Madaktari tumieni busara

Madaktari tumieni busara

Mungu tubariki tunapokwenda kufanya maamuzi magumu leo hapo Don Bosco...tutumie busara, pasi na jazba...ila busara yangu, inaweza ikawa upuuzi kwako. Kwetu sisi madaktari..kwa sasa hali ilipofikia, na matusi ambayo tumeshatukanwa..MGOMO ni busara kwetu. Natanguliza samahani kwa waTanzania wote watakaoathirika na uamuzi wetu. Lakini gharama inabidi ilipwe, na tunatamani kama gharama hiyo ingelipwa na serikali...na si mwananchi mlalahoi mwenzetu! Lakini huyu mlalahoi naye ana jukumu kwa madaktari, kama kweli anathamini mchango wetu kwa jamii...na jukumu lake ni kuwa mkweli na kutusupport!

Kama wanajamii ya Tanzania nao hawathamini mchango wetu katika kusimamia afya zao...basi sisi wa nini tena?! Hatuhitajiki, hata tukigoma hakuna athari! Lakini kama kutakuwa na athari, basi tunahitajika..na hivyo tuthaminiwe! We are going to DEMONSTRATE...demonstrate kuwa tunahitajika maana kuna malimbukeni serikalini na kwa baadhi ya wananchi hawajui hilo!

Mungu uwe nasi....mungu uwe na waTanzania. Nikiwa mwanachama mwaminifu wa MAT tunasema...tunawapenda sana waTanzania, na tutaendelea kuwapenda!

NB: Naelekea Don Bosco.

Wao wanapelekana apollo hivyo hawatujali kabisa! Tukidai walau haki yetu na haki ya wagonjwa tunaowahudumia wanatangaza eti tumekosa uzalendo?! Na wananchi kwa kuzoea majibu mepesi wanawakubalia! na kuwasapoti! Tujiulize kwa makini ni yupi aliyekosa uzalendo kati yetu??!!
Wakati flani wiki chache zilizopita nilikuwa mwanza,nikaingia labor ward ya hospitali ya wilaya Nyamagana, kweli hali inatisha! Hakuna kila kitu.. mama anaambiwa aje na Pamba, Gloves, hadi Oxytocin! Hakuna hata cannula za kuwapa wagonjwa dripu. Hakuna wala BP mashine!! (Haya nimeyashuhudia kwa macho yangu) Na hapo ilikuwa katika Jiji la mwanza, tena hospitali ya wilaya, je kule vijijini?
Na haya ndo mazingira yetu ya kufanya kazi, kila siku. Na kwa majibu ya yule 'kiongozi' ni kama anamaanisha tukome, kwa sababu tulishindwa kuchagua (ama labda wazazi wetu walishindwa kutuchagulia) masomo yenye future angavu zaidi?! Tujiulize busara ya hawa 'watawala' imekwenda wapi katika zama hizi?!
Sasa, tumeamua kujisimamia na kusema kile tunachoamini ni sahihi na hiyo ndiyo maana halisi ya busara.

 
Kwanin watu mnawalaum madaktari??

Nakwanin lawama hizo wasilaumiwe viongozi na serikali kwa ujumla??

Nyie hamuoni kama wamefanya busara kubwa sana kutoa msimamo wao wametoa malalamiko yao kwa serikal na wao hawataki kuwakamilishia wanaamua kugoma watu wanawalaumu je wangegoma kimya kimya nyie mnao walaum sindiyo mnakuwa wakwanza kung'aka ??

Ni nan awezaye kufanya kazi huku hanachochote mfukoni na kwake wanawe wanalia njaa?? Na huku haki yao kunawachache wameikalia??

Nawaunga mkono asilimia 800 wagome mwanzo mwisho mbona wao wabunge wamejiongezea posho kimya kimya na wananch walivyo ng'aka na kulalamika hawakuwa tayari kuchukua maamuzi ya busara??

Wao walidai maisha yamepanda bei kwan wao wanaishi wapi na maisha gan? Na madaktari wanaishi wapi??
 
wao wanapelekana apollo hivyo hawatujali kabisa! Tukidai walau haki yetu na haki ya wagonjwa tunaowahudumia wanatangaza eti tumekosa uzalendo?! Na wananchi kwa kuzoea majibu mepesi wanawakubalia! Na kuwasapoti! Tujiulize kwa makini ni yupi aliyekosa uzalendo kati yetu??!! Wakati flani wiki chache zilizopita nilikuwa mwanza,nikaingia labor ward ya hospitali ya wilaya nyamagana, kweli hali inatisha! Hakuna kila kitu.. Mama anaambiwa aje na pamba, gloves, hadi oxytocin! Hakuna hata cannula za kuwapa wagonjwa dripu. Hakuna wala bp mashine!! (haya nimeyashuhudia kwa macho yangu) na hapo ilikuwa katika jiji la mwanza, tena hospitali ya wilaya, je kule vijijini?na haya ndo mazingira yetu ya kufanya kazi, kila siku. Na kwa majibu ya yule 'kiongozi' ni kama anamaanisha tukome, kwa sababu tulishindwa kuchagua (ama labda wazazi wetu walishindwa kutuchagulia) masomo yenye future angavu zaidi?! Tujiulize busara ya hawa 'watawala' imekwenda wapi katika zama hizi?!sasa, tumeamua kujisimamia na kusema kile tunachoamini ni sahihi na hiyo ndiyo maana halisi ya busara.
halafu utakuta tangazo eti mama mjamzito huduma bure kila kona,,,,,,, wanawapa shida wafanyakazi wanaonekana wanapenda pesa...
 
inasemekana hiki ndicho kilichojibiwa kwa wawakilishi wa madaktari walivyoenda ofisi ya waziri mkuu.sasa kama ni kweli hapa ndipo utaona aina ya viongozi tulionao nchini.je ni yupi aliyepungukiwa busara?
maana yake ni kwamba kuna wale njaa mbele watawageuka wenzao...
 
Maneno haya yalishawekwa humu toka juzi!! usome thead nyingine mkuu!" Nawashangaa sana nyie madaktari mambo mnayofanyiana, yaani hampendani kabisa, hamna confidence na hata mkiweka tools down haitowasaidia! " "Nilifaulu PCB,lakini kwa kutambua ubovu wa MEDICINE mzazi wangu akanisomesha ACCOUNTS,sasa sijui mnalalamikia nini!, mlichagua wenyewe"
KWA MAJIBU YA DIZAINI HII BADO TUNAITA TUNA VIONGOZI KWELI?
 
Hili tatizo la madaktari na serikali naona sasa limegeuzwa la kisiasa!!
 
Leo katika gazeti la Mwananchi , kuna taarifa ya Makamu wa Rais wa Chama cha madaktari Tanzania (MAT), Primus Saidia kwamba Majibu toka kwa mwakilishi wa ofisi ya Waziri Mkuu yamewakatisha tamaa. Aidha kuna taarifa kwamba huduma katika hospitali ya muhimbili imedorora na kwamba kuna dalili kwamba kuna uwezekano wa kuwepo mgomo siku ya Jumatatu yaani kesho.


Pamoja na taarifa hiyo ya Dk Saidia , sikuona aya iliyotamka majibu walioyapata toka kwa Waziri Mkuu. Je majibu hayo ni siri?

Najiuliza swali hilo kwa vile ninakuwa na wasiwasi sana kwamba, isije ikawa Madaktari nao wanalihusisha tatizo hilo na mambo ya siasa na kujisahau kwamba wao ni wataalamu. Watuambie ni majibu gani wamepewa toka ofisi ya waziri Mkuu ili watanzania tujue ukweli. Mimi naamini Serikali inatambua umuhimu watumishi wake wote na siyo Madaktari pekee. Busara zaidi zinahitajika toka kwa wataalam wetu hawa. Wapime, wakumbuke pia kuwa Serikali haijishughulishi na Madaktari tu. Ni wazi kabisa kwamba madai yao ni halali, lakini kutokana na ukweli kwamba siyo wao peke yao wanaohitaji kuhudumiwa na Serikali , wanaowajibu wa kuangalia ukweli wa viwango wanavyovidai kwa kutambua kwamba ni watumishi wa umma kama watumishi wengine kama mwalimu, mhandisi, askari na wengine wengi. Zaidi wajiulize na kutafakari juu ya nafasi zao na jinsi ambavyo sasa wagonjwa wanapata shida pale. Muhimbili.


Wakumbuke pia kuwa viapo walivyoapa havikuchanganya maneno yenye kusadikisha migomo. Malaika wao waliyanukuu vizuri na watajibu siku ya hukumu!
 
Back
Top Bottom