Madam Ritha wa BSS Kufilisiwa

Madam Ritha wa BSS Kufilisiwa

Kikwete alifanya watu wengi sana waishi kimagumashi hapa mjini na ndiyo maana aliwatahadharisha kuwa watanzania mtanikumbuka mie. Kwa vyovyote vile katika hali ya kwaida, Maadam Rita lazima atakuwa anamchukia Magufuli na utawala wake kwa sababu hataki kulipa kodi bali anataka kuendelee kuishi kimagumashi kama zama za Kikwete. Uncle Magu lete heshima nchini baba yake, ulipaji kodi ni muhimu kwa kila mwananchi duniani, why NOT Tanzanians?
 
Si unajua zama hizo za figisufigisu, ukitoa kitu kidogo faili linasogezwa kushoto halafu mtu "anachekelea" kwamba yeye ni master, huwa halipi kodi kumbe anajitekenya na kucheka mwenyewe, faili liko palepale! Sasa limefufuka, mtu Puresha puuu!
Kama kweli Rita alikuwa anatoa rushwa ili asilipe kodi basi imekula kwake, hii ndo ile wanaiitaga SHORTCUT IS THE LONG CUT
 
Sasa deni bil 7.4 hizo Mali ni za bei gani? Kama mimi uzeni tu ntafungua nyingine kwa Jina lingine na ntaendelea kupiga mzigo kawaida
 
Billion sio shida binafsi nimeanza kuisimua benchmark muda mrefu sana na production sio biashara ya ubuyu ni serious money rotation ndio uhusika pale
 
Dah huyu nafasi yake kwa machache alichezea saa hizi angekua anakaa zake Dubai
 
Wao walikuwa wapi mpaka deni likawa kubwa ivo. Hao nao washughulikiwe.
Huwa mara nyingine kunakuwaga na makubaliano baina ya maafisa wasio waaminifu na mlipa kodi mahesabu yanafanyiwa mafelmeee, ukija ukaguzi mwingine unakuta kuna deni kubwa kuliko lile ambalo lilifanyiwa assesment na mfanyakazi mpiga dili.
 
Hongera TRA,
Naomba kuuliza: ni mdaiwa gan ambae wameshamfilisi mpaka sasa,
Vipi kuhusu mkono advocates , aliwalipa? ?
 
Mara nyingi sis watanzania tunashabikia habari zisizo na uhakika kabisa...., zile habari za kudhalilisha MTU au mwana jamii aliye na nafasi zaidi kuliko sisi kifedha au kitaaluma, au kidhamana ...
Tena bila kufikiri sawa sawa ..., bila kupima ukweli au uhalisia wa mambo yanayosemwa, utakuta mtu mzima anachangia kabisa kwa hisia ..., huku akionyesha chuki ya wazi wazi kwa anayesakamwa , na kumbe hata maskini ya mungu hamjui kwa sura wala kwa lolote anayesakamwa ...

Sasa tujiulize, hivi habari hii iko sahihi ...?! Ni kweli huyo Dada ana pesa kiasi cha kuweza kutakiwa kulipa kodi ya Billion 7 ..???!
Kwa mtu mwenye akili huwezi kuamini habari hii haraka haraka bila kusikiliza upande wa pili ...

Yaani huyu mama kweli anaweza kuwa ana worth 50 Billion kweli ... ????! Kwa biashara ipi ...??!
Hebu wana habari tutafute ukweli wa jambo hili ....

Acheni utani na pesa nyie watu ...!
 
tunamkaribisha kwenye kundi letu la mashetani ambalo jpm alikuwa analihubili "NATAKA NAO WAANZE KUISHI KAMA MASHETANI"
 
Back
Top Bottom