri na kupona matatizo yao.
Madaktari Bingwa hawa wa mama wamesaidia kuokoa maisha ya watu,kuondoa maumivu na machungu ya watu,kuokoa mali za watu ambazo zingeuzwa kwa hasara kwa ajili ya kugharamia matibabu, pamoja na wakati mwingine kupoteza kabisa maisha kwa kukosa tiba sahihi kutokana na wengine kuamua kuanza kutumia mitishamba kwa wingi huku ugonjwa ukiendelea kukua na kukomaa na kuwa mkubwa na sugu.
Kwa huruma na upendo wa Rais Samia kwa watanzania wanyonge ameweza kufikisha mkono wake wa upendo kwa wagonjwa waliopo majumbani na kuwafuta machozi ya maumivu na kuwapatia tabasamu na matumaini ya kuendelea na maisha mapya yenye afya njema na nzuri kwa ajili ya ujenzi wa Taifa letu.
Nani kama Mama? Nani kama Rais Samia?
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.