Madaraka ni dhamana ya muda mfupi sana, kutoka kupigiwa magoti hadi kusindikizwa nje ya Ikulu

Ni muhimu kupata katiba mpya kwa sababu mambo yote kuhusu haki na miongozo mbalimbali itakuwemo , Masuala ya Ma DED kuwa wasimamizi wa uchaguzi yatafutiliwa mbali , ndani ya Katiba mpya mtaondoa makada wa ccm kuwa viongozi wa Tume ya uchaguzi
 
Watanzania sio wapole..ni bahati mbaya tu kwamba asilimia kubwa sana ni wanafiki na waoga. Binadamu wengi ambao wanahisiwa kuwa wapole sio wapole bali ni wanafiki au waoga. Na unafiki huzalishwa na uoga. Hakuna muoga asiyekuwa mnafiki na hakuna mnafiki asiyekuwa muoga...hata serikali inakabiliwa na tatizo hilo ...
 
Hakika .
 
Ndio maana tunataka Katiba mpya ili hawa mamluki wanatufanya tuendelee kuumia wasipate upenyo
 
Mkuu 'Mazindu Msambule', umeandika vizuri sana, lakini umesahau kitu kinachotutofautisha sisi Tanzania, na hao wengine.
CCM, CCM, CCM..., ipo kila mahali, mahakamani, Bungeni, Jeshini, Usalama (wa CCM), Tume ya Uchaguzi, Mitaani tunakoishi, kila mtaa kuna CCM inayohakikisha ni wao tu ndio wenye kuamua kila kitu.

Katiba yetu ilivyo, mtu wa CCM ambaye ni Mwenyekiti na rais wa nchi, yupo juu ya katiba hiyo, anaamua kama 'mungu' hatma ya waTanzania wote.

Mimi sijui kama huko Zambia na kwenyewe kuliwahi kuwepo chama chenye muundo kama wa CCM kikiambatana na Katiba kama tuliyonayo sisi.
 
Naomba nikustushe/kukumbushe.

Uliwahi kumsoma mtu anayejulikana kwa jina la 'Iboya' hapa JF?

Hii ndiyo timu mpya na mambo mapya!

Hebu angalia #9 hapo juu.
ni miongoni mwa watu duni niliowapuuza kabisa hapa jf , kwanza siamini kama ana ubongo
 
Kuna mwingine hapa walianza kumwita hadi Mungu... huku yeye alichekelea.
 
Nakubaliana na wewe. Na viongozi wa CCM walishauona huu udhaifu ndiyo maana hawaogopi. Uchaguzi wa 2020 ulivyokuwa wa hovyo na ujambazi wa wazi, ingekuwa nchi nyingine Magufuli asingefia madarakani. Ila katiba ikiandikwa upya na izibe loopholes za wizi wa kura kadiri iwezekenavyo, mambo yanaweza kubadilika. Tatizo ni kuwa CCM hawatakubali kwa sababu wanajua itawaweka kwenye wakati mgumu.
 
Bro you speak it....that fact! watanzania hawajajua tatizo ni sisi wenyewe
 
Acha kudanganya katiba Zambia ilibadikishwa kabla Kaunda hajatoka madarakani!
 
Ni muhimu kupata katiba mpya kwa sababu mambo yote kuhusu haki na miongozo mbalimbali itakuwemo , Masuala ya Ma DED kuwa wasimamizi wa uchaguzi yatafutiliwa mbali , ndani ya Katiba mpya mtaondoa makada wa ccm kuwa viongozi wa Tume ya uchaguzi
tume ya uchaguzi inafumuliwa inaundwa upya vipi bado unataka katiba mpya?
 
tume ya uchaguzi inafumuliwa inaundwa upya vipi bado unataka katiba mpya?
Katiba Mpya ndio msingi wa Haki , kuna mambo ya kijinga ndani ya katiba ni lazima yaandikwe upya hata hii tume ya uchaguzi ipo kwa sababu ya katiba yenu mbovu , Mahera au Jecha wanaccm wasiojificha ni aibu kuongoza tume ya uchaguzi
 
Katiba Mpya ndio msingi wa Haki , kuna mambo ya kijinga ndani ya katiba ni lazima yaandikwe upya hata hii tume ya uchaguzi ipo kwa sababu ya katiba yenu mbovu , Mahera au Jecha wanaccm wasiojificha ni aibu kuongoza tume ya uchaguzi
nyie kinajulikana mnachotaka kibadirishwe hapo ni kwenye tume tu yaani hayo mengine wala hivi ukiulizwa sehemu gani nyingine unataka ibadirishwe utasema ni wapi? inawezekana hata katiba yenyewe huijui vizuri mnauchu wa madaraka sana mbona ya kwenu mmeshindwa kuiboresha mpaka mwenyekiti anajiamria aondoke lini kwenye madaraka? hilo hamlioni? hamna huruma na raia wa tanzania mna uchu wa madaraka
 
Tunataka serikali tatu; serikali ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar na serikali ya Muungano. Tunataka viti maalum vifutwe, tunataka madaraka ya Rais yapunguzwe na aweze kushtakiwa akivunja katiba na mengine mengi.
 
Huyo sio Haichelema alikuepo ni waziri mwingine wa Edgar Lungu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…