Madam Ritha wa BSS Kufilisiwa

Madam Ritha wa BSS Kufilisiwa

Rogart Ngaillo

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
908
Reaction score
1,911
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kushirikiana na Kampuni ya Udalali ya Yono,
wameifungia Kampuni ya Benchmark Productions na kuipa muda wa siku 14, iwe imelipa deni la kodi ya Sh bilioni 7.4, vinginevyo mali za kampuni hiyo zitauzwa kwa mnada.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Meneja Msaidizi wa Madeni wa TRA, Mkoa wa Kinondoni wa Kodi, Sylver Rutagwelera alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuidai kampuni hiyo inayomilikiwa na Rita Paulsen kwa muda mrefu bila kulipa.


Source:Habari leo
 
Yule Jimama mpenda Vijana kafulia sasa hiv antangaza AZAM tv Reality Show dah aisee hapa kazi Tu hakuna kukwepa Kodi hawa angalii Sura
 
Pole sana madam umewainua watu mpaka sasa wengine ni mamilionea,sasa wewe leo upo katika hatari ya kufilisiwa! Kosa lako limeanzia wapi? Nadhani pale ulipoamua kuhamisha bss yako kwa mbwembwe kwenda kuleee!!!
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), kwa
kushirikiana na Kampuni ya Udalali ya Yono,
wameifungia Kampuni ya Benchmark
Productions na kuipa muda wa siku 14, iwe
imelipa deni la kodi ya Sh bilioni 7.4,
vinginevyo mali za kampuni hiyo zitauzwa kwa mnada. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam
Meneja Msaidizi wa Madeni wa TRA, Mkoa
wa Kinondoni wa Kodi, Sylver Rutagwelera
alisema wamefikia hatua hiyo baada ya
kuidai kampuni hiyo inayomilikiwa na Rita
Paulsen kwa muda mrefu bila kulipa.

Source:Habari leo
Inawezekana tangu aanze biashara zake hakuwahi kulipa kodi, serikali ya awamu ya nne bhana duh ilikuwa janga la taifa
 
Awamu iliopita kulipa kodi ilikua ni option sio lazma teh
Sasa hatakama,
lakini kwanini wasimdai muda mfupi tangu deni lipo dogo?
Au walikuwa wanasubiri waje wamfilisi? Huku si ni kurudishana nyuma?
 
Sasa walikuwa wapi muda wote huo mpaka deni linakuwa kubwa namna hiyo??



Si unajua zama hizo za figisufigisu, ukitoa kitu kidogo faili linasogezwa kushoto halafu mtu "anachekelea" kwamba yeye ni master, huwa halipi kodi kumbe anajitekenya na kucheka mwenyewe, faili liko palepale! Sasa limefufuka, mtu Puresha puuu!
 
Nilisikia alikatwa mguu? Sasa mlemavu anadaiwa kodi? Hana msamaha? Au mpaka wahindi na wazungu? Tunammiss Mramba
 
Back
Top Bottom