Madaktari hasa wa Tanzania rudini maabara tena kuhusu ugonjwa wa U.T.I

nilichohoji kwenye hizo 24 hrs za BS ,ni lazima ifanye baada ya 24 hrs after preparation ya sample baada ya mdau kuwa na shaka na kipimo cha malaria kwa 30 min
Hyo mrdt kwa 30min tayar ishasoma majibu na tena chini ya hapo kuanzia 5min

Kama anakuwa na shaka anafanya BS tu haina shida Ni muda mfupi tu mana kila kitu kinafanyika within 15 minutes kwa BS teyar kama Kuna vifaa vya uhakika
 
Acha kudaganya watu wewe..culture ya Malaria,????? Maralia parasite au Malaria gani unaowazungumzia wewe??
 
Mfumo wa Afya na elimu za wagonjwa na kujali kwao ndo kumesababisha UTI kuongezeka.
Nyingi zinatengenezwa na
1. Tabia ya kujisafisha na kuingiliana njia mbili( hizi huwa za kweli)
2. Biashara
3. Uduni wa upimaji katika hospitali zetu (Diagnoatic profile).
4. Tabia ya watu kupenda kuambiwa wanaumwa wakati hawaumwi
5. Kutopenda kujifunza.

Tatu kati ya hizi unaweza epukana navyo.
Daktari akikwambia una UTI muulize dalili zake.
Dalili za UTI ziko wazi kwenye mtandao, usipopata maumivu wakati wa kukojoa au kukojoa mara kwa mara au kujihisi mkojo unabaki wakati wa kukojoa basi huna UTI.

Hauna sababu ya kunywa dawa ya UTI kama huna hizo dalili.

Mengine ya mfumo hayatabadilika kirahisi maana bado hata hospitali zetu za serikali ndio vipimo vinavyopatikana.
 
Ukitaka ugombane na mgonjwa mwambie haumwi chochote hapo atahamaki huyo balaaa
 
Kingine
Kunywa maji walau lita 1 na nusu kwa siku
Na kutumia vyoo vya umma kwa umakini mkubwa sana
Kama maji yapo flush kabla ya kutumia na usichuchumae hadi chini

Mtu choo kichafu/hukijui unanawa na maji?..
Choo hukijui unakaa kabisa ama unachuchumaa hadi chini mzima mzima?..
UTI itaishaje?.

Last watu mtumie toilet paper and wipe kwenda nyuma ili ubaki mkavu mda wote
 
Wewe Jamaa umetoa maelezo mazuri sana ila umetupiga kamba hasa tena amabao hawajui ndio umewapiga kamba ya kiwango Cha SGR!! Hivi Tangu lini epithelial cells ndio Tunasema ni UTI wakati hizo Mara nyingi tena kwa wadada n common na normal tu labda yawe mengi sana!! Kwa wanaume ni Mara chache sana kuyaona.. UTI tunaangalia Pus cells tena ziwe zaidi ya 5 kwenda juu tukikuta Pus cells 0-5/HPF huwa ni normal tu...


Maelezo mazuri sana ila umepuyanga sehemu ndogo tu na nimeshakuelezea hapo juu!!
 
Hebu nitolee utapeli hapa,mpigie waziri umpe hiyo elimu siyo mimi.
Sawa boss ila huyo waziri ameleta siasa za wazi hapo kwenye UTI ila kwa Typhoid namuunga mkono ila kwakuwa umekataa shule basi kausha
 
Vipi wewe huna u.t.i?
 
Ukikuta epithelial cell kwenye mkojo hapo hakuna UTI maana hizo ni cell zilizoharibika au kuisha mda wake zimetolewa ukikuta pus cell hapo ndo tunasema mtu ana UTI
 
Sababu ni hii Aggy

Mwili hutoa antibodies unaposhambuliwa na wadudu waletao maradhi sasa kila mdudu wa ugonjwa fulani mwili hutoa hizi antibodies za huo ugonjwa kumbuka kila ugonjwa mwili hutoa antibodies zinazoendana na huo ugonjwa.

Sasa ishu iko hivi mwili unapotoa antibodies wa typhoid na mtu anapoenda kupima damu kupitia kipimo cha widal test ambacho ni common kwa dispensari nyingi kile kipimo kina detect antibodies za typhoid na hapo tunasema una typhoida sasa ishu inakua hata ukitumia dawa na ukapona zile antibodies zina uwezo wa kubaki kwenye damu kwa muda wa miezi 6,sasa ikitokea ukaumwa ugonjwa kidogo ujaenda hospital na ukapima damu kupitia widal test bado kipimo kitasoma una typhoid maana antibodies bado zipo kwenye damu yako hapo ndo mtu huwa kila akienda anaona anaambiwa ana typhoid

Cha kufanya
Ukifika kwa daktari ukimweleza history yako na ukaona amekuandikia kipimo cha typhoid kile cha widal test na kama uliunwa typhoud niezi ya karibuni na ukatumia dawanipasavyo ukapona mwambie daktari kuwa uliumwa hivi karibu kumualert abadili kipimo iwapo kama hukumwambia mapema kuwa uliumw Huo ugonjwa kumbuka daktari ata order upime typhoid kwa sababu dalili za typhoid hufanana sana na malaria
 
mkuu unataka kusema njia ya mkojo kwa mwanamke ni sawa na njia ya uzazi.. maana hawa wadudu wanakaa mwanzoni mwa kibofu cha mkojo na kwenye mirija ya mkojo sasa dudu la yuyu linapita sehemu tofauti na ya mkojo linapita kwenye njia ya uzazi hebu tuwekane sawa hapa mwanaume unapataje UTI
 
Soma vzur mkuu unielewe emu , hakuna sehem nimesema ukiwa na epithilial cells ndo una u.t.i mm nimetoa mfano kwamba hosp ukienda ukionekana una moderate epithilial cells tu unaambiwa una u.t.i na nikapinga kwa mfano kwamba epithilial cells uki sex na ukienda kupima lazima zionekane au kwa mama wajawazito

Unakuja na povu litre 5 hapa
 
Hapana njia ya mkojo ipo tofauti na ya uzazi...

Mwanaume anapata UTI hasa ilie ya kwanza Urethritis(kwenye njia ya mkojo) kumbuka UTI zipo za aina tatu ambazo kwenye mrija wa uume,kibofu na figo so usikariri kuwa UTI inatokea kwenye kibofu tu hiyo ni stage nyingine pale backteria usipowatibu wanasambaa na wakifika mpaka kwenye figo ni hatari na utajuaje kuwa mtu UTI yake imefika kwenye figo,ukimpiga sehemu ya nyuma ya mgongo ambapo figo zinapatikana husikia maumivu makali
 
Deep stick sometimes usomaji wake unakuwa mgumu kwa mtu kuangalia rang zile

Njia pekee Ni kuotesha tu ( urine calct)
Kufanya culture ni gharama na hospital nyingi hawana uwezo...na mara nyingi culture hufanywa hasa pale panatokea drug resistance
 
1. wote wnye magonjwa ya zinaa wanasema wana UTI.
2.Maabara zinataka ziuze dawa.
3.Kwa wanawake ugonjwa wa fangasi ukeni ni kitu cha kawaida sana lakini mtu atakwambia nina UTI na si fangasi.
4.Utamaduni wetu wa kuchambia maji unatucost sana.
 
1. wote wnye magonjwa ya zinaa wanasema wana UTI.
2.Maabara zinataka ziuze dawa.
3.Kwa wanawake ugonjwa wa fangasi ukeni ni kitu cha kawaida sana lakini mtu atakwambia nina UTI na si fangasi.
4.Utamaduni wetu wa kuchambia maji unatucost sana.
Tuchambie nini Boss?
 
Kuna siku nilienda hospitali nikiwa najisikia vibaya,baada ya vipimo nikapewa dawa bila maelezo. Ikabidi nimrudie dk kuwa dawa hizi ni za nini? Naambiwa 'Una typhoid kwa mbali' Sikunywa hizo dawa na hadi leo sijisikii tatizo lolote.

Wapo ambao kweli wanaumwa,lakini hili suala la Typhoid na U.T.I linanipa mashaka sana. Nadhani kuna biashara ndani yake ambayo hawaangalii madhara kwa mtumiaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…