Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Huyu mdudu maisha yake yanazidi kuwa hatarini...Rafiki yangu Kitimoto anazidi kutoa misaada kwa binadamu ambayo sasa ni multipurpose😁😁😁
View attachment 2077394
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu mdudu maisha yake yanazidi kuwa hatarini...Rafiki yangu Kitimoto anazidi kutoa misaada kwa binadamu ambayo sasa ni multipurpose😁😁😁
View attachment 2077394
Wanafahamu atakufa kwani hakuwa ame-qualify kupata moyo mwingine wa binadamu, na wakaona anafaa kufanyiwa majaribio.Huyo bin adam atakufa tu wala huo moyo hautaleta matokeo kwake
Si kweli.Moyo unatolewa yanayobaki yanaliwa🤣🤣
Ngoja tuone matokeo ya kisayansi vs MuumbaWanafahamu atakufa kwani hakuwa ame-qualify kupata moyo mwingine wa binadamu, na wakaona anafaa kufanyiwa majaribio.
Hata hivyo huyu mgonjwa aliwahi kutumikia kifungo jela kwa kumchoma kisu mwanamme mwingine ambae alimhisi alikuwa na mahusiano na mkewe.
Hivyo alitumikia kifungo cha miaka 10 jela na alipotoka akawa na hilo tatizo.
Hili suala la kutumia mioyo ya wanyama limekuwa likifanyika nchini Marekani kwa siri.
Mwaka 1980 madaktari walipandikiza moyo wa sokwe kwa mtoto inasemwa ni (mtoto mwenye asili ya Afrika) aliezaliwa na moyo wenye tundu (congenital heart defect) na akafariki baada ya mwezi kutokana na mfumo wake wa kinga kukataa moyo huo wa sokwe.
Baada ya hiyo failure ndo wakaendelea na kumshughulikia zaidi nguruwe ili kupata moyo ambayo wafaa zaidi.
Ofcourse hata huo moyo umeeditiwa genes. Hapa tunaleta utani tuSi kweli.
Hawa nguruwe waitwa "GalSafe Pigs" hutayarishwa na kampuni moja yaitwa Revivicor ni regenerative medicine company.
Hii kampuni kazi yake ni kuwandaa hawa nguruwe na kisha kupata kibali kutoka FDAS ili watumiwe kwenye "Pharmacology".
Hivyo si nguruwe wa kawaida kiasi cha kumkarangiza na kumla.
Unajua tofauti ya antigen na DNA?Story hajawa adjsuted, nguruwe kabadilishwa dna maabara kawa kivingine hilo ndilo la msingi.
Yaani kafanyiwa matengenezo na si kuundwa. Nimetumia neno kapandikizwa nikimaanisha kabadilishwa, hivyo huyo hawezi kuwa nguruwe wa kawaida tena. Ndo maana wao wasema "genetic modified pig."
Hata ukimtumia kutaka piglets hutapata walo wazima kwa kila kinasaba.
Weye nguruwe huyo waweza kumla wakisema wanamrudisha mezani kutokea maabara?
Ndo maana wadau wa haki za wanyama welfare activits wanapinga masuala hayo ya "animal testing and modifications".
Sijajua kama hapa Tanzania itakubalika labda Moshi.
--
Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa binadamu nchini Marekani
View attachment 2077557
Katika picha hii iliyotolewa na Chuo cha kikuu cha Tiba cha Maryland, timu ya upasuaji inaonyesha moyo wa nguruwe tayari kupandikizwa kwenye mgonjwa
Kwa mara ya kwanza duniani, nchini Marekani, Madaktari wa upasuaji wamefanikiwa kupandikiza moyo kutoka kwa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba hadi kwa binadamu mgonjwa, Chuo Kikuu cha tiba ya Maryland kimesema.
Operesheni hiyo ilitekelezwa siku ya Ijumaa. Ilionyesha, kwa mara ya kwanza, kwamba moyo wa mnyama unaweza kuendelea kufanya kazi kwa binadamu bila usumbufu wowote, Chuo Kikuu cha Maryland kimeongeza.
David Bennett, 57, ambaye alipokea moyo wa nguruwe, alitangazwa kuwa hastahili kupokea upandikizaji wa moyo wa binadamu. Sasa anafuatiliwa kwa karibu na madaktari ili kuhakikisha kiungo kipya kinafanya kazi vizuri.
"Yaani yalikuwa mambo mawili kwa binadamu huyo, ima kifo au upandikizaji wa moyo wa nguruwe. Nataka kuishi.
Ninajua ilinigusa sana, lakini ilikuwa chaguo langu la mwisho, "mkazi wa Maryland alisema siku moja kabla ya upasuaji wake, kulingana na chuo kikuu cha matibabu. "Siwezi kungoja niweze kuamka kitandani mara tu ninapokuwa mzima," David Bennett, ambaye amelala kitandani kwa miezi michache iliyopita na kutumia mashine inayomfanya aendelee kuishi.
Nguruwe aliyebadilishwa vinasaba
Mamlaka ya Madawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha operesheni hiyo jioni ya siku ya kuamkia Mwaka Mpya. "Haya ni mafanikio makubwa ya upasuaji na ambayo yanatuwezesha kupata suluhisho dhidi ya uhaba wa viungo, " amebaini Bartley Griffith, aliyefanyiwa upandikizaji wa moyo wa nguruwe.
Nguruwe ambao moyo hutoka umebadilishwa vinasaba ili kutozalisha tena aina ya sukari ambayo kwa kawaida iko kwenye seli zote za nguruwe na ambayo husababisha kiungo kukataa kufanya kazi mara moja. Marekebisho haya ya jeni yalifanywa na kampuni ya Revivicor, ambayo pia ilitoa figo ya nguruwe ambalo madaktari wa upasuaji walifanikiwa kuunganisha kwa mishipa ya damu ya mgonjwa aliyekuwa mahututi huko New York mwezi Oktoba.
Takriban Wamarekani 110,000 kwa sasa wako kwenye orodha ya wanaosubiri kupandikizwa viungo na zaidi ya watu 6,000 wanaohitaji upandikizaji hufa kila mwaka nchini humo.
Walete halal sasa [emoji16]
NdioUnajua tofauti ya antigen na DNA?
Cd. 4 za kumwaga...Rafiki yangu Kitimoto anazidi kutoa misaada kwa binadamu ambayo sasa ni multipurpose[emoji16][emoji16][emoji16]
View attachment 2077394
Umesahau damuHivi nguruwe ana nini lakini? Chanjo ya corona nguruwe, chanjo ya tetenasi nguruwe, insulin nguruwe. Kwanini hawatengenezi kwa ngombe?
Hahaaahaaaa nimecheka sana mpaka simu yangu imeporomoka,,akila kitumoto kamla ndugu yake teteeeeheteeee jf ukiwa na mawazo yanakuzongo we log in jf mambo yanakua poaSwali la msingi ni umri wa nguruwe kuishi..
Nguruwe anaishi miaka minne maximum..
Je moyo wake utaendelea kuishi baada ya hapo?
Ila huyu mtu hatakiwi kula nyama ya nguruwe, wameshakuwa ndugu