Tetesi: Madaraka ni dhamana ya muda mfupi sana. Je, Lukuvi kumpiku Majaliwa?

Tetesi: Madaraka ni dhamana ya muda mfupi sana. Je, Lukuvi kumpiku Majaliwa?

Nimeuliza ili kupata majibu baada ya tetesi kunifikia, naomba mwenye kujua zaidi atueleweshe.

Na wala haishangazi, hii ni kwa vile uongozi ni kama mbio za kupokezana vijiti, anayeanza siyo anayemaliza.
Haiwezekani. Majaliwa amejaliwa Kubiaki kama Waziri Mkuu
 
😂😂😂😂kwenda kuwa rais wa kuongoza nini na kutetea maslahi ya nani na wapi?
Rais: Insta, FB, 'Twira,' YT, JF & Ufipa FC

Maslahi: mashujaa wa kiibodi plus nyomi ya kuediti na kura zao za kubumba
 
Lukuvi na Majaliwa hawapishani kiutendaji but Lukuvi ni harsh zaidi, Kwa vile ni swahiba wa muda mrefu wa mkuu, huenda akamwachia kiti 2025 so lazima awe kwenye better position, istoshe Lukuvi yupo aware Sana na miradi mizito ya mkuu ambayo kimsingi hata 2025 haitakuwa imekamilika.

Hivyo ili ikamilike inahtaji atayepokea kijiti awe more experienced kwenye serikali kitu ambacho majaliwa anakosa lakni Lukuvi anacho. Lakn mkuu ulidai Lissu asipoapishwa bas ndo mwisho wa tz, vip mbna thread zako zinaonyesha tz inasonga mbele?
Majaliwa ni sawa na UPEPO tu but Lukuvi ni mtendaji mzuri tu

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Majaliwa ni sawa na UPEPO tu but Lukuvi ni mtendaji mzuri tu

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Wote ni watendaji makini bila hata cheche yoyote ya mashaka. Majaliwa ni mzuri sana kwenye "clearing & fowarding" (ni msafirishaji, msafishaji, mnadishaji na mfikishaji mzuri sana wa ajenda kuu za kitaifa kwa umma); halafu ni 'konekta' na mleta-watu pamoja. Majaliwa ni FOREMAN.

Lukuvi ni "detail follow-up person & meticulous executor" --- zile minute na hidden technicalities zote yeye ni mbobezi. Huyu ni mjuzi na fundi wa paper work, na anamudu sana, na hapa ndipo eneo lake la kujidai. Lukuvi ni FRILL-MAN (analyzer).
 
Chadema ukianza kudiskasi mambo ya sisiemu wakati huamini ushindi wao ni ushahidi kuwa sasa mambo yanakwrnda vzr na mmeelewa kuwa hakuna wizi
 
Yoyote atakaechaguliwa kwa nafasi za wizara Awamu hii ni KAZI KAZI hakuna excuse, asilimia kubwa ya wabunge na madiwani wanatoka chama tawala na hii itawasaidia sana kwenye utendaji.

Naiona CONNECTION nzuri kati ya serikali yaani mawaziri na wawakilishi wa wananchi.

Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wakitumia wataalamu katika sehemu zao, na wakashirikiana na wabunge na madiwani wao vizuri watamsaidia sana rais katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea watanzania maendeleo.

Tufike mahala rais anapopita kwenye maeneo yetu tuone akipewa pongezi zaidi ya yale malalamiko ya wananchi kukosa huduma au kukosa wa kuwasikiliza.
 
Majaliwa anafaa sasa kuwa Waziri wa Ulinzi achukue nafasi ya Mwinyi. Uwaziri mkuu apewe mtu anaeuweza
 
Uliandamana kuunga juhudi za Viongozi wako?
Je baada ya kupigwa kipingo Cha Mbwa Koko kwenye uchaguzi huu umechukua hatua zipi?

Vipi wale wabunge wako uliokuwa unatumia nguvu kubwa kuwatangaza watashida hapa Jf wataapishwa lini? (Likiwemo Jimbo la Mbarali)

Narudia Tena nyie makamanda wa jf Ni wanafiki tu hamna faida ndani na nje ya Chama.
Kwa taarifa yako ni kwamba kwenye uchaguzi huu hakuna kura yoyote iliyopigwa na wananchi iliyohesabiwa , matokeo ya kila jimbo yalipangwa wiki 2 kabla ya uchaguzi , Kwa mfano , Jimbo la Hai matokeo yalitangazwa usiku wa manane huku hata masanduku mengine ya kura yakiwa hayajafika kwenye majumuisho , Masanduku yalikamilika kufikishwa kwenye kituo cha majumuisho saa 2 asubuhi , huku tayari matokeo yakiwa yametangazwa .

Jimbo la Temeke karibu vituo vyote vya kupigia kura ilibandikwa kuwa Lissu kapata kura 19 , vituo vyote ni 19 tu , sasa hata kama huna akili timamu hata hili hukuliona ? ilitajwa wiki moja kabla ya uchaguzi kwamba Tume ilimuandalia Magufuli kura mil 12 , hakuna aliyekanusha , na ikawa hivyo hivyo , haya yote hukuyaona ? Nafahamu unachotaka tukifanye ili ujue hatukuridhika , na bila shaka utakipata , Stay Tuned
 
Nimeuliza ili kupata majibu baada ya tetesi kunifikia, naomba mwenye kujua zaidi atueleweshe.

Na wala haishangazi, hii ni kwa vile uongozi ni kama mbio za kupokezana vijiti, anayeanza siyo anayemaliza.

Nadhani atampa Prof Palamagamba Kabudi uwaziri mkuu.
 
Sasa nafurahia naona mmeshapunguza machungu..haya ya kufitinisha ni ya kawaida tuu.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi

CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Nimeuliza ili kupata majibu baada ya tetesi kunifikia, naomba mwenye kujua zaidi atueleweshe.

Na wala haishangazi, hii ni kwa vile uongozi ni kama mbio za kupokezana vijiti, anayeanza siyo anayemaliza.
Majaliwa Kassim Majaliwa anatosha!
 
Back
Top Bottom