Madaktari bingwa wafanikiwa kumpandikiza binadamu moyo wa nguruwe

Pigo kubwa sana kwa wapenda-kula nguruwe, because sasa haitakuwa kuwafuga kwa ajili ya bacon & pork, bali kwa ajili ya mioyo yao.
 
Inawezekana kabisa hii ikawa ni mojq ya mbinu ya udini. Ni kweli walikosa mnyama aina nyingine ambae anafanania zaidi na binadamu kama sokwe wakaamue wamtumie nguruwe ambae wanajua fika kuwa ni haramu kwa waislamu. Hii vita ya udini japo haipo waziwazi lakini inaonekana kuendelea chinichini.
 

Hapana hakuna vita yeyote bali ni elimu tu na uvumbuzi
Uislam umeweka wazi kila kitu na suala la kuuliza na kujisomea tu

Zipo dawa ambazo hatuweza kutumia ila wengine wanatumia

Kuhusu hili jaribio hawakukurupuka tu bali ni la mda mrefu sana na Islamic council waliliongelea sana na tunajua ni Haram

Kwa hiyo acha wafanye majaribio yao na sisi kama kwetu haitufai tunaacha
 
Mkuu, umenisoma uzuri hapo juu?
 
Mwanaume wa marekani amekuwa mtu wa kwanza kabisa duniani kupata moyo wa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba(GMO).

David Bennett, mweNYE umri wa miaka 57, anaendelea vyema siku tatu baada ya upasuaji wa majaribio hayo uliofanyika katika mji wa Baltimore, wanasema madaktari.

Upandikizaji wa moyo huo unachukuliwa kama matumaini ya kuyaokoa maisha a Bw Bennett, ingawa haijawa wazi bado ni fursa ya kiasi gani aliyo nayo ya kuishi maisha marefu.

" Ulikuwa ni upandikizaji wa kufanya au afe," Bw Bennett alielezea siku moja kabla ya upasuaji.

''Ninafahamu kwamba ni jambo la kubahatisha, lakini ni chaguo langu la mwisho," alisema.

Madaktari wa Chuo Kikuu cha Maryland kito cha tiba walipewa idhini maalum na wasimamizi wa matibabu kuendelea na upasuaji huo, kwa misingi kwamba vinginevyo Bw Bennet angekufa.

Alikuwa ameonekana kwamba hakuwa na uwezo wa kupandikiziwa moyo wa binadamu, uamuazi ambao mara nyingi huchukuliwa na madaktari wakati mgonjwa anapokuwa na afya duni sana.

Kwa timu ya madaktari iliyofanya upandikizaji huo, mafanikio hayo yamehitimisha miaka kadhaa ya utrafiri na yanaweza kubadili maisha kote duniani.

Daktari wa upasuaji Bartley Griffith alisema upasuaji utaileta dunia katika "hatua moja ya kukaribia kutatua mzozo wa ukosefu wa kiungo cha mwili ",Chuo kikuu cha tiba cha Maryland kilisema katika taarifa yake kwa umma.

Kwamba mzozo huo unamaanisha kuwa watu 17 kwa siku hufariki nchini Marekani wakati wakisubiri kufanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa viungo, huku zaidi ya 100,000 wakiripotiwa kungojea upasuaji.

Uwezekano wa kutumia viungo vya Wanyama kwa ajili ya kile kinachoitwa xenotransplantation ili kufikia mahitaji umekuwa ukifikiriwa kwa muda mrefu, na matumizi ya mishipa ya moyo wa nguruwe tayari limekuwa ni jambo la kawaida.

Mwezi Oktoba, 2021, madaktari wa upasuaji mjini New York walitangaza kwamba wamefanikiwa kupandikiza figo la nguruwe kwa binadamu.

Wakati huo, upasuaji huo ulikuwa ni jaribio la teknolojia ya hali ya juu zaidi kuwahi kufikiwa.

Hatahivyo, ubongo wa mtu alyepandikiziwa ulikufa na hakuna matumaini ya kupona.

Bw Bennett, hatahivyo , anamatumaini kuwa upandikizaji wake wa moyo wa nguruwe utamuwezesha kuendelea na maisha yake.

Alikuwa amelala kitandani kwa wiki sita mfulurizo kabla ya kufanyiwa upasuaji, na aliwekewa mashine ambayo ilimuwezesha kuendelea kuishi baada ya kupatikana na maradhi yanayoua ya moyo.

"Natazamia kunyenyuka na kuondoka kitandani baada ya kupona ," alisema wiki iliyopita.

Jumatatu, Bw Bennett aliripotiwa kupumua mwenyewe huku akiendelea kufuatiliwa kwa karibu.

Lakini kile kitakachotokea baadaye hakijawa wazi. Nguruwe aliyetumiwa katika upandikizaji alifanyiwa mabadiliko ya vinasaba ili kuondoa jeni kadhaa ambazo zingefanya kiungo hicho kikataliwe na mwili wa Bw Bennet, linaripoti shirika la habari la AFP.

Bw Griffith anasema wanaendelea kumfuatilia kwa makini na kwa uangalifu mkubwa, huku mwanae wa kiume David Bennett Jr akiliambia Shirika la Habari la ovAssociated Press kwamba familia yao iko "katika hali ya sintofamu wakati huu".

Lakini aliongeza : "Alitambua ukubwa wa kile kilichofanyika na anatambua umuhimu wake."

''Hatujawahi kufanya hili kwa binadamu na ninapenda kufikiria kwamba tumempatia chaguo bora kuliko kile ambacho kingetokea kama angeendelea kupewa matibabu aliyokuwa akiyapata," alisema Bw Griffith . Lakini iwapo [ataishi kwa] siku, wiki , mwezi, au mwaka, sijui."
 
Huyo bin adam atakufa tu wala huo moyo hautaleta matokeo kwake
 
Hivi nguruwe ana nini lakini? Chanjo ya corona nguruwe, chanjo ya tetenasi nguruwe, insulin nguruwe. Kwanini hawatengenezi kwa ngombe?
Hapo kwenye chanjo ya tetanus umetu piga changa la macho hakuna TT ya nguruwe bro
 
Nguruwe hakutengenezwa maabara Bali amekuzwa chini ya uangalizi na wameondoa gene za kufanya asiweze kuzalisha antibodies za zitakazo sababisha organ rejection full stop! Yeye bado ni kitimoto halisi hakuna ku adjust story
 
Nguruwe hakutengenezwa maabara Bali amekuzwa chini ya uangalizi na wameondoa gene za kufanya asiweze kuzalisha antibodies za zitakazo sababisha organ rejection full stop! Yeye bado ni kitimoto halisi hakuna ku adjust story
Story hajawa adjsuted, nguruwe kabadilishwa dna maabara kawa kivingine hilo ndilo la msingi.

Yaani kafanyiwa matengenezo na si kuundwa. Nimetumia neno kapandikizwa nikimaanisha kabadilishwa, hivyo huyo hawezi kuwa nguruwe wa kawaida tena. Ndo maana wao wasema "genetic modified pig."

Hata ukimtumia kutaka piglets hutapata walo wazima kwa kila kinasaba.

Weye nguruwe huyo waweza kumla wakisema wanamrudisha mezani kutokea maabara?

Ndo maana wadau wa haki za wanyama welfare activits wanapinga masuala hayo ya "animal testing and modifications".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…