Madaktari na wataalamu wa chakula, kwa nini haishauriwi kuongeza chumvi baada ya chakula kuiva?

agudev

Member
Joined
Apr 5, 2016
Posts
80
Reaction score
128
Hili swali nimekuwa nikijiuliza bila kuelewa, nimekuwa nikisikia majibu kama chumvi mbichi na chumvi iliyoiva, sielewi ni namna gani chumvi inaitwa imeiva wakati yenyewe ni kemikali.

Tuchukulie mifano hii:
  1. Nimepika maharage kilo moja bila kutia chumvi halafu nikaja kuongeza vijiko vitatu vya chumvi baada ya maharage kuiva na kuiacha kwa muda ili chumvi iyeyuke na kuenea kwenye maharage
  2. Nimepika maharage kilo moja na kuongeza chumvi vijiko vitatu nikaacha viive kwa pamoja

Je, kuna tofauti gani kati ya mapishi haya mawili ikiwa kiasi sawa cha chumvi kimewekwa kote na kimesabaa kwa uwiano sawia?
 
Sio kwamba hairuhusiwi, hapana! ila ni "Haishauriwi" kufanya hivyo kutokana na maelezo yafuatayo:

Ukiweka chumvi wakati wa kupika chakula utafanya chumvi ienee vizuri katika chakula chako, hivyo kiwango cha chumvi itakayotumika kitakua ni kile tu kinachotakiwa kunogesha chakula chako hivyo mwili wako utapata kiwango kidogo cha chumvi.

lakini ukitumia chumvi ya kuongeza kidogo kidogo mezani wakati wa kula, itakufanya utumie chumvi nyingi zaidi ya inavyotakiwa
(Assume ukiwa unakula nyama isiyowekwa chumvi kabla ya kupikwa, kila wakati utakua unachovya chumvi ili usikie ladha si ndio?)

Hali hii itasababisha mwili wako kuwa na chumvi nyingi hivyo kukusababishia Magonjwa kama shinikizo la damu (Blood pressure and hpertension) na mawe ya figo (kidney stone)
 
Tukichukulia mifano hii:
  1. Nimepika maharage kilo moja bila kutia chumvi halafu nikaja kuongeza vijiko vitatu vya chumvi baada ya maharage kuiva na kuiacha kwa muda ili chumvi iyeyuke na kuenea kwenye maharage
  2. Nimepika maharage kilo moja na kuongeza chumvi vijiko vitatu nikaacha viive kwa pamoja

Je, kuna tofauti gani kati ya mapishi haya mawili ikiwa kiasi sawa cha chumvi kimewekwa kote na kimesabaa kwa uwiano sawia?
 
Tukichukulia mifano hii:
  1. Nimepika maharage kilo moja bila kutia chumvi halafu nikaja kuongeza vijiko vitatu vya chumvi baada ya maharage kuiva na kuiacha kwa muda ili chumvi iyeyuke na kuenea kwenye maharage
  2. Nimepika maharage kilo moja na kuongeza chumvi vijiko vitatu nikaacha viive
chumvi iive na chakula, ili uvunjike vizuri na iweze kubalance vizuri kwenye mlo wote, kusiwe na different concentration. maana chumvi unayoongeza baadae haita breakdown vizuri na ku distribute vizuri, hvyo digestion na absorption yake ni tofauti. so ishu ni difference in concentration/density
 
Kuongeza chumvi baada ya chakula kuiva haishauriwi kwa sababu inaweza kuwa hatari kwa afya yako...

Kwa kawaida, chumvi ina kiwango kikubwa cha sodiamu ambayo huyeyushwa na kuunguzwa pale inapochemswa..

kuongeza baada ya hapo hupelelekea mwili kupokea kiwango kikubwa cha sodium ambayo hupelekea kuongeza shinikizo la damu, na hii inaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, na pia magonjwa mengine kama kisukari...
 
chumvi iive na chakula, ili uvunjike vizuri na iweze kubalance vizuri kwenye mlo wote, kusiwe na different concentration. maana chumvi unayoongeza baadae haita breakdown vizuri na ku distribute vizuri, hvyo digestion na absorption yake ni tofauti. so ishu ni difference in concentration/density
Exactly...
 
Back
Top Bottom