Mara nyingi sis watanzania tunashabikia habari zisizo na uhakika kabisa...., zile habari za kudhalilisha MTU au mwana jamii aliye na nafasi zaidi kuliko sisi kifedha au kitaaluma, au kidhamana ...
Tena bila kufikiri sawa sawa ..., bila kupima ukweli au uhalisia wa mambo yanayosemwa, utakuta mtu mzima anachangia kabisa kwa hisia ..., huku akionyesha chuki ya wazi wazi kwa anayesakamwa , na kumbe hata maskini ya mungu hamjui kwa sura wala kwa lolote anayesakamwa ...
Sasa tujiulize, hivi habari hii iko sahihi ...?! Ni kweli huyo Dada ana pesa kiasi cha kuweza kutakiwa kulipa kodi ya Billion 7 ..???!
Kwa mtu mwenye akili huwezi kuamini habari hii haraka haraka bila kusikiliza upande wa pili ...
Yaani huyu mama kweli anaweza kuwa ana worth 50 Billion kweli ... ????! Kwa biashara ipi ...??!
Hebu wana habari tutafute ukweli wa jambo hili ....
Acheni utani na pesa nyie watu ...!