Bob Lee Swagger
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 1,362
- 517
Mungu tubariki tunapokwenda kufanya maamuzi magumu leo hapo Don Bosco...tutumie busara, pasi na jazba...ila busara yangu, inaweza ikawa upuuzi kwako. Kwetu sisi madaktari..kwa sasa hali ilipofikia, na matusi ambayo tumeshatukanwa..MGOMO ni busara kwetu. Natanguliza samahani kwa waTanzania wote watakaoathirika na uamuzi wetu. Lakini gharama inabidi ilipwe, na tunatamani kama gharama hiyo ingelipwa na serikali...na si mwananchi mlalahoi mwenzetu! Lakini huyu mlalahoi naye ana jukumu kwa madaktari, kama kweli anathamini mchango wetu kwa jamii...na jukumu lake ni kuwa mkweli na kutusupport!
Kama wanajamii ya Tanzania nao hawathamini mchango wetu katika kusimamia afya zao...basi sisi wa nini tena?! Hatuhitajiki, hata tukigoma hakuna athari! Lakini kama kutakuwa na athari, basi tunahitajika..na hivyo tuthaminiwe! We are going to DEMONSTRATE...demonstrate kuwa tunahitajika maana kuna malimbukeni serikalini na kwa baadhi ya wananchi hawajui hilo!
Mungu uwe nasi....mungu uwe na waTanzania. Nikiwa mwanachama mwaminifu wa MAT tunasema...tunawapenda sana waTanzania, na tutaendelea kuwapenda!
NB: Naelekea Don Bosco.
Wao wanapelekana apollo hivyo hawatujali kabisa! Tukidai walau haki yetu na haki ya wagonjwa tunaowahudumia wanatangaza eti tumekosa uzalendo?! Na wananchi kwa kuzoea majibu mepesi wanawakubalia! na kuwasapoti! Tujiulize kwa makini ni yupi aliyekosa uzalendo kati yetu??!!
Wakati flani wiki chache zilizopita nilikuwa mwanza,nikaingia labor ward ya hospitali ya wilaya Nyamagana, kweli hali inatisha! Hakuna kila kitu.. mama anaambiwa aje na Pamba, Gloves, hadi Oxytocin! Hakuna hata cannula za kuwapa wagonjwa dripu. Hakuna wala BP mashine!! (Haya nimeyashuhudia kwa macho yangu) Na hapo ilikuwa katika Jiji la mwanza, tena hospitali ya wilaya, je kule vijijini?
Na haya ndo mazingira yetu ya kufanya kazi, kila siku. Na kwa majibu ya yule 'kiongozi' ni kama anamaanisha tukome, kwa sababu tulishindwa kuchagua (ama labda wazazi wetu walishindwa kutuchagulia) masomo yenye future angavu zaidi?! Tujiulize busara ya hawa 'watawala' imekwenda wapi katika zama hizi?!
Sasa, tumeamua kujisimamia na kusema kile tunachoamini ni sahihi na hiyo ndiyo maana halisi ya busara.