Madaktari wameshauri akatwe miguu

Madaktari wameshauri akatwe miguu

Joined
Aug 27, 2013
Posts
40
Reaction score
8
Nina mtoto mwenye umri wa mwaka moja na busy na amezaliwa na ulemavu wa miguu yaani anamfupa mmoja kila mguu madaktar Wanasema akatwe miguu kuanzia kwenye magoti ili aanzishwe mazoezi ya viungo bandia sasa ninachojiuliza jee taratibu za kitabibu zinasemaje kuhusu ya kukata viungo vya mtoto mdogo kama huyu na jee nyie akizaliwa na mfupa mmoja hawezi kutembea kwamba ile mfupa hauna uwezekano wa kutembea
 
mi nashauri ufanye utafiti wa kutosha ikiwa ni pamoja na kujua kama hakuna hosp nje ya nchi zinazoweza kutibu shida hilo kabla ya kumkata mguu.
 
Pole. Nenda MOI na fanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa consent
 
ni mfupa gani anao..???
-kama mfupa alionao ni fibula(yani hana tibia) sidhani kama ataweza kutembea
-ila kama ana tibia(yani hana fibula) nadhani ataweza kutembea maana kuna watu kibao wanafanyiwa "bone grafting" kwa kuondolewa fibula na wanatembea kama kawaida tu na hata kukimbia yani wanakuwa normal kabisa
ushauri wangu jaribu kwenda hospitali kubwa zaidi na hata ikibidi hospitali za nje
 
pole sana mkuu! sijajua kiundani tatizo la mtoto wako ni lipi , ila kutokana na maelezo yako naona linafanana na hemimelia (fibular hemimelia au tibial hemimelia au fibular and tibial hemimelia)

hayo ni miongoni mwa matatizo makubwa sana katika afya ya mtoto na matibabu yake ni magumu sana,,,,,,,,,

ninaweza kurudi baadae na shule kamili ila kwa kifupi kuna option 2 za matibabu........

1. ya kwanza ni hiyo ya kukata mguu ( amputation) ili kuweza kujifunza matumizi ya miguu ya bandia katika umri mdogo , huku akibadilishiwa kila mwaka kulingana na anavyokua.

2. ni upasuaji wa mfululizo wa kurekebisha hiyo hali kila anapokua , hii ina athari nyingi sana ikiwemo deformities na maumivu ya mara kwa mara bila kusahau ni bei ghali sana na inafanyika marekani.
 
Asanteni sana lndia Ndio wameshauri akatwe na report yake tukijaaliwa salama kesho nitaiweka hapa ili madaktar muweze kuiona na kunishauri kwa sababu niliisahau ofisini tangu ijumaa kuna daktari nilimpelekea aione.
 
Sorry to say ,siamini madaktari wetu!
Sio mimi tu,hata vilaza wa CCM hawatibiwi hapo,NI ULAYA medical check ups.

India au South Africa ndio wamebobea haya,sisi tumekalia politics & udini,
 
Sorry to say ,siamini madaktari wetu!
Sio mimi tu,hata vilaza wa CCM hawatibiwi hapo,NI ULAYA medical check ups.

India au South Africa ndio wamebobea ohaya,sisi tumekalia politics & udini,
Mkuu kweli mimi nililiona hilo tukajichanga mpaka tukafanikiwa kwenda India
Wao ndo wakaja na hiyo conlusion
 
pole sana mkuu! sijajua kiundani tatizo la mtoto wako ni lipi , ila kutokana na maelezo yako naona linafanana na hemimelia (fibular hemimelia au tibial hemimelia au fibular anyyd tibial hemimelia)

hayo ni miongoni mwa matatizo makubwa sana katika afya ya mtoto na matibabu yake ni magumu sana,,,,,,,,,

ninaweza kurudi baadae na shule kamili ila kwa kifupi kuna option 2 za matibabu........

1. ya kwanza ni hiyo ya kukata mguu ( amputation) ili kuweza kujifunza matumizi ya miguu ya bandia katika umri mdogo , huku akibadilishiwa kila mwaka kulingana na anavyokua.

ii2. ni upasuaji wa mfululizo wa kurekebisha hiyo hali kila anapokua , hii ina athari nyingi sana ikiwemo deformities na maumivu ya mara kwa mara bila kusahau ni bei ghali sana na inafanyika marekani.

Nitaiweka report Kesho mkuu mpate kunisaidia coz kuna baadhi ya wakati anasimamia vitu
 
Mungu akutie nguvu mkuu.Fwatilia wataalamu mbalimbali Madr wa hospital na hawa wamitishamba

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Asanteni sana lndia Ndio wameshauri akatwe na report yake tukijaaliwa salama kesho nitaiweka hapa ili madaktar muweze kuiona na kunishauri kwa sababu niliisahau ofisini tangu ijumaa kuna daktari nilimpelekea aione.

Kaka pole sana.
 
Nina mtoto mwenye umri wa mwaka moja na busy na amezaliwa na ulemavu wa miguu yaani anamfupa mmoja kila mguu madaktar Wanasema akatwe miguu kuanzia kwenye magoti ili aanzishwe mazoezi ya viungo bandia sasa ninachojiuliza jee taratibu za kitabibu zinasemaje kuhusu ya kukata viungo vya mtoto mdogo kama huyu na jee nyie akizaliwa na mfupa mmoja hawezi kutembea kwamba ile mfupa hauna uwezekano wa kutembea
Nenda Tanga,njia ya Kwenda Mombasa Kenya,njiani upande wa Tanzania,kuna Kijiji kinaitwa Kibiboni,ukipanda bus za Dar Tanga Msa,mwambie konda akushushe hapo,yupo mtaalam,Mtanzania,ni dr wa tiba za asili(tiba mbadala wa mifupa,hapo nina uhakika tatizo la mtoto wako litakwisha.
 
India ndiko walikoshauri hivyo

Hata kama ingekuwa Marekani wameshauri hivyo, usikubaliane na huo ushauri mkuu. Mungu pekee ndo mwenye final say on whether miguu inakatwa au inabaki. Ushauri wangu do not pursue with the Doctors' option.
Rudini mbele za Mungu nae atamponya na atatembea kama kawaida. Kumbuka injili aliyoleta Yesu iliponya wagonjwa vilema wakatembea. Hakuna kisichowezekana kwake yeye aaminiye. Kama huamini nakushauri uendelee kuwasikiliza hao madaktari ila kama unaamini kuwa Mungu muumba anaweza acha kijana aje kutembea na miguu yake ikiwepo.
Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom