Madaktari wa kitengo cha dharura Muhimbili mmenitoa machozi

dala dala

Senior Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
106
Reaction score
105
Mara kadhaa watoa huduma za Afya hapa nchini wamekuwa wakishutumiwa kwa kutoa huduma chini ya matarajio ya wateja wao yaani clients. Inawezekana kabisa kukawa na ukweli katika hili au pengine ukweli huu unaongezwa chumvi sana. Ninashawishika kuweka mada hii katika JF kwa lengo la kutoa ushuhuda wa utendaji uliotukuka niliouona kutoka kwa wahudumu katika hospitali zetu za serikali hapa nchini.

Hivi karibuni nilipata mkasa ambapo mwanafamilia yangu alipata ajali ya moto nikalazimika kutafuta huduma katika hospitali za serikali hapa Jijini Dar es salaam. Nilikuwa na hofu endapo atapata huduma stahiki ukizingatia hali yake ilivyokuwa. Awali alipelekwa Hospitali ya Mkoa (jina linahifadhiwa) na kisha kupata rufaa katika Hospitali ya Taifa yaani Muhimbili National Hospital (MNH).

Nilichokishuhudia katika hospitali hizi mbili ni kitu cha ajabu ambacho sikufikiria kukutana nacho katika hospitali zetu. Ni kweli kuna changamoto za mazingira magumu sana ya kazi, ukosefu wa vitendea kazi pamoja na madawa lakini kipekee na mbele za Mungu aliye Hai ninapenda kutoa shukurani na pongezi nyingi kwa timu ya Madaktari vijana ambao kwa kweli wamejipanga vizuri hasa eneo la Casuality au Emergency pale MNH. Kwa macho yangu nilishuhudia upendo mkubwa na roho ya kizalendo waliokuwa nayo wale vijana. Wanajituma na pia wana lugha nzuri kwa wagonjwa. Vile vile wanaonekana wameenda madarasa vizuri. Pengine hili limewaongezea uelewa wa nini maana ya UHAI wa mtu kwamba ukitoka haurudi tena hivyo ni lazima upiganiwe kwa gharama zozote.

Nilishuhudia mtoto wa miaka kati ya 7 na 10 akiletwa kutoka mojawapo ya satellite hospitals akiwa na majeraha ya kuanguka mtini. Aliletwa na bibi yake na kwa haraka ilikuwa wazi kuwa wametoka katika familia yenye uchumi mgumu sana. Vipimo zaidi ya vitano (x-ray, damu, etc) vilihitajika kuchukuliwa ambapo wanandugu (bibi) alitakiwa kulipia. Kama nilivyosema awali, bibi hakuwa na uwezo wa kulipia hata shilingi mia, nilishangaa kuona vijana wale wanapitisha karatasi kwa ajili ya kuchangia huduma za vipimo. Walitoa kwa moyo wa upendo (hata kama mtu haamini hili lakini ndio ukweli), nilihisi kuguswa sana na uzalendo huu. Katika dunia ya leo aghalabu mara chache unaweza kushuhudia mambo haya yakitendeka. Nilijisikia furaha sana kutambua kuwa kuna wazalendo katika nchi hii wenye kuipenda nchi yao na watu wao licha ya mazingira magumu sana ya kazi.

Sina cha kuwalipeni enyi watoa huduma wa Emmergency Muhimbili zaidi ya kuwaombea kwa Mungu awajaze Baraka zake ziwafuate popote pale mtakapokuwa ninyi na vizazi vyenu. You showed me what it takes to be a Doctor/Nurse/Pharmacist and others in the Health Sector. Rai yangu kwa serikali ni kwamba watazameni kwa jicho la tatu watoa huduma hawa. Boresheni mazingira yao ya kazi, watatufanyia mengi mazuri. Zile fedha za ESCROW ziende huku jamani, wapeni hawa watusaidie sisi wenye nchi hii.

Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo na pia ALLAH kwa upande wa pili awabariki sana enyi Madaktari wa MNH.
BIG UP THE YOUNG DOCTORS AT MUHIMBILI CASUALITY; I’M PROUD OF YOU GUYS.
 
Ulienda tarehe ngapi....muda gani...we need to award the guys
 
Asante kwa kutuhakikishia kuwa kumbe wazalendo bado wapo ktk nchi hii,mana wengi wetu tumekata tamaa!Hao madaktari wanastahili pongezi za dhati! Mungu abariki kazi za mikono yao na familia zao!
 
Mungu awabariki sana hao vijana na awaongezee akiba ya uhai ili waendelee kututumikia. katika dunia hii ya kibwanyenye chini ya utawala wa KIFISADI wa serikali ya CCM ni nadra sana kuwakuta wazalendo kama hao. God bless u so much guys.
 
Ni matumaini yangu na wewe ulichangia pesa katika suala la huyo mtoto. Hongera sana kwa madaktari
 
Unachosema ni kweli kabisa. Washkaji wa pale emergency wako poa sana. Niliwahi kupelekwa pale nikiwa hoi lakini huduma n faraja nilipona fasta kuliko muda uliotegemewa.
 
Basi ni jambo la heri sio mbaya, tutawakumbuka hata kwa hilo
 
Reactions: BAK
Ulienda tarehe ngapi....muda gani...we need to award the guys

Naunga mkono hoja
Itasaidia kujua ni nani walikuwa zamu na ikiwwzekana kuwa rewarded.

Thx Youngs doctors at least ubinadamu unaanza kurudi katika sehemu nyeti kama hospital!
 
Reactions: BAK
Mungu mkubwa safi vijana bt hyo heading imenitisha
 
Kuna watu wana mioyo ya kujituma suna wawapo kwenye sehemu zao za kazi. Ila wanaharibiwa na kuchafuliwa na watu wachache sana.
 
Mungu awabariki sana hao vijana,wenye moyo wa uzalendo bado wapo,ila hiki kitengo cha Emergency wako vizuri wengi wao wana moyo mzuri hasa katika kumtia moyo mgonjwa.
 
Reactions: BAK
Muhimbili inavurugwa na wakurugenzi waliopo na siyo serikali
 
Nami nakuunga mkono Mkuu dala dala Mungu atawajalia heri wachapa kazi wa hapo Emergency MNH. Mimi nilimpeleka Baba yangu jinsi alivyohudumiwa nilifarijika sana sikuamini! kuna Dr.Miranda alikuwa anambembeleza Mzee wangu kama mtoto wake kwa kila alichokuwa anamfanyia.

Mungu awabariki sana kwa roho zenu za huruma
 
Reactions: BAK
Hongera umesema Hospitali ya Muhimbili je Hospitali zingine kama za Ilala Amana ,Magomeni na Mwananyamala wanatoa huduma nzuri? au hapo tu Muhimbili tu?
 

Machozi ya furaha: cc King'asti - kumbuka maneno yako kwa thread ya Dark City: Mwanyasi yuko.....
 
Last edited by a moderator:
Hahaha kaka hata nakumbuka basi? Nikumbushe bwana, nazeeka dada yako.

Ila two weeks ago shosti wangu alikuwa anauguza mama yake mzazi MOI. Yaanj walitoa laki 2 ili apate private room na ilishindikana. Japo alipata kitanda, hakulazwa chini. Zile wards za muhimbili, nakumbuka kumuambia BAK kuwa nilienda kumtfuta mgonjwa mmoja nikajisikia kama mchawi. Viatu vyangu vya kokoko nilitamani kushikilia mkononi, kiukweli niliona aibu mbele ya wapiga kura wale (nikaelewa kwa nini waziri mkuu analiaga)
Machozi ya furaha: cc King'asti - kumbuka maneno yako kwa thread ya Dark City: Mwanyasi yuko.....
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…