Kindokomile
New Member
- Sep 9, 2022
- 1
- 0
MADALALI WA VYUMBA MAJUKUMU YAO KUSIMAMIWA NA MWENYEKITI WA MTAA ILI KUPATA SULUHISHO LA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA MADALALI PAMOJA NA WATEJA WAO KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.
Madalali ni watu ambao wanarahisisha shughuli za mahitaji ya watu kwa urahisi kwa kuwa daraja baina ya mwenye Mali na mnunuzi kwa gharama zenye makubaliano Kati yao wahusika wenye Mali, Changamoto inayokuwepo ni kwamba malipo ya kazi muda mwingine yanaweza yasilipwe au kulipa nusu kutokana na matatizo tofauti tofauti, Kuna madalali ambao wamesajiliwa na ambao hawajasajiliwa, Mara nyingi wasiosajiliwa ndo huaga na matatizo mengi Sana Kama vile kupangisha wapangaji wawili sehemu moja au kumdhulumu mpangaji au kuchukua hela ya udalali pande zote mbili baina na mpangishaji na mpangaji.
Kumekuwa na malalamiko juu ya ulipaji wa hela ya udalali kipindi Cha hivi karibuni kuhusu hela ya udalali itoke kwa nani Kati ya mwenye eneo husika au mpangaji, swala hili liliingiliwa Hadi na Waziri wa ardhi nyumba, maendeleo na makazi wa kipindi icho Mh William Lukuvi lakini swala Hilo halikutafutiwa ufumbuzi mpaka leo, Nilivopata huu wasaa wakuandika swala kiuchumi linalozunguka jamii yangu kupitia jamii forum nikaona ndio muda sahihi wa kuliandikia swala hili utaratibu mzuri juu ya ufumbuzi wa matatizo ya madalali na wenye Mali pamoja na wapangaji Kama vile kudhueumiana, ugomvi na kukosa kuelewana lakini pia na kutokutambulika kisheria kwa madalali waliowengi.
Wazo langu juu ya hawa madalali ni kwamba kazi ya udalali iwe chini ya mwenyekiti wa mtaa, Madalali wote wanaohusika na upangishaji wanatakiwa kuwa chini ya mwenyekiti wa mtaa ambae wao ndo watakuwa Kama boss wao, endapo mtu anataka kupanga anaenda kwa mwenyekiti anakuta namba za simu zote za madalali wa mtaa ule nje ya ofisi ya mwenyekiti na kuchukua na kumpigia au kwenda kwa mwenyekiti moja kwa moja na kuomba kukabidhiwa dalali ambae atamtafutia eneo analotaka kwa uaminifu akiwa chini ya uangalizi wa uongozi wa eneo husika na kwa utaratibu mzuri wa kisheria
Hii itasaidia kutengeneza uhalali wa kazi ya dalali ambayo itajumuisha juu malipo ambayo anapaswa kulipwa kwa mujibu wa kazi anayoifanya kwa muda huo lakini pia itasaidia kwa mpangaji nae kujua anapaswa kulipa yeye au mwenye eneo na Kama no yeye anapaswa kulipa shilingi ngapi, vilevile hili swala la madalali likiwa chini ya mwenyekiti wa mtaa limaliza suala la uhamiaji haramu ndani ya nchi sababu sidhani Kama kutakuwa na mtu ambae ataingia kwenye bila kutambulika na mwenyekiti, lakini pia itamsaidia mwenyekiti kuwatambua wananchi wote anaowaongoza katika mtaa wake.
Madalali wakishaingia kwenye mfumo ambao upo chini ya mwenyekiti wa mtaa hii itawafanya nao kutambulika kiserikali lakini kwenye itawafanya wawe wanapata Hela kihalali bila dhuluma au mkanganyiko wowote ule na wateja wao, tofauti na mwanzo ilikuwa inafanyika kiholela na kufanya kuwa na matatizo mengi sana, lakini utaratibu huu ukifuatwa udalali map utakuwa Ni miongoni mwa ajira rasmi na chanzo kikuu cha kipato Kwa wananchi sababu kila siku watu wanapanga na wanauza au kununua kwahiyo utakuwa na faida kiuchumi Kwa serikali na wananchi Pia sababu watakuwa wanajiingizia kipato.
Kuna kipindi kilifikaga udalali ilikuwa imeingia kwenye Mila potofu za kishirikina, ilisemekana Kwamba huwezi kufanya shughuli ya udalali kama wewe Sio mchawi la sivyo shughuli yako itakuwa ngumu kufanyika na kupata Hela, lakini Sasa tupo katika kipindi cha kidigitali inatakiwa tuweke Mbali mambo ya kishirikina na kuchapa Kazi kama MH Rais Mama Samia aanavyosema Kazi iendelee basi iendelee Kweli bila changamoto yoyote ile.
Wazo la pili madalali wakishatambulika na serikali Kazi ifanyike kidigitali zaid kama vile katika kipindi hiki cha sensa ambacho watu walihesabiwa Kwa kutumia vishkwambi ambapo taarifa zao zinaenda moja Kwa moja makao makuu na kutambulika yeye ni nani na anaishi wapi, ndio hivyo hivyo kwenye kupangisha eneo Kwa madalali baada ya kutambulika na serikali Kazi wazifanye kupitia kishkwambi, Yani kuwe na mfumo ambao madalali watautumia pamoja na mwenye nyumba kumpangisha mtu taarifa zake za upangaji ziingizwe kwenye kishkwambi na kufika serikalini na kutambua Kwamba mtaa Fulani Kuna mtu amehamia na amehamia na nani na anafanya shughuli gani, hii itasaidia Pia kuondoa kupangisha watu wasiojulikana na wahamihaji haramu ambao wanaweza wakasababisha madhara katika eneo husika.
Hitimisho kuhusu swala madalali ikifika hatua ya madalali kutambulika na kutumia teknolojia hiyo ya kishkwambi kupangishia wapangaji mwisho ni kuwa uhalali zaidi kwa kuwatengenezea vitambulisho ambavyo vitawatambulisha na kujulikana Kwamba ni wakina nani na wanafanya shughuli hiyo kiuhalali bila tatizo lolote na kuendelea kujenga uaminifu Kwa wananchi lakini Pia baada ya hapo ila sio kwa umuhimu serikali itenge bajeti iwapeleke shule watu wote wanaohusika na udalali hapa nchini Tanzania ikiwezekana iiingie kwenye mfumo wa elimu na ajira hapo baadae Kwa kwetu hapa nchini Tanzania.

Upvote
0