Madaktari wahamasishe ulaji wa ugali wa dona

Madaktari wahamasishe ulaji wa ugali wa dona

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
2,956
Reaction score
1,114
Moja ya sababu za maradhi yasiyoambukiza lakini yamewaathiri watu wengi (lifestyle diseases) ni ulaji mbovu wa vyakula hasa vya asili ya wanga na mafuta. Maradhi haya ni kisukari, maradhi ya moyo n.k

Kwa kuwa chakula kikuu cha wananchi wetu ni ugali wa mahindi nawashauri madaktari wetu wawashauri wagonjwa wao waachane ulaji wa ugali wa sembe kila wanapokwenda kwao kwa matibabu. Pia wenye mashine za kusaga unga wabadilike na kuanza kusaga unga wa dona wenye ubora ili tuanze kuuzoea.
 
Lakini mkuu hiyo dona inahitaji maandalizi ya kuosha vizuri ili kutoa ile sumu inayotumiwa kuhifadhia mahindi vinginevyo isipofanyiwa usafi dona hiyo italeta madhara kwa Afya za binadam
 
Lakini mkuu hiyo dona inahitaji maandalizi ya kuosha vizuri ili kutoa ile sumu inayotumiwa kuhifadhia mahindi vinginevyo isipofanyiwa usafi dona hiyo italeta madhara kwa Afya za binadam
Lakini kukoboa sio dawa ya kuziondoa hizo sumu pia.

Sent from my SM-N9002 using JamiiForums mobile app
 
Lakini mkuu hiyo dona inahitaji maandalizi ya kuosha vizuri ili kutoa ile sumu inayotumiwa kuhifadhia mahindi vinginevyo isipofanyiwa usafi dona hiyo italeta madhara kwa Afya za binadam
Ndiyo maana nimeeleza kuwa wenye mashine wasage unga ulio bora kwa kuyaosha mahindi vizuri na kuyakausha. Pale NMC Arusha kuna mashine yenye kupepeta, kuyaosha, kuyakausha na kusaga dona. Wawekezaji wengine wachukue fursa hiyo na nina hakika watapiga pesa kwani wengi tunajali afya zetu.
 
Back
Top Bottom