Madaktari hasa wa Tanzania rudini maabara tena kuhusu ugonjwa wa U.T.I

Madaktari hasa wa Tanzania rudini maabara tena kuhusu ugonjwa wa U.T.I

nilichohoji kwenye hizo 24 hrs za BS ,ni lazima ifanye baada ya 24 hrs after preparation ya sample baada ya mdau kuwa na shaka na kipimo cha malaria kwa 30 min
Hyo mrdt kwa 30min tayar ishasoma majibu na tena chini ya hapo kuanzia 5min

Kama anakuwa na shaka anafanya BS tu haina shida Ni muda mfupi tu mana kila kitu kinafanyika within 15 minutes kwa BS teyar kama Kuna vifaa vya uhakika
 
Acha kudaganya watu wewe..culture ya Malaria,????? Maralia parasite au Malaria gani unaowazungumzia wewe??
 
Mfumo wa Afya na elimu za wagonjwa na kujali kwao ndo kumesababisha UTI kuongezeka.
Nyingi zinatengenezwa na
1. Tabia ya kujisafisha na kuingiliana njia mbili( hizi huwa za kweli)
2. Biashara
3. Uduni wa upimaji katika hospitali zetu (Diagnoatic profile).
4. Tabia ya watu kupenda kuambiwa wanaumwa wakati hawaumwi
5. Kutopenda kujifunza.

Tatu kati ya hizi unaweza epukana navyo.
Daktari akikwambia una UTI muulize dalili zake.
Dalili za UTI ziko wazi kwenye mtandao, usipopata maumivu wakati wa kukojoa au kukojoa mara kwa mara au kujihisi mkojo unabaki wakati wa kukojoa basi huna UTI.

Hauna sababu ya kunywa dawa ya UTI kama huna hizo dalili.

Mengine ya mfumo hayatabadilika kirahisi maana bado hata hospitali zetu za serikali ndio vipimo vinavyopatikana.
 
Ukitaka ugombane na mgonjwa mwambie haumwi chochote hapo atahamaki huyo balaaa
 
Ukiona mwanaume ana UTI jua kuna moja kati ya haya

1.Kapata kwa demu wake kupitia uke
2.Anafanya mapenzi kinyume na maumbile maana bakteria mkuu anaye sababisha yupo hayo maeneo hayo

Turudi kwa mtoa mada
UTI ni kweli tatizo ni uchafu ila usielewe vibaya kuwa kuoga kila wakati,wanawake wanapata sana UTI kwa sababu hizi hapa
1.Kunawa kutoka nyuma(kinyeo) kwenda mbele(ukeni) hasa baada ya kukata kimba hivyo unakua una wabeba wale wadudu kutoka walipotakiwa kuwa na kuwapeleka pasipotakiwa.
2.Kutokumaliza dozi hasa kwa wale ambao walishawahi kuumwa
3.Kupata kutoka kwa mwenza wake kama na yeye ana maambukizi
4.matumizi ya pedi kwa muda mrefu bila kubadilisha mara kwa mara.
5.Matumizi ya sabuni kali ambazo zina pelekea kuua Normal flora wa uke na kuruhusu mdudu huyo kuingia kirahisi

Cha kufanya
1.safisha maeneo yako ya siri kutoka mbele kwenda nyuma
2.usitumie sabuni kali
3.ukiipata tumia dawa hadi umalize na usifanye ngono mpaka upone pia mwambie na mwenzi wako apime kama kapata atumie dawa
4.badili pedi mara kwa mara
Kingine
Kunywa maji walau lita 1 na nusu kwa siku
Na kutumia vyoo vya umma kwa umakini mkubwa sana
Kama maji yapo flush kabla ya kutumia na usichuchumae hadi chini

Mtu choo kichafu/hukijui unanawa na maji?..
Choo hukijui unakaa kabisa ama unachuchumaa hadi chini mzima mzima?..
UTI itaishaje?.

Last watu mtumie toilet paper and wipe kwenda nyuma ili ubaki mkavu mda wote
 
U.t.i ina sababishwa na mambo mengi sna mkuu , sio tu kua mchafu
Miongoni mwa sababu ni hizi zifuatazo

1. Kutumia chemical kupaka sehem za siri kama vile (baadhi ya powder )

2.kutopenda kunywa maji ya kutosha ( kunywa maji mara kwa mara ( hii hupelekea bacteria ambao wanaweza kuingia huku
kwa njia moja ama nyengine wasiwe flushed out , pia hupelekea mkojo kua very concentrated ( kuwemo na crystals ,na elements zengine nying ktk mkojo )

3. Kutokua na kawaida ya kujisafisha kwa kina dada punde tu baada ya sex na kua na utamaduni wa kulazishia kwa sisi wanaume

4. Kwa kina dada kua na kawaida ya kujisafisha kwa maji kutoka nyuma kuja mbele baaada ya haja kubwa hivyo wanamchukua bacteria ambae anaitwa Escherichia coli kutoka kwenye kinyesi kumleta kwenye uke na kutokana na wadada distance ya urethra zao na blader ni ndogo basi ndo maana wanaugua U.T.I mara kwa mara ukilinganisha na sisi wanaume kwani distance ya urethra zetu ni kubwa hadi kufikia urinary blader

5.kupendelea vinywaji vya chemical ambavyo vinaweza ku distarb kidney nephron ( glomerula) hivyo large molecules kama leucocytes , protein na blood( RBC ) kuweza kupenye had kuweza kuonekana ktk mkojo wanaojua wanajua kwamba upatikanaj wa protein ktk urine pia ni U.T.I

Nimezungumza hayo kwanza ili niende hasa directly kwenye sabbu ya kwanini kila sku ukienda hosp unaambiwa una u.t.i husan kwenye hospital za private kwa wakina dada

1. Poor test used to diagnose u.t.i ( kiilivyo ili kuthibitisha kama mtu anaugua real U.T.I lazima ufanye culture ( uoteshaji wa bacteria ) ukimaliza unafanya na sensitive test ( je ikiwa ipo u.t.i ni dawa gani itamtibu muhusika )

Sasa hospital zetu hakuna huo utaratibu watu wanapiga chemical na microscopical habar imeisha ndo maaana mara nying mda mwengin watu wanabandikwa u.t.i ambazo sio za ukwel

Mfano : mtu unamkuta na cells za epithilial ambazo ni moderate tu unamwambia ana u.t.i mtu huyo huyo pengine ka sex 3 hours ago

Tunajua epithilial ni cells ni cells zinazojenga kuta laini sasa kama mtu kapata msuguano wa sex kwann zisionekane hapo utakuta anapigwa powercef mtu huyu

2. Utumiaji wa antibiotic kiholela , wote tunajua antibiotic sio dawa za kutumia kama pipi hasa hasa strong antibiotic

Ila sasa watu wamefanya fashian akienda na ki u.t.i uchwara anapigwa powercef inafiga mda mtu anafanya DRUG RESISTANCE hivyo hata akiigua u.t.i ya ukwel na kupewa dawa za antibiotic bas dawa hizo hazimtibu u.t.i bali anaendelea kuwa na u.t.i yake na kwa vile hatuna utaratibu wa re - testing soon after treatment basi mtu anaamin u.t.i imepona kumbe bado ipo sema inasubir Immunity ikishuka tu inajitokeza

3.Bussiness reason: sababu ya mwisho ni ya kibiashara zaid hasa kwenye ma hospital ya private kuna madawa ya gharama(antibiotic ) sna kama vile augumentin , amoxyclave etc mtu hawezi kuacha hizi dawa zi expire katika phamancy hivyo hapo ni mwendo wa kuzitoa kwa njia yyte ile

Ndo pale nilipoongea hapo juu kwamba ukikutwa na moderate tu epithilial cells , hutoambiwa unywe maji ya kutosha badala yake utapigwa augumentin

Hizo ndo sababu nilizooona kwa expirience yngu
Wewe Jamaa umetoa maelezo mazuri sana ila umetupiga kamba hasa tena amabao hawajui ndio umewapiga kamba ya kiwango Cha SGR!! Hivi Tangu lini epithelial cells ndio Tunasema ni UTI wakati hizo Mara nyingi tena kwa wadada n common na normal tu labda yawe mengi sana!! Kwa wanaume ni Mara chache sana kuyaona.. UTI tunaangalia Pus cells tena ziwe zaidi ya 5 kwenda juu tukikuta Pus cells 0-5/HPF huwa ni normal tu...

Maelezo mazuri sana ila umepuyanga sehemu ndogo tu na nimeshakuelezea hapo juu!!
 
Hebu nitolee utapeli hapa,mpigie waziri umpe hiyo elimu siyo mimi.
Sawa boss ila huyo waziri ameleta siasa za wazi hapo kwenye UTI ila kwa Typhoid namuunga mkono ila kwakuwa umekataa shule basi kausha
 
Ndugu yangu ni karibu Mara tatu tofauti..akijiskia vibaya akienda hosputal akirud anatuambia vipimo vinasema ana UTI na Typhoid...
Nae anaamini..anaambiwa typhoid yako ni ile ya juu na ipo kwenye damu ndo maana tofauti na wengine..
Kila akienda kupima majibu ni hayo tu.
Vipi wewe huna u.t.i?
 
Wewe Jamaa umetoa maelezo mazuri sana ila umetupiga kamba hasa tena amabao hawajui ndio umewapiga kamba ya kiwango Cha SGR!! Hivi Tangu lini epithelial cells ndio Tunasema ni UTI wakati hizo Mara nyingi tena kwa wadada n common na normal tu labda yawe mengi sana!! Kwa wanaume ni Mara chache sana kuyaona.. UTI tunaangalia Pus cells tena ziwe zaidi ya 5 kwenda juu tukikuta Pus cells 0-5/HPF huwa ni normal tu...

Maelezo mazuri sana ila umepuyanga sehemu ndogo tu na nimeshakuelezea hapo juu!!
Ukikuta epithelial cell kwenye mkojo hapo hakuna UTI maana hizo ni cell zilizoharibika au kuisha mda wake zimetolewa ukikuta pus cell hapo ndo tunasema mtu ana UTI
 
Sababu ni hii Aggy

Mwili hutoa antibodies unaposhambuliwa na wadudu waletao maradhi sasa kila mdudu wa ugonjwa fulani mwili hutoa hizi antibodies za huo ugonjwa kumbuka kila ugonjwa mwili hutoa antibodies zinazoendana na huo ugonjwa.

Sasa ishu iko hivi mwili unapotoa antibodies wa typhoid na mtu anapoenda kupima damu kupitia kipimo cha widal test ambacho ni common kwa dispensari nyingi kile kipimo kina detect antibodies za typhoid na hapo tunasema una typhoida sasa ishu inakua hata ukitumia dawa na ukapona zile antibodies zina uwezo wa kubaki kwenye damu kwa muda wa miezi 6,sasa ikitokea ukaumwa ugonjwa kidogo ujaenda hospital na ukapima damu kupitia widal test bado kipimo kitasoma una typhoid maana antibodies bado zipo kwenye damu yako hapo ndo mtu huwa kila akienda anaona anaambiwa ana typhoid

Cha kufanya
Ukifika kwa daktari ukimweleza history yako na ukaona amekuandikia kipimo cha typhoid kile cha widal test na kama uliunwa typhoud niezi ya karibuni na ukatumia dawanipasavyo ukapona mwambie daktari kuwa uliumwa hivi karibu kumualert abadili kipimo iwapo kama hukumwambia mapema kuwa uliumw Huo ugonjwa kumbuka daktari ata order upime typhoid kwa sababu dalili za typhoid hufanana sana na malaria
Ndugu yangu ni karibu Mara tatu tofauti..akijiskia vibaya akienda hosputal akirud anatuambia vipimo vinasema ana UTI na Typhoid...
Nae anaamini..anaambiwa typhoid yako ni ile ya juu na ipo kwenye damu ndo maana tofauti na wengine..
Kila akienda kupima majibu ni hayo tu.
 
Ukiona mwanaume ana UTI jua kuna moja kati ya haya

1.Kapata kwa demu wake kupitia uke
2.Anafanya mapenzi kinyume na maumbile maana bakteria mkuu anaye sababisha yupo hayo maeneo hayo

Turudi kwa mtoa mada
UTI ni kweli tatizo ni uchafu ila usielewe vibaya kuwa kuoga kila wakati,wanawake wanapata sana UTI kwa sababu hizi hapa
1.Kunawa kutoka nyuma(kinyeo) kwenda mbele(ukeni) hasa baada ya kukata kimba hivyo unakua una wabeba wale wadudu kutoka walipotakiwa kuwa na kuwapeleka pasipotakiwa.
2.Kutokumaliza dozi hasa kwa wale ambao walishawahi kuumwa
3.Kupata kutoka kwa mwenza wake kama na yeye ana maambukizi
4.matumizi ya pedi kwa muda mrefu bila kubadilisha mara kwa mara.
5.Matumizi ya sabuni kali ambazo zina pelekea kuua Normal flora wa uke na kuruhusu mdudu huyo kuingia kirahisi

Cha kufanya
1.safisha maeneo yako ya siri kutoka mbele kwenda nyuma
2.usitumie sabuni kali
3.ukiipata tumia dawa hadi umalize na usifanye ngono mpaka upone pia mwambie na mwenzi wako apime kama kapata atumie dawa
4.badili pedi mara kwa mara
mkuu unataka kusema njia ya mkojo kwa mwanamke ni sawa na njia ya uzazi.. maana hawa wadudu wanakaa mwanzoni mwa kibofu cha mkojo na kwenye mirija ya mkojo sasa dudu la yuyu linapita sehemu tofauti na ya mkojo linapita kwenye njia ya uzazi hebu tuwekane sawa hapa mwanaume unapataje UTI
 
Wewe Jamaa umetoa maelezo mazuri sana ila umetupiga kamba hasa tena amabao hawajui ndio umewapiga kamba ya kiwango Cha SGR!! Hivi Tangu lini epithelial cells ndio Tunasema ni UTI wakati hizo Mara nyingi tena kwa wadada n common na normal tu labda yawe mengi sana!! Kwa wanaume ni Mara chache sana kuyaona.. UTI tunaangalia Pus cells tena ziwe zaidi ya 5 kwenda juu tukikuta Pus cells 0-5/HPF huwa ni normal tu...

Maelezo mazuri sana ila umepuyanga sehemu ndogo tu na nimeshakuelezea hapo juu!!
Soma vzur mkuu unielewe emu , hakuna sehem nimesema ukiwa na epithilial cells ndo una u.t.i mm nimetoa mfano kwamba hosp ukienda ukionekana una moderate epithilial cells tu unaambiwa una u.t.i na nikapinga kwa mfano kwamba epithilial cells uki sex na ukienda kupima lazima zionekane au kwa mama wajawazito

Unakuja na povu litre 5 hapa
 
mkuu unataka kusema njia ya mkojo kwa mwanamke ni sawa na njia ya uzazi.. maana hawa wadudu wanakaa mwanzoni mwa kibofu cha mkojo na kwenye mirija ya mkojo sasa dudu la yuyu linapita sehemu tofauti na ya mkojo linapita kwenye njia ya uzazi hebu tuwekane sawa hapa mwanaume unapataje UTI
Hapana njia ya mkojo ipo tofauti na ya uzazi...

Mwanaume anapata UTI hasa ilie ya kwanza Urethritis(kwenye njia ya mkojo) kumbuka UTI zipo za aina tatu ambazo kwenye mrija wa uume,kibofu na figo so usikariri kuwa UTI inatokea kwenye kibofu tu hiyo ni stage nyingine pale backteria usipowatibu wanasambaa na wakifika mpaka kwenye figo ni hatari na utajuaje kuwa mtu UTI yake imefika kwenye figo,ukimpiga sehemu ya nyuma ya mgongo ambapo figo zinapatikana husikia maumivu makali
 
Deep stick sometimes usomaji wake unakuwa mgumu kwa mtu kuangalia rang zile

Njia pekee Ni kuotesha tu ( urine calct)
Kufanya culture ni gharama na hospital nyingi hawana uwezo...na mara nyingi culture hufanywa hasa pale panatokea drug resistance
 
1. wote wnye magonjwa ya zinaa wanasema wana UTI.
2.Maabara zinataka ziuze dawa.
3.Kwa wanawake ugonjwa wa fangasi ukeni ni kitu cha kawaida sana lakini mtu atakwambia nina UTI na si fangasi.
4.Utamaduni wetu wa kuchambia maji unatucost sana.
 
Tuchambie nini Boss?
 
Kuna siku nilienda hospitali nikiwa najisikia vibaya,baada ya vipimo nikapewa dawa bila maelezo. Ikabidi nimrudie dk kuwa dawa hizi ni za nini? Naambiwa 'Una typhoid kwa mbali' Sikunywa hizo dawa na hadi leo sijisikii tatizo lolote.

Wapo ambao kweli wanaumwa,lakini hili suala la Typhoid na U.T.I linanipa mashaka sana. Nadhani kuna biashara ndani yake ambayo hawaangalii madhara kwa mtumiaji.
 
Back
Top Bottom