Madam Ritta umeizika Bongo Star search (BSS)?

Madam Ritta umeizika Bongo Star search (BSS)?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wana Jamvi wasalaam!
Happy New year 2015.
Allah ni mwema wakati wote!

Wana jamvi bila shaka kila mtu analikumbuka shindano la kusaka vipaji vya waimbaji maarufu kama Bongo Star Search (BSS)! Nilitegemea kuliona hili shindano mwaka uliopita lakini sijaliona na sijui kumetokea nini hadi mwaka 2014 lisiwepo?

Mbali na kuwasaidia vijana kuibua vipaji vyao na kuwa kama daraja lao la mafanikio ya vijana walio shindwa kupata nafasi, lakini limekuwa likitupa burudani watazamaji na mashabiki wa muziki!

Bado najiuliza kumetokea nini shindano hili kukosekana mwaka uliopita? Madam Ritta ameamua kuachana nalo? amekosa wadhamini? ameshindwa kuliendesha tena?

Ningependa kuona shindano hili linarudi maana linawasaidia sana vijana!

Karibuni wana jamvi!
 
Labda ameamua kukoboa na sio kusaga tena vipaji....hata mie nimelimiss!!!!

Mimi tangu shindano liamie TBC nilipata shaka na uhai wake na pia lilianza kupoteza umaarufu kabisa! Sasa sijui nini kimetokea mwaka jana halijaonekana kabisa!
 
RIP BSS...
Zantel nao wamepiga chini?
 
Toka Mzee Machache ajitoe lilianza kulegalega kiaina hivi
 
Mengi kampiga chini kakosa hadi udhamini!!!

NJE YA MADA:hivi haya mashindano kwanini huwa lazima kuwe na jaji mwenye makuzi kama Salma kwa bongo,Kate Henshaw(Nigeria got talents),Simon (British got talent),yniaani hawa wanafana kila kitu kuponda na kukatisha tamaa,sielewi kwanini majaji wengi wa mashindano ya aina hii lazima kuna mmoja ni mnoko,Simon ni mnoko sana,Kate Henshaw anavyojibu yaani afadhali hata Salma Jabir,Salmar mwenyewe mapozi na majibu ya haja,kwanini hawa majaji baadhi lazima wawe umiza kichwa!
 
alisema litarud mwaka huu wanajipanga zaid ndo mana mwaka jana halikuwepo
 
Mengi kampiga chini kakosa hadi udhamini!!!

NJE YA MADA:hivi haya mashindano kwanini huwa lazima kuwe na jaji mwenye makuzi kama Salma kwa bongo,Kate Henshaw(Nigeria got talents),Simon (British got talent),yniaani hawa wanafana kila kitu kuponda na kukatisha tamaa,sielewi kwanini majaji wengi wa mashindano ya aina hii lazima kuna mmoja ni mnoko,Simon ni mnoko sana,Kate Henshaw anavyojibu yaani afadhali hata Salma Jabir,Salmar mwenyewe mapozi na majibu ya haja,kwanini hawa majaji baadhi lazima wawe umiza kichwa!

Majudge aina ya Salma wanachangansha shindano pamoja na washiriki
 
Nimemiss sana vituko na burudani ya BSS,ni shindano zuri la kusisimua.Madame afanye mpango lirudi sasa,tena ITV sio Tbc1 ya wazee.

Hawezi kulirudisha ITV tangu Machache achepuke na miss Tz uhusiano wao kushneh
 
vipindi vyote vikishahamiaga tbc ndo vinakaribia kukutwa na umauti....ile ni tv ya wazazi sio vijana, angalieni mboni show itavyofwariki soon.
 
vipindi vyote vikishahamiaga tbc ndo vinakaribia kukutwa na umauti....ile ni tv ya wazazi sio vijana, angalieni mboni show itavyofwariki soon.

Hapo Mboni kapotea njia bora ange kwenda Clouds TV! tafiti zinaonesha vipindi vinavyo kwenda TBC hufa taratibu!

Tatizo hawa wenye vipindi wakipandishiwa gharama za kurushwa vipindi vyao wanafikiri ni ugomvi!

Nasikia hata Madam Ritta walimpandishia gharama za kurusha kipindi akaona aende TBC bila kuzingatia biashara za wadhamini wa kipindi!

Pengine mtu anaweza kupoteza wadhamini kwa kwenda kituo ambacho wadhamini wanajua hawatapata watazamaji wengi!
 
ZANTEL yenyewe maji ya shingo..

Zantel wangepata wateja wengi kama shindano linge onekana ITV maana kuna watazamaji wengi ukilinganisha na TBC
 
Back
Top Bottom