Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Pigo kubwa sana kwa wapenda-kula nguruwe, because sasa haitakuwa kuwafuga kwa ajili ya bacon & pork, bali kwa ajili ya mioyo yao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walete halal sasa 😁
Inawezekana kabisa hii ikawa ni mojq ya mbinu ya udini. Ni kweli walikosa mnyama aina nyingine ambae anafanania zaidi na binadamu kama sokwe wakaamue wamtumie nguruwe ambae wanajua fika kuwa ni haramu kwa waislamu. Hii vita ya udini japo haipo waziwazi lakini inaonekana kuendelea chinichini.Sijajua kama hapa Tanzania itakubalika labda Moshi.
--
Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa binadamu nchini Marekani
View attachment 2077557
Katika picha hii iliyotolewa na Chuo cha kikuu cha Tiba cha Maryland, timu ya upasuaji inaonyesha moyo wa nguruwe tayari kupandikizwa kwenye mgonjwa
Kwa mara ya kwanza duniani, nchini Marekani, Madaktari wa upasuaji wamefanikiwa kupandikiza moyo kutoka kwa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba hadi kwa binadamu mgonjwa, Chuo Kikuu cha tiba ya Maryland kimesema.
Operesheni hiyo ilitekelezwa siku ya Ijumaa. Ilionyesha, kwa mara ya kwanza, kwamba moyo wa mnyama unaweza kuendelea kufanya kazi kwa binadamu bila usumbufu wowote, Chuo Kikuu cha Maryland kimeongeza.
David Bennett, 57, ambaye alipokea moyo wa nguruwe, alitangazwa kuwa hastahili kupokea upandikizaji wa moyo wa binadamu. Sasa anafuatiliwa kwa karibu na madaktari ili kuhakikisha kiungo kipya kinafanya kazi vizuri.
"Yaani yalikuwa mambo mawili kwa binadamu huyo, ima kifo au upandikizaji wa moyo wa nguruwe. Nataka kuishi.
Ninajua ilinigusa sana, lakini ilikuwa chaguo langu la mwisho, "mkazi wa Maryland alisema siku moja kabla ya upasuaji wake, kulingana na chuo kikuu cha matibabu. "Siwezi kungoja niweze kuamka kitandani mara tu ninapokuwa mzima," David Bennett, ambaye amelala kitandani kwa miezi michache iliyopita na kutumia mashine inayomfanya aendelee kuishi.
Nguruwe aliyebadilishwa vinasaba
Mamlaka ya Madawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha operesheni hiyo jioni ya siku ya kuamkia Mwaka Mpya. "Haya ni mafanikio makubwa ya upasuaji na ambayo yanatuwezesha kupata suluhisho dhidi ya uhaba wa viungo, " amebaini Bartley Griffith, aliyefanyiwa upandikizaji wa moyo wa nguruwe.
Nguruwe ambao moyo hutoka umebadilishwa vinasaba ili kutozalisha tena aina ya sukari ambayo kwa kawaida iko kwenye seli zote za nguruwe na ambayo husababisha kiungo kukataa kufanya kazi mara moja. Marekebisho haya ya jeni yalifanywa na kampuni ya Revivicor, ambayo pia ilitoa figo ya nguruwe ambalo madaktari wa upasuaji walifanikiwa kuunganisha kwa mishipa ya damu ya mgonjwa aliyekuwa mahututi huko New York mwezi Oktoba.
Takriban Wamarekani 110,000 kwa sasa wako kwenye orodha ya wanaosubiri kupandikizwa viungo na zaidi ya watu 6,000 wanaohitaji upandikizaji hufa kila mwaka nchini humo.
Inawezekana kabisa hii ikawa ni mojq ya mbinu ya udini. Ni kweli walikosa mnyama aina nyingine ambae anafanania zaidi na binadamu kama sokwe wakaamue wamtumie nguruwe ambae wanajua fika kuwa ni haramu kwa waislamu. Hii vita ya udini japo haipo waziwazi lakini inaonekana kuendelea chinichini.
Ni kweli!
[emoji134][emoji134][emoji119][emoji119]Aisee,tujiandae kuwekewa kizazi chake na matokeo yake
Mkuu, umenisoma uzuri hapo juu?Inawezekana kabisa hii ikawa ni mojq ya mbinu ya udini. Ni kweli walikosa mnyama aina nyingine ambae anafanania zaidi na binadamu kama sokwe wakaamue wamtumie nguruwe ambae wanajua fika kuwa ni haramu kwa waislamu. Hii vita ya udini japo haipo waziwazi lakini inaonekana kuendelea chinichini.
Moyo unatolewa yanayobaki yanaliwa🤣🤣Pigo kubwa sana kwa wapenda-kula nguruwe, because sasa haitakuwa kuwafuga kwa ajili ya bacon & pork, bali kwa ajili ya mioyo yao.
Sasa hiyo si sawa na kumla mwanadamu, au?Moyo unatolewa yanayobaki yanaliwa🤣🤣
Hapo kwenye chanjo ya tetanus umetu piga changa la macho hakuna TT ya nguruwe broHivi nguruwe ana nini lakini? Chanjo ya corona nguruwe, chanjo ya tetenasi nguruwe, insulin nguruwe. Kwanini hawatengenezi kwa ngombe?
Nguruwe hakutengenezwa maabara Bali amekuzwa chini ya uangalizi na wameondoa gene za kufanya asiweze kuzalisha antibodies za zitakazo sababisha organ rejection full stop! Yeye bado ni kitimoto halisi hakuna ku adjust storyHiyo ni kama medical trial na aliepandikizwa huyo moyo ni mgonjwa tayari wa moyo na anaweza kufa siku yoyote.
Pili, kabla hao madaktari hawajafanya huo upasuaji na kupandikiza huo moyo wa nguruwe waliomba kibali maalum kutoka serikalini na waliporuhusiwa ndo wamefanya hivyo.
Tatu, huyo nguruwe si nguruwe hawa tulozoea wa kuliwa kitimoto bali alipandikiwa maabara kwa ajili ya kujaribiwa katika upandikizaji yaani "genetically modified pig" hivyo si nguruwe wa kawaida.
Hivyo huyo mgonjwa baada ya kushindwa kumpata donor ambae yupo "healthy" ili kumsaidia kuendelea kuishi akaamua kukubali hiyo "experiment" ambayo ameambiwa haina uhakika wa kudumu yaani "guarantee".
Hitaji la viungo vya kupandikiza kama moyo ni kubwa sana nchini Marekani na mwaka jana pekee watu 3,800 walifanyiwa upasuaji wa moyo, na hiyo ni taarifa kutoka United network for Organ Sharing ambayo ni sehemu ya mfumo unosimamia upandikizaji wa viungo kwa mtu yoyote nchini Marekani.
Daktari bingwa wa upasuaji na mtaalam wa magonjwa ya moyo alofanya upasuaji kwa mgonjwa mzee David Bennett anaitwa Dr Muhammad Mohiuddin.
Dr Mohiuddin ndie alisimamia zoezi la kumtengeza nguruwe wa maabara na pia ni mtaalam wa upandikizaji wa viungo kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yaani "animal-to-human transplant".
hahaaHapo kwenye chanjo ya tetanus umetu piga changa la macho hakuna TT ya nguruwe bro
🤣🤣🤣 Ina maana nguruwe ndo our closest ancestor na siyo chimpanzeeSasa hiyo si sawa na kumla mwanadamu, au?
Story hajawa adjsuted, nguruwe kabadilishwa dna maabara kawa kivingine hilo ndilo la msingi.Nguruwe hakutengenezwa maabara Bali amekuzwa chini ya uangalizi na wameondoa gene za kufanya asiweze kuzalisha antibodies za zitakazo sababisha organ rejection full stop! Yeye bado ni kitimoto halisi hakuna ku adjust story