Kwanza labda nichangie kwa kusema kuwa Madaktari wazuri na waadilifu serikalini ni wachache mno na ni kutokana na mfumo wetu mbovu wa kiuchumi na kisiasa, ni Hospitali gani hapa Tanzania isiyo mahili kwa Rushwa? Muhimbili kumeoza wala sihitaji kuelezea, Ocean road binafsi nimetoa rushwa kwa daktari mahiri tu na bado mgonjwa wangu akafa, KCMC nako nimeshuhudia rushwa kwa bingwa mzimaaa na ndipo mgonjwa akapewa Respirator machine baada ya kutoka Operation room, (fikiria nini kilitokea kwani machine hiyo ilizimwa toka kwa mgonjwa mwingine) Ukweli rushwa na hospitali zetu ni kama uji na mgonjwa na kama humpendi mgonjwa wako basi acha kuwapa chochote/CCD uone moto utakavyokuwakia, Mifano hai ninayo mingi lakini tuachane na hilo turudi kwenye hoja zako nilipoweka red, Nafikiri wewe ni daktari na ningependa nikuulize kama upo Monduli na umegundua mgonjwa wako ana Ca basi unataka kutuaminisha kuwa hawezi kuwa referred KCMC? Mbona Temeke hupeleka wagonjwa wao wa Cancer Muhimbili kwanza halafu Muhimbili ndio huwapeleka Ocean road,(Naamini unajua kwa nini huwa hivyo) tafadhali acha uongo kuwa mkweli na hata huyo naye Dr Israel mie namwona na makosa mawili tu ambayo ni ya kitaaluma/Medical ethics, moja kama kweli mgonjwa alikuwa na kansa je kwa nini Dr Israel ashindwe kutoa Palliative care hapo Mt Meru mpaka hapo nduguze watakapokuwa tayari kumhamishia KCMC au Ocean road? hivi kweli hujui kuwa Daktari hapaswi kumtoa mgonjwa wadini mpaka hapo mgonjwa atakaposema amepata nafuu? au ndio yaleyale ya kunyanyasa wagonjwa na kusahau kuwa muda wote madaktari mnapaswa kunyenyekea wagonjwa wenu pasipo kuonyesha dalili yoyote ya ku solicit rushwa, Pili Dr Israel haku- handle vizuri mgonjwa wake kwa kutokumuambia ukweli mgonjwa na nduguze..truth telling, kama alikuwa anafanya non voluntary Euthanasia then is fine vinginevyo alipaswa kukaa na mgonjwa/nduguze na awape elimu tosha na nafikiri wangemuelewa na ndugu Mvumbuzi asingeliweka hapa complain zake na kuwaita wauaji, Dr Chichi jaribuni kwenda na wakati la sivyo si mbali sana mtajikuta mnashitakiwa kila mara kwa kushindwa kutimiza wajibu wenu ulioandikwa vizuri tu ndani ya medical ethics, mnatakiwa mshukuru watu kama Mvumbuzi ni wengi japo mie naona ilikuwa ni haki kabisa huyo Dr Israel kushtakiwa pamoja na kwamba bado ni intern bado ingefundisha na wengine kuwajibika kwa wagonjwa ipasavyo