Madam Rita ateseka siku 365 Muhimbili

Madam Rita ateseka siku 365 Muhimbili

madame!!! ulienda kipindi cha mgomo nini?
 
Lazima tujivunie Tanzania yetu licha ya matatizo mengi yanayotusibu, mjenga nchi ni mwananchi.
 
Mmh mwenzio kuna kipindi nilikuwa nachambwa mmh had naipata fresh, nilikuwa sijawazoea watu wa humu vizur, sasa ivi we hii namba nyingine ukilianzisha utajuta kujifahamu na kiduku juu

Binamu uwe unatembelea na majukwaa mengine kama siasani eee sawaa
 
Kuna nn uko, kila mtu ananiambia niende, mi majukwaa mengine sijayazoea kabisa sijui naonaje

Uwe unaenda hata kusoma tu kuna watu wanachambwa hukooo wewee achaa kule ni ccm na chadema bas kuna michambo balaaa
 
Madaktari na walimu wakianzisha mgomo wa nyongeza ya mshahara mnakuja hapa kuwatetea lakini hawa watu hakuna kazi yoyote ya maana wanayoifanya..., wanakula pesa za bure na utendaji zero.

Kama kuna ufuto make sure una delete hii post yako
 
Tatizo ni hela tuu mtu uende kutibiwa Muhimbili kweli? Pale labda huduma ya kwanza...

Au mmesahau mtu alikuwa afanyiwe operation ya Mguu akafanyiwa ya kichwa yule wa kichwa akafanyiwa ya Mguu, matokeo yake mtu anafanyiwa operation mbili. Afu Mganga mkuu anadunda tu ofisini.


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Siaamini hii story kabisa..fracture yoyote ya kwenye mguu hapo MOI hata mwanafunzi wa mwaka wa tano udaktari anaweza kuigundua..hawa global publisher wana tatizo na muhimbili..
 
Sidhani pale moi kabisaa washindwe kuona mfupa uliovunjika??
Kuna kitu na hawa global publisher..watu tunafanya diagnosis hapa jf doctor na watu hatuwaoni ndo iwe machief wa MOI there something fishy..na huyu mama hii mara ka ya tatu hivi anailalamikia MOI
 
Mi siamini kama muhimbili moi walimiss hiyo fracture akafungue kesi kama kweli usikute yeye mwanyewe alikata ushauri wa kifanyiwa x ray wabongo ni wajuaji w kila kitu ndio maana mi huwa mtu akikataa ushauri ninaompa huw namwambia asile the better option aonayo yeye na si mi kufanya anavyotaka yeye
Fracture zote za mguu hata md5 anadiagnose alafu anasema MOI waliimisi..huyu anamatatizo...alafu hii swala la kulalamika lalamika nmemsikia tangu mwaka jana..
 
attachment.php


Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Productions inayoendesha shindano la kusaka vipaji vya muziki, Bongo Star Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ amesimulia mateso aliyopitia takriban mwaka sasa (siku 365) baada kuvunjika mguu mwaka jana alipopata ajali ya gari katikati ya Jiji la Dar.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum hivi karibuni aliponaswa na gongo linalomsaidia kutembea, Madam Rita alisema kwa kusikitisha kwamba, baada ya kupata ajali alitibiwa kwenye Hospitali ya Muhimbili lakini madaktari walimwambia aliteguka tu kumbe alikuwa amevunjika mfupa.


“Nimepitia mateso makubwa. Mwaka jana baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu nilipopelekwa Muhimbili waliniambia nimeteguka tu, na wakaamua kunifunga hogo ambalo baadaye walinifungua na kuniambia nimepona,” alisimulia Madam Rita na kuongeza:


“Baada ya pale nilianza kujiachia hata niliposikia maumivu na kuwaambia walisema niukanyagie tu kwamba hali hiyo ingebadilika kwa sababu ulielekea kupona, kumbe nilikuwa nimevunjika kabisa mfupa na kama ningejua siku nyingi hata nisingejiumiza kiasi hicho.


“Ujue baada ya kuambiwa hivyo, nilishangaa kuona maumivu yanazidi, nikaamua kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuuangalia zaidi mguu wangu kwa sababu maumivu yalikuwa yakiongezeka kila siku.

“Nilikwenda kwenye Hospitali ya Morning Site ya Afrika Kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na kugundulika nilivunjika mfupa na kwamba tayari nilipokuwa nikitembea ilikuwa ikipandiana.

“Ona sasa nilivyoteswa na mguu huu maana ajali nilipata mwaka jana na huu upasuaji nimefanyiwa mwaka huu Afrika Kusini.


“Kiukweli hospitali zetu saa nyingine zinatusababishia shida ambazo siyo za lazima maana kama awali wangenifanyia upasuaji wakati nawaambia ninaumia baada ya kunitoa hogo, basi leo ningekuwa nafanya shughuli zangu.


“Naona bora pale Fame Centre (Dar) maana wao waligundua tatizo na kunishauri kwenda Sauzi ambapo nimefanyiwa upasuaji na mguu unaelekea kupona kwa sababu mwanzo nilikuwa natumia magongo mawili lakini ona leo ninajikongoja kwa gongo moja ambalo nalo si muhimu sana sasa.”

attachment.php


Habari ya Hisani ya GLobal Publishers TZ

MY TAKE:
Huyu Mama alikuwa na uwezo wa kwenda Afrika ya Kusini kwa Uchunguzi zaidi na ikabainika kuwa Madaktari wa Muhimbili walikosea. Mtanzania masikini asiye na uwezo wa kwenda kuhakiki afya yake nje ya nchi ana wakati mgumu sana.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mapendo,
TANMO.

nan anamla huyu madam?

Analiwa na data
 
hiyo picha nyingine ya kimashauzi si ya kiugonjwa!!
 
Back
Top Bottom