Madaktari tumieni busara


Wao wanapelekana apollo hivyo hawatujali kabisa! Tukidai walau haki yetu na haki ya wagonjwa tunaowahudumia wanatangaza eti tumekosa uzalendo?! Na wananchi kwa kuzoea majibu mepesi wanawakubalia! na kuwasapoti! Tujiulize kwa makini ni yupi aliyekosa uzalendo kati yetu??!!
Wakati flani wiki chache zilizopita nilikuwa mwanza,nikaingia labor ward ya hospitali ya wilaya Nyamagana, kweli hali inatisha! Hakuna kila kitu.. mama anaambiwa aje na Pamba, Gloves, hadi Oxytocin! Hakuna hata cannula za kuwapa wagonjwa dripu. Hakuna wala BP mashine!! (Haya nimeyashuhudia kwa macho yangu) Na hapo ilikuwa katika Jiji la mwanza, tena hospitali ya wilaya, je kule vijijini?
Na haya ndo mazingira yetu ya kufanya kazi, kila siku. Na kwa majibu ya yule 'kiongozi' ni kama anamaanisha tukome, kwa sababu tulishindwa kuchagua (ama labda wazazi wetu walishindwa kutuchagulia) masomo yenye future angavu zaidi?! Tujiulize busara ya hawa 'watawala' imekwenda wapi katika zama hizi?!
Sasa, tumeamua kujisimamia na kusema kile tunachoamini ni sahihi na hiyo ndiyo maana halisi ya busara.

 
Kwanin watu mnawalaum madaktari??

Nakwanin lawama hizo wasilaumiwe viongozi na serikali kwa ujumla??

Nyie hamuoni kama wamefanya busara kubwa sana kutoa msimamo wao wametoa malalamiko yao kwa serikal na wao hawataki kuwakamilishia wanaamua kugoma watu wanawalaumu je wangegoma kimya kimya nyie mnao walaum sindiyo mnakuwa wakwanza kung'aka ??

Ni nan awezaye kufanya kazi huku hanachochote mfukoni na kwake wanawe wanalia njaa?? Na huku haki yao kunawachache wameikalia??

Nawaunga mkono asilimia 800 wagome mwanzo mwisho mbona wao wabunge wamejiongezea posho kimya kimya na wananch walivyo ng'aka na kulalamika hawakuwa tayari kuchukua maamuzi ya busara??

Wao walidai maisha yamepanda bei kwan wao wanaishi wapi na maisha gan? Na madaktari wanaishi wapi??
 
halafu utakuta tangazo eti mama mjamzito huduma bure kila kona,,,,,,, wanawapa shida wafanyakazi wanaonekana wanapenda pesa...
 
inasemekana hiki ndicho kilichojibiwa kwa wawakilishi wa madaktari walivyoenda ofisi ya waziri mkuu.sasa kama ni kweli hapa ndipo utaona aina ya viongozi tulionao nchini.je ni yupi aliyepungukiwa busara?
maana yake ni kwamba kuna wale njaa mbele watawageuka wenzao...
 
 
Hili tatizo la madaktari na serikali naona sasa limegeuzwa la kisiasa!!
 


Wakumbuke pia kuwa viapo walivyoapa havikuchanganya maneno yenye kusadikisha migomo. Malaika wao waliyanukuu vizuri na watajibu siku ya hukumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…