#COVID19 Madaktari waishauri Serikali chanjo ya Corona kuwa ya lazima

Point kubwa sana umeandika mzee👋👏
 
Hawa sio wataalam? Hebu soma profile yao na kwa nini wamejiuzulu!

 
Sasa wewe inakuuma nini tukiwa wapumbavu? Au kinakusokota nini tukifa? Si ndio vizuri mbakie mliochanja werevu? Kinachokufurukuteni ni kipi haswa?

Empty head kabisa wewe!
 
Kwahiyo unashauri nini?
Sina ushauri kwa kuwa mpaka sasa ni jambo la hiari kila mtu atajuwa anataka nini ila kitu kimoja na uhakika baadae itakuwa ni lazima na zitatumika njia mbadala kulazimisha nchi zingine wameshaanza huwezi kwenda kazini kama hujachanja huwezi kwenda ofisi za serikali hujachanza watumishi wa umma utachagua kazi au chanjo taratibu itaanza optional lakini itabadilika. Corona haitaisha leo wala kesho kila mwaka kuna wave mpya inakuja tuko ya 3 sijui ya 4 na wameshasema dawa ni kuchanja tu huko mbele hutarusuhiwa kuhatarisha maisha ya watu wengine sababu ya maoni ya mtu binafsi huu ugonjwa wa dunia sio Tanzania tu. Nakuhakikishia iko siku watu watapiga foleni kuomba chanjo na hii msg yangu hifadhi utakumbuka haya maneno. Iko siku hata CV za kazi kigezo itakuwa umechanja? kuingia chuo umechanja? yanakuja yote haya na ubishi utaisha tu dunia imeamua ni suala la muda tu.
 
Wewe si uchanjetu basi
Na wewe si usichanje tu kuna sehemu nimelazimisha mtu akachanje? mbona mnajitoa ufahamu. kwa taarifa yako siku itakuja utaitafuta mwenyewe chanjo na hili linakuja wala usiwe na hofu ubishi wote utaisha usidhani sasa hivi unabembelezwa ndio itakuwa hivi maisha taraitibu mtu ataambiwa achague achanjwe au akae nyumbani maana hata kubaliwa sehemu taratibu tu imeanza... mark hii msg
 
Kati ya watanzania milioni 57 waliochanja hawafiki Laki nne, ina maana hao million 56 wote wasiochanja ni wafuasi wa Askifu Gwajima?
 
Lakini waliochanja wataendelea kufa na kuambukiza.
 
Lakini waliochanja wataendelea kufa na kuambukiza.
Elimu inayotolewa ndogo sana ndio tatizo. Hakuna chanjo duniani inazuia kufa huu ni opotoshaji. Chanjo inakusaidia kutoumwa sana mpaka kufikia kuhitaji huduma za ICU inapunguza makali lakini haina maana huwezi kuumwa kuambukiza asilimia 10% mtu aliyechanja anaweza kuambukiza ndio maana nchi zingine ukiwa umechanja hutakiwi kuwa quarantine chance ya kuambukiza ndogo. Kufa tutakufa tu iwe corona au sio corona haina maana kwa kuwa siku tutakufa tu basi tusipate tiba. Sasa ukiweza kupunguza hatari ya kuumwa kwa asilimia 90% utapuuza hili? Hakuna sehemu yoyote wamesema ukichanjwa basi wewe huwezi kufa ila unapunguza hatari kwa kiasi kikubwa na hili data zimethibitisha hili. Elimu haijatolewa vizuri kwa watu na sitaki kumlaumu tu kama hajapata taarifa za kutosha ana haki ya kuuliza ila hata hao wanaokuja na hoja mnapewa msizae hoja dhaifu maana kama issue kuzaa basi wangewachoma watoto wachanga ambao tunawapeleka clinic wenye future waje wanichome mimi nimeshajichokea na watoto kumi huko na wala siwezi kuzaa tena.
 
Uliyaelewa vizuri maelezo ya madaktari wakati wakishauri chanjo iwe lazima? Walidai wananchi wengi kutokuchanja imesababisha wao madaktari wafe kwa kuambukizwa wakati wanawatibu hao wananchi wasiochanja. Sasa swali madaktari wanakufaje wakati wamechanja na hata kwa mujibu wa maelezo yako ukichanja uko safe?
 
Kati ya watanzania milioni 57 waliochanja hawafiki Laki nne, ina maana hao million 56 wote wasiochanja ni wafuasi wa Askifu Gwajima?
Usipochanja ni mjinga tu rudia kusoma comment yangu usipoelewa mwombe Mungu akuepushe na corona.

Kitabu ninacho kiamini Biblia kuna story 2 za mfano


1. Nabii Nuhu aliokoka peke yake na familia yake wengine wote tunaambiwa waliangamia.

2. Sodoma na Gomora ni story nyingine alitoka Lutu peke yake

Jaribu kufunguka kichwa bro hivi nani aliyekwambia wanachokiamini wengi ndio sahihi, nimekupa huo mfano ili kukusaidia kufikiri.

Hata historia inaonyesha waliogundua ndege, umeme, na kwamba dunia ni mviringo walipata shida kuaminika.

Ukiona huwezi kubungua bongo na kufanya upembuzi mwenyewe kama wewe ila una fuata upep0 wa wingi basi jihesabu umetumbukia katika dimbwi la wajinga waliopitiliza. Na hakuna atakekusaidia mpaka likukute la kukufundisha.
 
Usipochanja ni mjinga tu rudia kusoma comment yangu usipoelewa mwombe Mungu akuepushe na corona.
Sijachanja na sitachanja kamwe na ninadunda fit tu. Ninamtegemea Mungu sana na ndiye anayenikinga na corona.

Mjinga ni wewe unayejifanya una uchungu sana na wasiochanja.
 
Wameshauri lini na wapi?

Mbona unaokoteza ubuyu na kutuhatibia misingi ya great thinkers?
 
Mimi sishangai kwan Tanzania ndo inch yenye madakitar wasio prove hakil yao nakuwa tegemez kifikra , ndo maana wakiulizwa hata content za chanjo hawajui chochote, swal linakuja inakuwaje mtu ambaye hana na hajui chochote kuhusu hicho kitu half anashaul watu milion 60 watumie ? huo ni ulemavu wa hakil
 
Chanjo hauziuii kuambiukizwa au kuambukiza corona...

Chanjo zinapelekesha haswa...

Wanaofariki kwa chanjo ni wengi kuliko wasiochanjwa...
 
Mimi nadhani hayo ni maneno yako ukisema wamesema wanakufa ungeweka data ni wangapi wamepata na wangapi wamekufa? Je wangekuwa hawajachanja kabisa number zingekuwa vipi? kusema sisi tunakufa huku tumechanja na watu wachanjwe haileti maana. Ni wapi wamesema ukichanja ndio uko safe 100%. Chanjo inapunguza watu kuumwa sana mpaka kufikia kuwa ICU au inapunguza makali ya ugonjwa kwa kiasi kikubwa kuumwa bila kufikia hatua mbaya, na hili limethibitishwa nchi zilizochanja kwa wingi corona ipo lakini ICU ziko empty kuna wakati kabla ya chanjo kulikuwa hakuna nafasi Hosp zimejaa watu ICU leo corona ipo lakini hawafikii kuumwa kwenda Hosp. Chanjo haizuii kifo inapunguza kwa kiasi kikubwa sana. Ni kama dawa za malaria zipo na ukiumwa malaria chance kubwa utapona ukitumia dawa lakini pia kuna watu wanakufa na malaria pamoja na kutumia dawa sasa ingekuwa hakuna dawa kabisa za malaria ingekuwaje kwa wagonjwa. hoja utasema situmii dawa ya malaria faida yake nini mbona watu wanakufa kwa malaria.
 
Sijachanja na sitachanja kamwe na ninadunda fit tu. Ninamtegemea Mungu sana na ndiye anayenikinga na corona.

Mjinga ni wewe unayejifanya una uchungu sana na wasiochanja.
Nimeshajanja single dose tarehe 12 Aug. Hao madaktari ndio wananafasi nzuri ya kujua wanaokufa waliochanja au wasiochanja, sababu kila siku watu wanakufa kazini kwao.

Wewe na mimi labda hatuna nafasi hiyo acha kujidai mjanja.
Woga wa kufa tu na story za Gwaji.

Ukiulizwa kwa nini huchanji utajibu upuuzi tu ndio mana nimekupa list ya nchi wamegundua chanjo wenyewe rudia comment, sio lazima uchanje ila likitokea lile balaa ujilaumu mwenyeee.
 
Chanjo hauziuii kuambiukizwa au kuambukiza corona...

Chanjo zinapelekesha haswa...

Wanaofariki kwa chanjo ni wengi kuliko wasiochanjwa...
We ni daktari, weka takwimu hapa. Walichanja laki 4 waliokufa wangapi ?
 
M
Wanapukutika wengine sana...
Na wengine wapo hoi hawajielewi sababu ya chanjo...
Mi nimechanja acha uongo. Naona woga wa kufa unakusumbua.

Sijui kwa wengine mi nimechanja maneromango kisarawe,
Hakuna homa wala kichwa kuuma wala nini, wala kizunguzungu, huenda wengine wamepata hayo matatizo. Hata bomba la kutolea maji kwa mbele liko safi kwa utendaji wake, wife hajasema lolote.

Ila usiseme wengi sana, tsja namba, waliochanja laki 4, hao madaktari wanaxo taarifa na takwimu ambazo wewe huna.
 
Inasikitisha sana... Watu wanataabika...
Misiba ni miingi baada ya chanjo...

Watu wanashindia sawa za maumivu na miti shamba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…